Sababu kuu tatu zinazokwamisha Feisal Salum asiende kuchezea Simba

DELETED ACCOUNT

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
9,805
Reaction score
15,476
Mijadala mingi inayohusiana na uhamisho wa Feisal Salum kutoka Azam kwenda Simba imejikita kwenye gharama za uhamisho huo ila ukweli ni kuwa kuna sababu tatu kuu zingine tofauti kabisa zinazokwamisha uhamisho huo.

Gharama inayotajwa ya bilioni 2 na ushee siyo pesa nyingi kulinganisha na faida za kibiashara ambazo Simba itakuja kuzipata. Hamsha hamsha ya ununuzi wa jezi za Simba zitaongezeka mno. Simba imestruggle sana kwenye mahudhurio ya mashabiki viwanjani katika misimu hii miwili ya nyuma ila usajili wa Feisal utaongeza sana mahudhurio viwanjani tena hata kwa ongezeko kidogo la bei ya viingilio.

Matajiri na wadhamini mbalimbali wa Simba hawawezi kushindwa kuchangishana shilingi bilioni 2.5 ili waje kupata faida hizi za kibiashara.

Ngoja nitaje sababu hizo tatu zinazokwamisha dili hili lisifanikiwe.

1. Ushindani wa kibiashara wa Mo na Azam. Tukumbuke bidhaa nyingi ambazo Azam wanamtumia Feisal kuzitangaza ndani na nje ya mkataba wake rasmi na Azam FC zinafanana na bidhaa ambazo Mo Dewji pia anazalisha. Kumuachia Feisal aende Simba ni kama kumuachia mpinzani wako mkuu akushinde katika masoko ya bidhaa za viwandani ambazo wanashindana. Sitashangaa kuona Feisal anasaini dili lingine la kubaki Azam.

2. Utamaduni wa Yanga na Simba kutopenda kumfaidisha mwenzie kifedha ni sababu nyingine kubwa. Kama nilivyosema, Simba ina uwezo wa kukusanya hizo bilioni 2.5 ila kipengele cha kuipa bilioni 1 Yanga katika hizo 2 kinaleta ukakasi sana katika tamaduni zetu za mpira. Mara nyingi Simba imeshaonyesha maturity katika maeneo mengi, mimi naona Simba ifungue ukurasa na mwanzo mpya katika mpira wetu, Yanga ilipwe pesa yake imnyakue Feisal. Nina uhakika Yanga watashangaa na kushtuka sana hili likifanyika na ndani ya mioyo yao wataiheshimu sana Simba ikifanya kitendo hicho na Simba itakuwa imeweka rekodi nyingine mpya ya ustaarabu katika mpira wa Tanzania.

3. Mshahara wa Feisal nao ni kikwazo. Unajua, watu wengi wanaangalia tu gharama za uhamisho wa mchezaji ila wanasahau kuwa kwa jinsi gharama za uhamisho zinapokuwa kubwa, kuna uwezekano wa mshahara na marupurupu ya mchezaji nao kuwa mkubwa. Ukiacha bilioni 2.5 za uhamisho wa Feisal, hapo haujaongelea mshahara wake ambao unaweza kufika au hata kuzidi shilingi milioni 600 kwa mwaka. Hapo bado haujahesabu signing fee, pesa anayolipwa mchezaji moja kwa moja pale anaponunuliwa ambapo kwa Feisal inaweza kufika 800M. Ndiyo maana wanaletwa kina Neo Maema kwa mkopo maana pamoja na kwamba wapo kwenye mikataba mikubwa na ni gharama kubwa kuwanunua, ila uhamisho wa mkopo unakuwa unahusisha gharama za mshahara pekee kwa hiyo mzigo unakuwa nafuu kiasi hata kama mshahara unafanana au hata unazidi kidogo wa mchezaji inayebidi kuhamishwa mazima kama Feisal.

ZIADA: Hii inaweza iwepo au isiwepo ila ni muhimu pia kuizingatia. Chembechembe ya Uzanzibari nayo inaweza kuchangia kumfanya Feisal atake kubaki Azam.

Kwa kumalizia niseme tu, isingekuwa sababu ya kwanza ya mgongano wa kibiashara kati ya Bakhresa na Mo, wangeweza kulicheza dili kifamilia ili kuepuka kuilipa Yanga hiyo bilioni 1 na kwa hiyo uhamisho kuwa nafuu zaidi kwa Simba. Njia za kufanya hivyo zipo ila mashabiki mandazi wa Yanga wanajulikana kwa jazba, fitna na undava. Tuliona wakati wa mgogoro wa derby jinsi walivyoanza hata kuipa shinikizo Azam TV wasirushe matangazo ya promo ya mechi waliyokuwa wanaigomea. Mashabiki na wanachama wa Yanga wangefanya kila njia kuiangusha kibiashara Azam na nadhani Azam hawako tayari kuingia katika hiyo vita ambayo kimsingi haina msaada wowote kwao.
 
