SoC02 Sababu 5 za wewe kuwepo ulipo sasa

SoC02 Sababu 5 za wewe kuwepo ulipo sasa

Stories of Change - 2022 Competition

tujuemoja

Member
Joined
Jul 26, 2022
Posts
7
Reaction score
2
Wengi tunaamini kwamba kila kitu kilichopo hapa duniani kina sababu ya hicho kitu kuwepo. Na hii Ikanipelekea kutafiti sababu zinazotufanya tuwepo katika hali tulionayo kwa sasa.

ZIFAHAMU SABABU (5)ZA WEWE KUWEPO ULIPO SASA.

01. UFAHAMU NA TAARIFA TULIZONAZO JUU YA MALENGO YAKO.
Ufahamu ni juu ya vitu vyote tunavyovifahamu katika kufikia hali fulani ya maisha. Lakini hekima ni namna bora ya kutumia ufahamu katika mazingira na wakati sahihi. Hivyo ni bora zaidi kuwa na ufahamu pia hekima ili kuweza kufikia hali bora ya maisha tunayotamani kuyaishi hapo mbeleni.

Kipindi cha ujana ni kipindi ambacho ni rahisi kupata ufahamu na taarifa juu ya mipango tuliyojiwekea, na hivyo tunapaswa kuitesa akili kipindi hiki cha ujana ili tusije tukaitesa kipindi cha uzee, ambapo mwili umechoka na maangaiko na mishughuliko tuliyoipitia kipindi cha ujana.

Taarifa na ufahamu tunaweza kupata katika mitandao ya kijamii, katika kusoma vitabu , katika kuudhulia semina mbalimbali ambazo zinaendana na matamanio yetu. Pia tunaweza pata taarifa kupitia kwa watu waliofanikiwa kufikia kile ambacho unatamani kukifikia.

02: MIHEMKO AU AKILI ZETU.
Muhubiri mmoja akiwa anahubiri, uhusiano uliopo kati ya mwili, Nafsi na roho. Aliweza kufafanua kwamba Nafsi Siku zote ipo katikati ya mwili na roho,
Na hivyo maamuzi yanayofanywa na nafsi hutegemeana na kile kilichotolewa na mwili au kilichotolewa na roho.

Ni kwamba kama nafsi itatenda isivyo itakuwa imeongozwa na mwili, Pia mwili hutegemea sana chakula kinacholishwa ili uweze kushawishi mwili kuufuata.

Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa, "Tunakuwa jinsi tulivyo kutokana na kile tunacho kula"
Kwa kutumia kanuni hii, Tunaweza kusema kuwa kile tunachokilisha mwili wetu, kwa kusikia na kuona ni matokeo yetu ya kuwepo katika hali tulizonazo za maisha.

Pia, kama Nafsi itaenenda ilivyo, inakuwa imechochewa na Matendo yaliyozalishwa na roho kutokana na kile kilichoingia katika roho kupitia kusikia na kuona.

"Roho iladhi lakini mwili ni dhaifu" Roho inasimama upande wa Kuongozwa na akili yenye hekima ya kiungu na mwili husimama upande wa kuongozwa na mihemko au matamanio ya mwili.

Angalia mfano huo hapo chini.
Kwa mfano. Hauna huhitaji wa nguo wala mpango wa kununua nguo katika kutembelea kwako sokoni, na katika kuzunguka kwako unakuta sharti nzuri ambayo ukatamani kuwa nalo , lakini akili inakukatalia kufanya maamuzi ya kununua sharti hilo, maana hauna huitaji wa nguo na pili mipango yako haikutaki kununua japokuwa una fedha za kukidhi kununua hilo sharti.

Katika hali hiyo itategemeana hasa na Kuongozwa na akili au mhemko katika kufanya maamuzi,
Pale unapoamua kununua , unakuwa umeendeshwa na mihemko na pale unapoacha kununua kutokana na hauna huitaji wala mpango hapo unakuwa umetumia akili katika kufanya maamuzi.

Wengi wamejikuta wakiishi maisha ambayo ni magumu kwao kutokana na mawazo ya mihemko waliyoyaamua hapo Nyuma.

Sifa za mawazo ya mihemko ni kwamba inaongozwa na tamaa, na hivyo huenda kinyume sana na kile ulichokipanga ndani ya akili yako. Na wengi wamejikuta wakiumia na kuwa watumwa kwa vitu ambavyo hawajapanga akilini mwao.
Lakini tamaa , kujilinganisha na kushindana kumewafanya wavitumikie. Mfano kuwa mtumwa wa mitindo mipya ya mavazi n.

