Sababu 5 zenye kufanya mwenza wako anapoteza hisia za mapenzi juu yako unapo mjali sana na kunyenyekea sana

Sababu 5 zenye kufanya mwenza wako anapoteza hisia za mapenzi juu yako unapo mjali sana na kunyenyekea sana

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Sababu hizo 5 ni hizi zifuatazo
1.HAUNA MIPAKA
Kama unaishi na mwenza wako huku unamnyenyekea sana,upo tayari kuvumilia tabia zake ikiwemo kukufokea, kukutukana, kukupa vitisho, vipigo, lawama,kutishia kuvunja mahusiano mara kwa mara, kukudhaliisha mara kwa mara lakini unakaa kimya lazima atafanya vituko kila siku.

Kama mwenza wako akiwa na hasira unahisi umefanya makosa na kuanza kuhofia usalama wako au mahusiano kuvunjika ndio unazidi kufanya anakuwa na kiburi

2.UMEWEKEZA GHARAMA KUBWA SANA KWAKE
Kama umetumia fedha nyingi sana kumsomesha mwenza wako, kumnunulia gari,kumjenga , kumtafutia kazi, kumchukulia mkopo benki, kusomesha watoto ambao amezaa na mtu mwingine, kusomesha ndugu zake,kujitoa mhanga kwa wazazi wake kwa muda mrefu sana unafanya mwenza wako anakuwa na kiburi sana kwako na kuona hauna uwezo wa kumuacha .

Kama imejitoa mhanga kwa mwenza wako kwa muda mrefu sana hawezi kukuheshimu maishani mwake kwa sababu anaona huna uwezo wa kupata mwenza mbadala .

Utashangaa hana msaada wowote kwako lakini anakufokea, kukutukana, kukupa vitisho, vipigo, lawama, kudhalilisha ndugu zako lakini hauna uwezo wa kumuacha.

3.UNAOGOPA UGOMVI NA MIGOGORO
Kama unaogopa kusemwa vibaya,kuogopa kuonekana mchoyo,kuogopa kukosolewa utafanya mwenza wako anakuwa na kiburi sana juu yako kwa sababu anakuwa anafanya makosa kwa makusudi kupima msimamo wako lakini wewe unaomba badala badala ya kumchukulia hatua kali za kinidhamu.

Wanaume na wanawake huwa wapo na tabia ya kumjaribu mwenza kwa kumfokea,kumkosoa, kumtishia kuvunja mahusiano na ikiwa mwenza mmoja ataonekana kutetereka inakuwa mwanzo wa manyanyaso katika mahusiano.

4.UNASAMEHE HARAKA
Kama mwenza wako anafanya makosa unasamehe haraka na kumuomba mrudiane kujenga familia pamoja anapata kiburi cha kurejea makosa yaleyale mara kwa mara.

Chunguza hata kwa watoto wadogo kama anajua mzazi wake hawezi kumuadhibu kwa kosa lolote anapata kiburi sana na anakuwa hana heshima kwa mzazi.

Katika mahusiano haina maana ya kupigana ngumi inamaanisha piga marufuku tabia kama kufokewa, kutukanwa, kupelekeshwa,kupewa vitisho na ikiwa mwenza wako hawezi kubadilika tabia mwambie upo tayari kuvunja mahusiano hayo muda wowote na isiwe kumtisha iwe msimamo wa kweli.

Yapo makosa ya kutoa msamaha sio kila kosa.Kwa mfano unajua mwneza wako ni mlevi kupindukia,anatumia bangi au dawa za kulevya kisha unaona ameuza mali zako bila ridhaa yako na kukusababishia hasara unatakiwa kuchukua hatua sio kusamehe kwa sababu anajua unaunga mkono tabia zake.

5.UNAAMINI UKIMUACHA ATATESEKA SANA BILA WEWE
Ikiwa mwenza wako hana maelewano mazuri na wazazi wake,hana marafiki wa kueleweka,hana maelewano mazuri kazini,anadaiwa kila kona,anatumia fedha nyingi sana ghafla,kila mtu amechoka kwa tabia zake lakini wewe unajitoa mhanga kwake lazima akupe hasara kisha anatokomea kusikojulikana.

Mwanaume au mwanamke yeyote ambaye hana maelewano na watu wengine ukijitoa mhanga kwake umeumia.
Ukiona mwenza wako anakuona wewe tu ndiye kimbilio lake huku kila mtu hana maelewano nae ujue hilo ni tatizo.

Ikiwa unaamini kwamba kama utateseka sana kwa niaba ya mwenza wako ndiyo anaweza kukupenda hapo unakosea .

Kwa kawaida "Wife material & husband material" huwa wanaogopa sana kuwa mizigo kwa watu wengine kwa maana wanaogopa kuegemeza matatizo yao kwa mtu mwengine badala yake wao wanataka kujikwamua kimaisha ili wapate kupendwa sio wao kutanguliza matatizo yao na kutaka huruma .

Wanawake wenye tabia za unyanyasaji hutanguliza matatizo yao kwa mwanaume na wanaume wenye tabia za unyanyasaji hutanguliza matatizo yao kwa wanawake kwa kusingizia maisha yao magumu sana na kutoa orodha ya watu wabaya juu ya ugumu wa maisha yao kisha wanataka uwe msaada wao na kimbilio la mwisho ukishindwa unageuka adui.

Kama unaamini mwenza wako hawezi kuishi bila wewe maana yake mwenza wako anapoteza hisia za mapenzi juu yako kwa kuona unajitoa mhanga sana kwake kisha ataenda sehemu anakosa mahitaji kabisa.

UFUMBUZI WAKE NI
#Epuka kujitoa mhanga katika mahusiano yako badala yake toa mchango wako kulingana na uwezo wako sio kuogopa kukosolewa na mwenza wako

#Weka mipaka katika mahusiano yako na mwenza wako
Punguza muda wa kupatikana akiwa anakuhitaji ,usiwe upo tayari kuonana naye kila dakika,ukiwa karibu sana na mwenza wako hawezi kuona umuhimu wako kwa sababu kanuni inasema kitu chochote chenye kupatikana kwa urahisi hakina thamani.

Hivi rafiki yako akipiga simu na mtu Mheshimiwa katika nchi akipiga simu kwako unapokea ya nani haraka ? Unajua kwanini? Kitu chochote ambacho kinapatikana haraka hakina thamani.

#Kemea tabia zake zenye maudhi.Kama huwezi kusema siwezi kuvumilia tabia za kufokewa, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kupuuzwa, kupelekeshwa, kufanywa kichekesho,kutishiwa na ikiwa huwezi kujirekebisha tabia basi tuvunje mahusiano.Maana yake mwenza wako anajua yupo huru kuongea chochote kwako ni sawa na ofisi haina sheria unakwenda muda wowote na kuondoka muda wowote hakuna kuhojiwa.

#Onyesha misimamo kwa baadhi ya mambo kuonyesha haupo tayari kupelekeshwa ikiwa huwezi atakutawala anavyotaka .
 
Hii ni kwaajir ya vijana tunaoanza kujifunza mapenz nyie makonki msije kutupoteza kabisa jamaa yupo sahihi sana na nmependa Asante sana
 
Back
Top Bottom