Mijadala mingi inayohusiana na uhamisho wa Feisal Salum kutoka Azam kwenda Simba imejikita kwenye gharama za uhamisho huo ila ukweli ni kuwa kuna sababu tatu kuu zingine tofauti kabisa zinazokwamisha uhamisho huo.

Gharama inayotajwa ya bilioni 2 na ushee siyo pesa nyingi kulinganisha na faida za kibiashara ambazo Simba itakuja kuzipata. Hamsha hamsha ya ununuzi wa jezi za Simba zitaongezeka mno. Simba imestruggle sana kwenye mahudhurio ya mashabiki viwanjani katika misimu hii miwili ya nyuma ila usajili wa Feisal utaongeza sana mahudhurio viwanjani tena hata kwa ongezeko kidogo la bei ya viingilio.

Matajiri na wadhamini mbalimbali wa Simba hawawezi kushindwa kuchangishana shilingi bilioni 2.5 ili waje kupata faida hizi za kibiashara.

Ngoja nitaje sababu hizo tatu zinazokwamisha dili hili lisifanikiwe.

1. Ushindani wa kibiashara wa Mo na Azam. Tukumbuke bidhaa nyingi ambazo Azam wanamtumia Feisal kuzitangaza ndani na nje ya mkataba wake rasmi na Azam FC zinafanana na bidhaa ambazo Mo Dewji pia anazalisha. Kumuachia Feisal aende Simba ni kama kumuachia mpinzani wako mkuu akushinde katika masoko ya bidhaa za viwandani ambazo wanashindana. Sitashangaa kuona Feisal anasaini dili lingine la kubaki Azam.

2. Utamaduni wa Yanga na Simba kutopenda kumfaidisha mwenzie kifedha ni sababu nyingine kubwa. Kama nilivyosema, Simba ina uwezo wa kukusanya hizo bilioni 2.5 ila kipengele cha kuipa bilioni 1 Yanga katika hizo 2 kinaleta ukakasi sana katika tamaduni zetu za mpira. Mara nyingi Simba imeshaonyesha maturity katika maeneo mengi, mimi naona Simba ifungue ukurasa na mwanzo mpya katika mpira wetu, Yanga ilipwe pesa yake imnyakue Feisal. Nina uhakika Yanga watashangaa na kushtuka sana hili likifanyika na ndani ya mioyo yao wataiheshimu sana Simba ikifanya kitendo hicho na Simba itakuwa imeweka rekodi nyingine mpya ya ustaarabu katika mpira wa Tanzania.

3. Mshahara wa Feisal nao ni kikwazo. Unajua, watu wengi wanaangalia tu gharama za uhamisho wa mchezaji ila wanasahau kuwa kwa jinsi gharama za uhamisho zinapokuwa kubwa, kuna uwezekano wa mshahara na marupurupu ya mchezaji nao kuwa mkubwa. Ukiacha bilioni 2.5 za uhamisho wa Feisal, hapo haujaongelea mshahara wake ambao unaweza kufika au hata kuzidi shilingi milioni 600 kwa mwaka. Ndiyo maana wanaletwa kina Neo Maema kwa mkopo maana pamoja na kwamba wana mikataba mikubwa, uhamisho wa mkopo unakuwa unahusisha gharama za mshahara pekee kwa hiyo mzigo unakuwa unapungua kidogo hata kama mshahara unafanana au hata unazidi kidogo wa mchezaji inayebidi kuhamishwa mazima kama Feisal.

ZIADA: Hii inaweza iwepo au isiwepo ila ni muhimu pia kuizingatia. Chembechembe ya Uzanzibari nayo inaweza kuchangia kumfanya Feisal atake kubaki Azam.

Kwa kumalizia niseme tu, isingekuwa sababu ya kwanza ya mgongano wa kibiashara Azam na Simba wangeweza kulicheza dili kifamilia ili kuepuka kuilipa Yanga hiyo bilioni 1. Njia za kufanya hivyo zipo ila mashabiki mandazi wa Yanga wanajulikana kwa jazba, fitna na undava. Tuliona wakati wa mgogoro wa derby jinsi walivyoanza hata kuipa shinikizo Azam TV wasirushe matangazo ya promo ya mechi waliyokuwa wanaigomea. Mashabiki na wanachama wa Yanga wangefanya kila njia kuiangusha kibiashara Azam na nadhani Azam hawako tayari kuingia katika hivyo vita ambayo kimsingi haina msaada wowote kwao.
mkuu ulitutangazia umeachana na mpira" yaani hushabikii tena mamipira ya hapa bongo. sasa imekuwaje?
 
simba waki delay sasa,atasaini dili mpya na azam na azam akishinwa kumshawishi hiyo mwakani injina atawaliza vibaya watu hapa mjini...mwamba atarudishwa jangwani
 
Yanga haina pesa ya kumlipa Feisal kwa kushindana na Azam
 
mkuu ulitutangazia umeachana na mpira" yaani hushabikii tena mamipira ya hapa bongo. sasa imekuwaje?
Kuna kamzuka tu kalinipanda hapo kati ila naona dalili za kurudi katika likizo yangu. Bado mauzauza ni mengi sana na yanaongezeka kila uchao.
 
Back
Top Bottom