Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
Kuwa mwanaume ni kazi sana kuliko watu wanavyodhani.
Mwanaume hawezi kukwepa majukumu,mwanaume hawezi kukwepa vitimbi au maudhi ya Mwanamke ndani ya familia, mwanaume hawezi kukwepa nafasi ya kiuongozi ndani ya familia akikwepa anamkosa mke pamoja na watoto.
Huwa tunasikia hadithi za kila aina kwamba wanawake hawajui wanataka nini lakini uhalisia ni kwamba kumuelewa mwanamke ni rahisi sana.Ikiwa wewe ni mwanaume na umekuwa unateseka sana kwenye mahusiano yako na mwenza wako mwisho wa soma ujumbe huu mpaka mwisho nakupa guarantee kwamba hautakuja kupitia "Stress" za mapenzi katika maisha yako yote.
Kuna sifa kama upole, huruma,kujali, kusamehe makosa, unyenyekevu, uvumilivu n.k hizi ni sifa nzuri sana kuzisikia tu lakini ukija kwenye ulimwengu halisi mwanaume mwenye sifa hizo huonekana DHAIFU SANA mbele ya jamii na hudharauliwa sana.
Unaweza kupatwa na mshangao lakini soma ujumbe mpaka mwisho.
Wanaume wenye sifa za kujali sana, kusamehe makosa haraka, uvumilivu kupita kiasi, unyenyekevu,kuogopa ugomvi na hasira ya mwanamke huitwa NICE GUYS kuna msemo unasema "Nice Guys finish last" kwa maana mwanaume mwenye kuonekana mstaarabu sana huishia kuwa wa mwisho katika kila sekta ya maisha yake.
Utajuaje kama wewe ni "Nice Guys" jibu maswali yafuatayo kwa kuandika NDIYO au HAPANA kulingana na hali yako kisha utagundua kwanini "NICE GUYS finish last"
1.Umekuwa unalalamika kwamba hakuna mwanamke anavutiwa na wanaume wastaarabu?
2.Je huwa unaumia sana pale ambapo mwanamke amekukataa?
3. Je huwa unaishia kupata marafiki wengi wa kike lakini haupati mwenza?
4. Umewahi kumsikiliza rafiki yako wa kike akilalamika kuhusu mahusiano yake kisha ulijenga matarajio kwamba anakwenda kumuacha mwenza wake kwa ajili yako wewe ?
5.Umekuwa mara kwa mara unasema kwamba wewe ni mtu mstaarabu,mwenye kujali sana watu na kuheshimu sana wanawake?
6.Umewahi kumwambia mwanamke ambaye ameumizwa na mapenzi kwamba wewe ni wa tofauti na utamjali sana kuliko mwenza wake anavyofanya ?
7.Huwa unashangaa kwanini wanaume ambao hawana huruma,hawajali kabisa Mapenzi wanapata wanawake wastaarabu haraka lakini wewe haupati?
8. Je unaamini kwamba kama ukimpenda mwanamke hautakiwi kukata tamaa hata kama amekukataa mara nyingi?
9.unaamini wewe ni mtu mstaarabu, mwenye kujali sana,mwenye huruma,mwenye tabia njema sana katika jamii kuliko wanaume wengine?
10. Je unajiona mnyanyasaji au mkosaji kama ukiona mwanamke yupo na huzuni,hasira,au anajisikia vibaya kisha unadhani ni wajibu wako kufanya chochote ili kumfurahisha?
11. Je huwa unaomba msamaha mara kwa mara kama ukiona mwanamke yupo na hasira kupita kiasi mbele yako na unaongea kwa sauti ya upole kupita kiasi kama mwanamke anaongea kwa sauti ya ukali kupita kiasi?
12. Je huwa unaanza kwa kujenga urafiki na mwanamke kwa kumsaidia sana kazi zake,kubeba mizigo yake,kumpa zawadi,kuongea vichekesho vichekesho bila kuzungumza moja kwa moja unataka nini kwake ?
Kama umejibu NDIYO nusu ya maswali hayo maana yake wewe ni NICE GUY kwa maana hiyo unaonekana mpole sana, mnyenyekevu, mwenye huruma kupita kiasi, uvumilivu,kusaidia sana,kuogopa ugomvi na migogoro ukiamini ndiyo tiketi ya kupendwa na wanawake lakini uhalisia ni tofauti kabisa.
Chanzo cha kujenga tabia hizo ni
I. KULELEWA BILA BABA AU KUPATA BABA DHAIFU SANA
vyanzo vya kumkosa baba utotoni au kupata baba dhaifu sana ni kifo cha baba, talaka, kutengana kwa wazazi, baba kufungwa gerezani, baba kuishi mbali sana na familia, baba kuitelekeza familia, baba kukataa ujauzito, baba kuhama makazi,baba kuathirika na dawa za kulevya, pombe kupindukia, kuvuta bangi,
#baba kuwa mzee sana au mgonjwa sana au mlemavu ambaye alikuwa hana uwezo wa kukuwajibisha ukifanya makosa utotoni.
