Nilimpenda mno ikawa big issue pale shuleni, kipindi hicho nipo form 6. Ikawa kesi maana kama mjuavyo sheria za shule haziruhusu.
Kwao alikatazwa haswa asiwe na mahusiano na Mimi lakini hakusikia lolote, baada ya mambo kuwa mengi wakataka kumuondoa nchini kumrudisha Oman. Alikaa siku 3 bila kufika shuleni na nkapata info kutoka kwa shoga yake ambae alikuwa jirani yake kwamba amekatiwa ticket tayar after two weeks anaondoka kuelekea Oman. Sikukubali nkaenda mpaka kwao, kufika nkaambiwa live mtoto wao hawezi kuwa na Mimi mtu mweusi. Hilo lilinifanya kwa moyo safi niachane nae na kuichukia sana familia yao