03: MITAZAMO YETU.
Mtazamo ni hali ya kuelewa na kutafsiri mambo mbalimbali.
Hali yetu ya maisha kwa sasa inapelekewa sana na namna tunavyo tafsiri mambo mbalimbali katika maisha yetu.
Hali ya kuwa na tafsiri chanya au hasi hutegemeana na kile tunachokilisha ndani ya bongo zetu.

Ubongo unalishwa kupitia milango mitano ya fahamu, hususani katika macho na masikio.

Hivyo tunaujasiri wa kusema mtazamo wako unategemeana na kile unachotazama au kuona na kile tunachokisikia au kusikiliza.

Wengi ambao huwa katika hali bora ya maisha hupenda kulinda ubongo wao kwa kusikiliza na kuona vitu sahihi kutokana na malengo na matamanio yao.

Pia, kwa upande wa watu ambao hushindwa kulinda ubongo wao kwa kuingiza vitu ambavyo ni sumu katika ubongo na hivyo upelekea kuwa na mtazamo hasi.

Tunaamini kuwa mtu mwenye mtazamo chanya Mara zote hutafsiri shida na changamoto zinazomkabili , kama fursa mpya mbele yake na hivyo huwaza kubuni mbinu mbadala wa kukabiliana na changamoto hizo.

04: ADUI ZAKO.
"Kama tungeumiza wanaotuumiza, kama tungelipa visasi , kama tungewachafua wanaotuchafua, kama tungewapiga wanaotupiga, Hakika tusingefika hapa tulipo.

Niligundua kuwa hali yangu ya maisha kwa sasa inatengenezwa na maadui zangu.
Adui zangu unipa changamoto ambazo zinanifanya nifikiri zaidi yao na kupiga hatua katika maisha yangu, na hivyo nina ogopa sana kukaa mahali ambapo sina maadui.

Hamini kuwa katika eneo unapoishi ukiwa na watu wanaokuunga mkono katika kila jambo na hawajawahi kukukosoa tambua kuwa haupo sehemu salama.

Hivyo ni wazi kusema kuwa akili inapata kufikiri zaidi pale inaporuhusu changamoto izikabili, hivyo ni kuduma kifikra unaporuhusu kukaa mahali ambapo hakuna maadui wa kukupa changamoto.

Adui ni mchambuzi na mkosoaji wa maisha yako, hivyo tunapaswa kuwapenda na kuwaombea sana, maana utupatia changamoto katika kile tunachokifanya.

Kama wewe ni mfuatiliaji wa mpira utakubariana na mimi kuwa sayansi ya mpira inasema kuwa, "Mtazamaji wa mpira ni rahisi kugundua uzaifu wa mchezaji ukilinganisha na mchezaji mwenyewe"

Hivyo sayansi hivyo inawataka wachezaji kusikiliza mawaidha na changamoto zitakazoletwa na wachambuzi na pia mashabiki wao.

Niliwahi soma msemo mmoja ambao ulisema kuwa, "Adui ni mtu aliyemakini sana kutazama na kufuatilia Maisha yako kuliko rafiki yako"

Ni kwamba Adui ni kama mchambuzi kwako, maana anakufunilia matatizo yako na kukupa changamoto ya kufikiri zaidi ya unavyofikiri.

05: MAOMBI YA WATU WA MUNGU JUU YAKO.
"Endapo utasikia sauti moja ya mtu mmoja ikikutia moyo katikati ya sauti za watu wengi za kukuvunja moyo, usirudi nyuma pambana utafikia matamanio na malengo yako".

Akili yangu inaniongoza kuamini maneno ya baraka ambayo tunachukulia kama utani pale tunapo ambiwa na watu wa Mungu, ambao tunakutana nao wanapoomba msaada kwetu mfano ombaomba barabarani.

Hali yako ya maisha kwa sasa imetengenezwa na maombi ya mtu wa Mungu ambaye humfahamu na hautakuja kujua kama anakuombea.

Hivyo tunapaswa kuwaheshimu Watu wote maana hatuja funuliwa kwetu mtu ambaye umlilia Mungu kila siku kwa ajili yetu.

Ebu jaribu kufikiri ni mara ngapi umewatusi na kuwadharau watu ambao huwajui , omba msamaha kwa Mungu maana huenda ni yule ambaye anakuombea ufanikiwe.

#Kuwa Taswira ambayo ni fumbo kwao#
Imeandaliwa:-
©tujuemoja
(David MALUNDA)
MWANAFUNZI KATIKA CHUO CHA RUCU
 
Upvote 0
Back
Top Bottom