Sababu 5 za kifo cha CHADEMA 2020-2025

Sababu 5 za kifo cha CHADEMA 2020-2025

sainass

New Member
Joined
Jan 18, 2018
Posts
2
Reaction score
0
1. KUTOSIMAMA NA VITI MAALUM 2020 KIMKAKATI
Baada ya uchaguzi kuisha na kushindwa kwa anguko kubwa Zaid yani hakuna mbunge hata mmoja kutoka CDM alieshinda. Wakasusia matokeo ya uchaguzi na kusema hawatopeleka wabunge wa viti maalum bungeni ( hii ilikuwa kosa kwao maana Magu effects, ilikuwa kubwa kiasi cha wananchi kuwa na imani na chama tawala)

Hapo hapo wakiwa wamezubaa wakastushwa na kupelekwa kwa majina ya viti maalum bungeni 😂 Yani halima mdee, bulaya na wengine waliendelea na haki Yao kikatiba (Hatuwezi kosa vyote kwa Miaka 5, waliingia bungeni kwa shangwe na kujiamini kwenda kuendeleza mapambano) kosa walilofanya chadema nikuwaona hawa ni wakosaji badala ya kuwatumia kuwa njia mbadala wa kuifikia 2025.

Wakafanya kazi yao bila msaada wa chama Chao japo walikuwa wakilipa stahiki zote za chama.

images (1).jpeg


2. KUKOSA DEMOCRACY NDANI YA CHAMA
Nafasi ya Mwenyekiti wa chama amekalia Freeman Mboe kwa muda wa Miaka 20 ( Yani hakuna mtu ambae anaweza fit hapa Ila yeye 😂 huu ni ubinafsi wa madaraka) kama chama kinakuwa kama cha familia mmoja sasa kitawezaje kuwa na malengo ya kitaifa?

Freeman_Aikaeli_Mbowe_(cropped).jpg

Viongozi wengi wameondoka kwenye chama na kugombana na Mwenyekiti kwa kugombania nafasi ndani ya chama ambazo hazina usawa wa kidemokrasia.

Chama chenye mrengo chanya hakiwezi ongozwa na familia moja mda wote. Leo tunavyo zungumza tunaona Mwenyekiti na Makamu wake wanatofautiana kimkakati huyu anasema hivi Yule anasema hivi. Sasa inakuaje hapa? Hivi ni dalili halisi za kugawana mbao.

GcWFyNgWkAAd252.jpg


3. LACK OF FOCUS (Kutokuwa na malengo ya kudumu kichama)
Chama hakieleweki kinataka nini either katiba Mpya, tume huru ya uchaguzi au kinataka maridhiano ya kisiasa.
Ukiangalia kwa umakini kabisa hakuna focus katika hayo yote na kama vile wanatapata (kuku kakatwa shingo 😂) mwanzoni walikuwa Wana fight kuwa wanataka katiba Mpya wakapiga kelele wiki moja Kisha wakatulia, baadae walivyoona Uchaguzi unakaribia wakaongeza Tume huru na mwisho wakaja kukaa mezani na chama tawala 😂 kwenye kikao cha maridhiano ambayo hakuna mwananchi wala media ambao wanajua waliridhia nini (sasa hapa tumia akili zako) Chama hakijakaa kiukombozi kimekaa kimaslahi Tu. Huu ndio ulikuwa mvunjiko wa Kwanza kwa CDM.

4. Kuacha kuikosoa serekali hadharani sio mitandaoni
Kama kuna kosa wamefanya CDM kubwa basi ni hili, kuto chambua report na mikataba hadharani (CAG report) kufichua ufisadi na mengine mengi Hili linafanya kupoteza mvuto mbele ya wananchi (Ambao wanaitaji pande zote for check and balance)

Badala yake wanapambania Tume huru ili waje kuingia bungeni kupata mahitaji Yao binafsi
Wamesahau kuwa wananchi ndio wanaweza fanikisha katiba Mpya na tume huru ya uchaguzi badala ya kuona wanaowapigania wanakosa nafasi wakati waliwachagua. Sio wapambanie alafu nyie muende kwenye vikao vya maridhiano 😭😭😭 Yani watu waandamane Kisha nyinyi mnaenda kwenye maridhiano ambayo hata Wananchi hawayajui 😭😭😭 (Secret Agenda and Agreement)

images (3).jpeg


5. Kukosa ukachelo ndani ya chama
Kila chama kinakuwa na makachelo. Sasa chama hakina makachelo ndani ya vyama vingine. Mfano vyama 14 vimeridhia nyinyi chama kikuu kipo wapi mmeshindwa penyeza Sera na viongozi huko? Ili mkisimama mnasimama pamoya. Watu wa chama wanapotea na hata mnashindwa jua wapo wapi na ushahidi wa Nani kakamatwa na nani (hiki ni chama kweli). Huwezi kuwa mpizani alafu huna technics za kujilinda na kuwapata watu wako.

6. BONUS POINT
Kutoandaa vijana wakusimamia chama Kila wilaya na mikoa. Kama chama kitakosa vijana wenye weledi na mataifa ya kuitangaza Sera ya chama basi hicho chama kitakufa

Rest in peace CDM in advance
Kwa Leo ni hayo kama nitakuwa nimewakwanza mnisamehe ila nimewasanua Tu. Wale wafia chama msinisagie kunguni 😂 Mama Samia Mitano tena 😂
 

Attachments

  • Freeman_Aikaeli_Mbowe_(cropped).jpg
    Freeman_Aikaeli_Mbowe_(cropped).jpg
    323.9 KB · Views: 3
Back
Top Bottom