article
Senior Member
- Sep 10, 2016
- 186
- 344
Amani iwe nanyi!.
Nimepata nafasi ya kufanya uchambuzi wa wa taarifa za fedha (Statement of comprehensive income and statement of cash flows) za CRDB za robo ya tatu 2016 na kugundua sababu zifuatazo zilizosababisha Benki kupata hasara ya takribani Tsh.2 bilioni:
1.Kuongezeka kwa matumizi yasiyo ya riba kama vile mishahara na ada kwa 38.72% (kutoka Tshs.77,605 millioni.mpaka Tshs.107,651 milioni).
2.Kupungua kwa mapato yasiyo ya riba kama vile mapato yanayotokana na kubadilisha fedha za kigeni,ada kwa wateja na kamisheni kwa 12% (kutoka Tshs.44,036milioni mpaka Tshs.38,556 milioni.)
3.Kuongezeka kwa malipo/madai ya Riba yanayotokana na CRDB kukopa kutoka taasisi nyingine za fedha kwa 52.55%(kutoka Tshs.23,213 milioni mpaka Tshs.38,556 milioni).
4.Kuongezeka kwa hasara ambazo zitasababishwa na wateja waliochukua mikopo na "advance" kushindwa kurejesha fedha kwa 195%( kutoka hasara ya Tshs.13,093 milioni mpaka kufikia hasara ya Tshs. 38,687 milioni.)
5.Huduma mbaya za opereshini za kibenki za kila siku (operating activities) zilizopelekea hasara ya fedha taslimu Tshs15,173 milioni ukilinganisha na fedha taslimu Tshs 33,778 milioni zilizopatikana katika kipindi cha ulinganifu.
Napenda kuchukua nafasi hii kuuomba uongozi wa CRDB kutoa taarifa kwa wadau kuhusiana na hatua ambazo uongozi unatategemea kuchukua kurekebisha hasara hii pia Naupongeza uongozi wa benki kwa kwa kufanya vizuri kwenye uwekezaji(investing activities) kwa kupata fedha taslimu Tshs 235,694 milioni ukilinganisha na hasara ya fedha taslimu Tshs 64,240 milioni katika kipindi cha ulinganifu.
Nawakilisha,
Article.