II. KUWEPO BABA AMBAYE HANA ATHARI ZOZOTE KWAKO
Unaweza kuwa "Nice guy" kwa sababu katika familia yenu mwenye kauli ya mwisho ni mama huku baba yupo kama bendera tu.
Hivyo unaishi kwa kugombezwa na mama huku baba anakuacha huru uishi vile ambavyo unataka bila kujali athari zake ukubwani.
III. KUMLEA MZAZI BADALA YA MZAZI KUKULEA WEWE
Unaweza kuwa "Nice guy" kwa sababu umeanza kulea familia yenu ukiwa mdogo sana labda kwa sababu ya umasikini kupita kiasi,ugomvi wa mara kwa mara wa wazazi,baba kufungwa gerezani, baba kuitelekeza familia, baba kuwa mzee sana au mgonjwa sana au mlemavu au mlevi kupindukia hivyo ulibeba majukumu makubwa kabla ya umri.
SABABU 5 ZENYE KUFANYA WANAUME WAPOLE SANA, WENYE KUJALI SANA, WENYE KUSAIDIA SANA HUISHIA KUPATA MWENZA DIKTETA, MGOMVI MGOMVI,NA MBABE
Zifuatazo ni sababu 7 zenye kufanya wanaume wenye tabia za upole kupita kiasi, uvumilivu kupita kiasi, unyenyekevu, huruma kupita kiasi,kujali sana, kusamehe makosa kupata mwenza dikteta, mgomvi mgomvi, mwenye lugha ya udhalilishaji.
1. KUSHINDWA KUSIMAMA KAMA KIONGOZI NDANI YA FAMILIA
Mwanaume Rijali huwa kichwa cha familia kisha mwanamke anakuwa chini ya uangalizi.Lakini hawa Nice guy huwa kinyume chake anaweza kuwa "Mario" ambaye anaishi kwa kumtegemea mwanamke kwa kila kitu au anaishi huku anatoa huduma zote ndani ya familia lakini maamuzi yote hufanywa na mwanamke yeye anafuata maagizo ya mwanamke.
Kwa kawaida wanawake wenye upendo, huruma,kujali, kunyenyekea huvutiwa kimapenzi na mwanaume mwenye kujiamini,mwenye kusimama kama kiongozi.
Hivyo wakiona mwanaume mpole sana wanamuona kama mwanamke mwenzao hivyo wanajenga nae urafiki tu.
Ukiwa mwanaume mstaarabu sana kisha unaona upo "single" na umezungukwa na marafiki wengi sana wa kike ni kwa sababu wanakuona kama mwanamke mwenzao.
Wanawake wenye tabia za ubabe, ukali kupita kiasi,jeuri,dharau na majigambo na majivuno huwa wanasema kwa mwanaume "Chagua mimi au mama yako mzazi" kwa mwanaume Rijali akisikia kauli hiyo papohapo hapo anamfukuza mwanamke bila maelezo yoyote lakini kwa wanaume ambao ni nice Guys huanza kutafuta ushauri wa kubadilisha tabia ya MWANAMKE jambo ambalo sio sifa ya mwanaume.
2. KUOGOPA UGOMVI NA MIGOGORO
Sifa ya mwanaume Rijali huwa haogopi ugomvi wala migogoro na mtu yeyote lakini wanaume ambao ni nice Guys huwa wapo kama "Wife material" kwa maana sifa ya upole, huruma,kujali, kusamehe makosa, unyenyekevu, uvumilivu huwa utambulisho wao uhalisia ni kwamba hizo ni sifa za mwanamke siyo mwanaume.
Sifa za mwanaume ni kuwa kiongozi,kuwa shujaa, mpambanaji, asieogopa kusemwa vibaya,hataki kupendwa na kila mtu,hataki kuungwa mkono na kila mtu.
Kama ni mwanaume unaogopa migogoro na ugomvi utafanya mwanamke aishi kwa dhiki,taabu, simanzi, huzuni na upweke kila siku kwa sababu dada zako na mama yako watakuona hauna sifa za mwanaume hivyo wataamua wao kuingilia maisha yako na mwenza wako wataanza kukupangia namna ya kuishi na mwenza wako,wakiamua kumfukuza mwenzao wako na kuleta mwanamke wanamtaka watafanya hivyo kwa sababu hawaoni kama unaweza kujiongoza.
Mwanaume Rijali anamlinda , kumtetea mwenza wake,anamlindia heshima na vilevile haonekani kunyenyekea sana mapenzi kwa hofu ya kusalitiwa au kuachwa na vilevile endapo mwanamke atafanya utovu wa nidhamu anapewa onyo kali na akileta jeuri anarudishwa kwao bila maelezo yoyote.
