Saa zingine nampenda Magufuli

Saa zingine nampenda Magufuli

Eti kukata tamaa, wewe unajua kinachoendelea sasa hivi kuhisiana na vita dhidi ya ufisadi? Mbona hivi majuzi mawaziri kadhaa wamekuwa summoned na DPP na DCI? Tena wakaketi mbele yao na kujibu maswali huku wakijetetea wakiwa wametokwa na kijasho? Hakuna wakati ambapo vita dhidi ya ufisadi umetekelezwa kwa nia na kujitolea kama sasa hivi. DPP Noordin Haji, DCI Kinoti na AG Kariuki wameliamsha na kitaeleweka. Kwani Echesa alifutwa kazi kwanini? Taasisi mbali mbali ikiwepo mahakama zimekomaa na kuimarika. Hatutegemei mtu mmoja.
Sasa kwanini unasingizia katiba kutompa mamlaka rais kuweza kuwafuta watu kazi wanapotuhumiwa kula rushwa au kushindwa kusimamia kazi zao?, kwa taarifa yako, katiba ya Kenya inamruhusu rais kuwafuta kazi kuanzia CS, wakurugenzi na wateule wengi tu kama akipenda, kama ambavyo alivyofanya marekebisho madogo ya mawaziri hivi juzi.

Hii lugha ya kwamba hakuna serikali iliyopambana na rushwa hapo Kenya kushinda Jubilee, hayo ni maneno ya viongozi wa Jubilee kuwahadaa wananchi, wanekua wakiyasema mara kwa mara, lakini utafiti uliofanyika hivi karibuni, Wakenya wengi hawakubaliani, wengi wanasema Uhuru Kenyatta hana nia ya dhati Wala uwezo wa kupambana na rushwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hehehe! 😀 Ndio maana thamani ya shilingi inaimarika kila uchao. Viashiria vinaonesha 'Investor confidence', 'ease of doing business' na vitu kama hivyo vinazidi kuboreka. Ugatuzi unaonesha matunda yake na marais na wawekezaji wa nchi za nje wanatiririka Kenya kila uchao. Miundu mbinu inaimarishwa. Haya yote chini ya tishio la ugaidi. Kweli rais U.K. amefeli.
Shilingi inaimarika lakini Wakenya wanaendelea kufa kwa njaa, hii inakupa picha gani?," Kenya's economy is inversely proportion with better life"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona ameenda hapo ujue ana intel zote.

Hakuna mkandarasi anayeweza kuchelewesha mradi kimaksudi, tatizo huwa pumba za urasimu serikalini halafu walivyo wavivu na mafisadi, mwisho wa siku mkulu kama ni mpenda kiki za wanahabari atakuibukia na kukuzomea zomea.
 
Hakuna mkandarasi anayeweza kuchelewesha mradi kimaksudi, tatizo huwa pumba za urasimu serikalini halafu walivyo wavivu na mafisadi, mwisho wa siku mkulu kama ni mpenda kiki za wanahabari atakuibukia na kukuzomea zomea.
Boss, wazembe nchi yetu wapo wengi Sana. Bila shuruti hawaendi.
 
Huyu jamaa hapendi mchezo,
1.Anateuwa mtu mwingine wa kuifanya Kazi.
2.Anafuta wazembe - Kesho usionekane hapa
3.Unaambiwe ueleze vile pesa zilivyotumika
4.Halafu unaambiwa mungu akubariki

😀😀😀😀


Ile level ya indicipline tunayo Afrika, inataka watu kama Magufuli. Wacha wengine waonewe lakini inasaidia kuogopa public fund.

Afrika ni aibu.
 
Back
Top Bottom