joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Sasa kwanini unasingizia katiba kutompa mamlaka rais kuweza kuwafuta watu kazi wanapotuhumiwa kula rushwa au kushindwa kusimamia kazi zao?, kwa taarifa yako, katiba ya Kenya inamruhusu rais kuwafuta kazi kuanzia CS, wakurugenzi na wateule wengi tu kama akipenda, kama ambavyo alivyofanya marekebisho madogo ya mawaziri hivi juzi.Eti kukata tamaa, wewe unajua kinachoendelea sasa hivi kuhisiana na vita dhidi ya ufisadi? Mbona hivi majuzi mawaziri kadhaa wamekuwa summoned na DPP na DCI? Tena wakaketi mbele yao na kujibu maswali huku wakijetetea wakiwa wametokwa na kijasho? Hakuna wakati ambapo vita dhidi ya ufisadi umetekelezwa kwa nia na kujitolea kama sasa hivi. DPP Noordin Haji, DCI Kinoti na AG Kariuki wameliamsha na kitaeleweka. Kwani Echesa alifutwa kazi kwanini? Taasisi mbali mbali ikiwepo mahakama zimekomaa na kuimarika. Hatutegemei mtu mmoja.
Hii lugha ya kwamba hakuna serikali iliyopambana na rushwa hapo Kenya kushinda Jubilee, hayo ni maneno ya viongozi wa Jubilee kuwahadaa wananchi, wanekua wakiyasema mara kwa mara, lakini utafiti uliofanyika hivi karibuni, Wakenya wengi hawakubaliani, wengi wanasema Uhuru Kenyatta hana nia ya dhati Wala uwezo wa kupambana na rushwa.
Sent using Jamii Forums mobile app