3. HAWANA UWEZO WA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU
Nice Guys huwa wanaume wenye sifa za kike japokuwa wao hujiona ni wastaarabu saba kwenye jamii lakini uhalisia ni tofauti.
Kwa mfano mwanamke akitaka kuachana na mwanaume huonyesha tabia zifuatazo kumfokea, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia, kutoroka kwenda kwao mara kwa mara,kuzusha uongo,kutishia muachane kila siku,kuomba fedha nyingi sana kuliko uwezo wa mwanaume ,kutafuta ugomvi mara kwa mara ili apate sababu ya kurudi nyumbani kwao.
Anaweza kuchati na wanaume wengine mpaka saa 8 usiku, anaweza kutongozwa mbele ya mwanaume wake na kusingizia hakuna kitu chochote kibaya kinaendelea baina yao.
Hapa anafanya makusudi ili mahusiano yavunjike,hataki risala, hataki vitisho,hataki ushauri,hataki kukumbushwa wema ambao mwanaume amefanya .Kitu pekee anataka ni mahusiano kuvunjika tu..
Hawa wanaume ambao ni nice Guys huanza kulia, kuomba msamaha, kupiga magoti,kupiga simu mfululizo kwa ndugu wa mwanamke ,kutishia kujiua hizo ni sifa za wanawake sio wanaume .
Kwa upande wa mwanaume Rijali akiona utovu wa nidhamu tu ampa onyo kali sana mwanamke na kusisitiza anataka heshima na ikiwa hakuna heshima basi wataachana papohapo.
Hawa wanaume ambao ni nice Guys wanaweza kukaa kimya, kuvumilia usaliti, kuvumilia matusi, vipigo, lawama,vitisho, tuhuma za uongo kwa miaka mingi sana kwa sababu ya kukosa sifa za uanaume ndani ya familia.
4. KUSHINDWA KUVUTIA WANAWAKE WENGINE
Kwa kawaida wanawake huvutiwa kimapenzi na mwanaume ambaye anapendwa na wanawake wengine , wanaamini huyu atakuwa na mbegu nzuri ya kuzaa watoto na kuwapa matunzo na ulinzi.
Nice Guys huwa kinyume chake.Anakuwa mwanaume anataka wanawake wakimuona tu wampende na kujenga nae familia bila yeye kufanya juhudi za kumfuata mwanamke..
Kwa asili wanawake hawana ujasiri wa kumwambia mwanaume kama wanampenda bali hufanya mitego, kujipitisha pitisha,kumtega kwa uvaaji na sauti lakini sio kuongea moja kwa moja.
Hawa wanaume ambao ni nice Guys huonyesha tabia hizohizo za kike kama vile kujenga urafiki kwanza,kumsaidia sana mwanamke kisha baadaye wanataka mwanamke aone kwamba wanafaa kuwa "Husband material" kwa wema ambao wamefanya.
Wanawake hupenda kupitia wivu ,akiona wivu kwa mwanaume anaamini mwanaume huyo akimpata atakuwa na furaha sana.
Haiwezekani kwa mwanamke kuona wivu kwa nice Guys kwa sababu haonekani kama mwanaume mwenye kuvutia katika jamii.
5.KUSHINDWA KUJIWEKEA MIPAKA
Nice Guys hawana mipaka baina yao na wanawake..
Kwa kawaida mwanaume huonekana mwenye kuvutia kama hapatikani kwa urahisi, vilevile hatabiriki..
Anaweza kupokea simu na wakati mwingine hapokei kwa sababu anakuwa busy sana.
Nice Guys huwa anapatikana muda wote saa 24 anaamini akikaa kimya bila mawasiliano hata kwa dakika kadhaa ataziumiza hisia za mwanamke na kufanya mwanamke amcchukie lakini uhalisia ni kwamba wanaume ambao hawapatikani kwa urahisi huwa ndiyo wenye kuvutia sana machoni kuliko hawa wanaopatikana muda wote.
.
Nice Guys akiombwa fedha nyingi sana yupo tayari kwenda kukopa ,jambo ambalo hufanya anapoteza mvuto moja kwa moja.
Mwanamke akiomba kitu chochote anapewa papohapo jambo ambalo husababisha mwanamke kumchoka mwanaume haraka.
Uhalisia ni kwamba mwanamke anampenda sana mwanaume pale ambapo hana uhakika wa kupata mahitaji yake yote kwa sababu inakuwa kama surprise na siku zote surprise huzidisha mapenzi kuliko kitu chenye kutabirika.
🤺🤺
Kama tatizo lako ni kubwa zaidi tunaweza kuwasiliana kwa ajili ya Counselling session na ufafanuzi wa kilichoandikwa hapo juu na utaona mabadiliko na kujisikia nafuu ndani ya muda mfupi baada ya mazungumzo.(Counseling kwa njia ya simu gharama Tshs 3......,... , kuonana uso kwa uso Tshs 4..............