Uchaguzi 2020 Sababu kuu ya Lissu kushindwa, asilimia 80 ya Watanzania wanaishi Vijijini hawamjui Lissu ni nani, Magufuli anajulikana kila kona Vijijini

Kwa hisia za humu ndani Lissu ameshakua rais yani nyie binadamu nyie hata Mungu anawaona, hebu fanyeni kazi.
 
Bibi yangu ana miaka 80 yupo kijijin huko kila cku analalamika kwanin serikal haitoi ajira? Anasema waz hatoipigia ccm
 
usichokijua ni kwamba hao wengi unaohisi wanamjua Jpm ndo wanaomchukia kutokana na maisha halisi tunayoishi ni "Magumu" pata picha ww baba wa familia ujenge,ununue gari na usomeshe pia ndani ya mwaka lazima familia iyumbe kabisa ndicho kinachomkuta mkuu miradi mingi SN lazima nchi iyumbe
 
Vijiji gani unazungumzia ambavyo havina simu janja?wewe unadhani tecno spark xote xiko wapi?
 
Uchaguzi huu ukanda hautafanikisha chochote hata huku mimi siwezi kumpa kura Magu mbele ya Lissu labda niwe nimerogwa
 
Uchaguzi huu ukanda hautafanikisha chochote hata huku mimi siwezi kumpa kura Magu mbele ya Lissu labda niwe nimerogwa
 
Mbna unapandisha maibilisi ww bi mdada?
 
Nimerejea tu toka safari yangu huko mkoa,

Kwa kweli jamaa hawampendi kajiharibia sana alipokuwa anawatetea Accacia, wanamuaita msaliti, hawataki hata kumsikia.

Mazungumzo yaliyopo ni kuwa jamaa katumwa kuja kutuvuruga.

Lisu ana hasira sana ya kuumizwa hivyo yupo tayari kuona kila mtu akiwa katika hali kama yake ndio afarijike.

Chadema wangetumia nafasi hii kumtibu kisaikolojia badala ya kumpa nafasi ya kugombea Urais.
 
Magufuli anajulikana zaidi vijijini tokea alipokuwa waziri wa barabara. Kwani alitembea kwa gari nchi nzima mara kwa mara akikagua barabara.
Pili anajulikana zaidi vijini wakati wa kampeini ya uraisi 2015.
Tatu tokea apate uRaisi amekuwa ni kawaida kusimamisha msafara wake na kutatua matatizo ya wananchi papo kwa papo.
 
Kwaiyo sisi tuliousimamisha msafara wake kipindi kile cha tetemeko kagera alutatuaje zaidi ya kusema hajaleta tetemeko yeye? Juzi Kilwa kawaambia wananchi kuwa hawezi akawajengea stend kisa walimchagua mbunge wa upinzani?.Ndo kulikana kwake huko vijijini anajulikana kwa maamuzi ya kukurupuka yasiyo na logic as presidential man
 
Aliwatetea ACCACIA kwenye mahakama gani yeye akiwa wakili wa hiyo kampuni? Tuwekee data hapa
 
Lakini anajulikana yawe mema au mabaya.
 
Kura za upinzani kanda ya kusini kuna Membe,kanda ya Pwani na Dar watagawana na Membe.Lakini hata wakiamua kumsimamisha mmoja wao kitu ambacho ni nadra bado kuna mapungufu.
 
Wewe ni muongo hadi unatia kinyaa. Kama hakubaliki kwao kabisa Chato ndio atakubalika kwingine kanda ya ziwa?
Kawawekea Airport, traffic lights, CRDB isiyo na wateja, hospitali ya rufaa, TAKUKURU jengo kubwa lakini ndio kiwango cha upinzani kwake kiko juu.
Safari hii wanasema,
 
Akutukanaye hachagui tusi. Wanakijiji tumekuwa wajinga kiasi gani tusimjue Lissu. Subirini oktoba mtajua kijani mbichi.
 
Unafiki kuwa sehemu ya maisha ya mtu ni hatari, kama hawamjui zikianza kampeni watamjua tu wewe haikuhusu 'you ca not brainwash people as simple as that'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…