Sababu kuu zenye Mantiki zilizowafanya na zinazowafanya Wayahudi wengi Wasimuamini Yesu Kristo

WARUMI/ROMAN 11:13-24
13.Lakini nasema na ninyi, mlio watu wa mataifa.Basi, kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa mataifa, naitukuza huduma ilio yangu, 14.nipate kuwatia wivu walio damu moja na mimi na kuwaokoa baadhi yao. 15.Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu,je! kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhai badala ya kufa? 16.Tena malimbuko yakiwa matakatifu,kadhalika na donge lote; na shina likiwa takatifu,matawi nayo kadhalika.17.Lakini iwapo matawi mengine yamekatwa,na wewe mzeituni mwitu ulipandikizwa kati yao, ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake, 18.usijisifu juu ya matawi yale;au ukiwa wajisifu,si wewe ulichukuae shina,bali ni shina likuchukualo wewe.19.Basi utasema,matawi yale yalikatwa kusudi ili nipandikizwe mimi.20.Vema.Yalikatwa kwa kutokuamini kwao,na wewe wasimama kwa imani yako.Usijivune bali uogope.21.Kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili,wala hatakuachia wewe.22.Tazama,basi,wema na ukali wa Mungu; kwa wale walioanguka, ukali, bali kwako wewe wema wa Mungu,ukikaa katika wema huo;kama sivyo,wewe nawe utakatiliwa mbali.23.Na hao pia,wasipokaa katika kutokuamini kwao,watapandikizwa;kwa kuwa Mungu aweza kuwapandikiza tena.24.Kwa maana ikiwa wewe ulikatwa ukatolewa katika mzeituni,ulio mzeituni mwitu kwa asili yake,kisha ukapandikizwa,kinyume cha asili,katika mzeituni ulio mwema,si zaidi sana wale walio wa asili kuweza kupandikizwa katika mzeituni wao wenyewe??

HAPO JUU NI NAFASI WALIOPO WAYAHUDI NA WATU WA MATAIFA KWA SASA INATAKIWA KUELEWA TU.BILA KUSAHAU SHINA NDIO YESU KRISTO.WAYAHUDI NI MATAWI NA MATAIFA NI MATAWI

KUHUSU WAYAHUDI AT THE END OF DAY
ROMAN 11:25-27
25.Kwa maana,ndugu zangu,sipendi msiijue siri hii, ili misijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, MPAKA UTIMILIFU WA MATAIFA UWASILI.26.Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa,
Mwokozi atakuja kutoka sayuni;Atamtenga Yakobo na maasia yake.Na hili ndilo AGANO langu nao."Nitawaondolea dhambi zao.""

Kuna ratiba maalum kwa mambo yote yanayoendelea hapa duniani,,dunia haiendi yenyewe tu, yupo INCHARGE.Kuna time of Gentiles na pia time for Jews.Kwa hio wayahudi kutomwamini YESU sio maamuzi yao ni neema ili na wengine wasio kwenye bloodline yao wapate nafasi lakini nafasi ya wayahudi ikiwa haijapotea.
 
Sawa
 
Wallah huu mjadali haukuhitaji mhemko... bunafsi nimesoma nimepata head against na nnacho amini.
Kwa hoja zilizopo nashindwa kureson kwakua nimeambiwa ni amini tuu🥵🥵🥵
 
Msaada tu Mdogo nikupatie ndugu yangu, kidogo tu maana Maada yako imekaa kiubishiubishi tu wala hauna hata nia ya kujifunza,

Ukihitaji kujifunza na kipengele kingine niambie

,,,,,,,,,,,,,
VSababu pekee ya Bwana Yesu kujulikana kama mwana wa Daudi, ni kutokana na Baraka Daudi alizozibeba, lakini si kutokana na undugu wa kidamu..Wewe unaitwa mwana wa Baba yako kutokana na uhusiano wa kidamu..lakini unaweza ukaitwa mwana wa Raisi wako, ila si kwa uhusiano wa kidamu bali wa pengine wa kiitikadi fulani….

Kwamfano pia sisi wakristo tunaitwa Wana wa Mungu, si kwasababu tumezaliwa familia moja na Muumba wetu,hapana au kwamba tuna damu moja na Mungu, hapana ni kutokana na Baraka za kimbinguni zinavyohusiana na sisi ndio maana tunaitwa wana wa Mungu.

Vivyo hivyo tunajulikana kwamba ni wana wa Ibrahimu , sio kwasababu sisi tuna damu moja na Ibrahimu, hapana bali ni kwasababu ni warithi wa Ahadi zile zile alizopewa Ibarahimu na Mungu, ndio maana na sisi tunajulikana kama wana wa Ibrahimu, Na Bwana Yesu ndio hivyo hivyo, Baraka alizopewa Daudi na mnyororo wa ukoo wake wote zilimhusu pia Bwana wetu Yesu Kristo…Daudi alikusudia kumjengea Mungu, Nyumba na hivyo Mungu akambarikia yeye na uzao wake kuwa uzao wa kifalme milele.(soma 2 Samweli 7:1-12)

kwasababu alizaliwa katika nyumba ya Yusufu ambaye alikuwa ni wa ukoo wa Daudi uliobarikiwa (ukoo wa kifalme),..Moja ya Baraka za ukoo wa Daudi ni kwamba utakuwa ni ukoo wa kifalme, kwamba wazao wote wa Kwanza wa Daudi walipakwa Mafuta na Mungu wawe wafalme soma (2 Wafalme 8:19,). Na ndio maana Bwana Yesu alipozaliwa katika nyumba ya Yusufu kama mzaliwa wa kwanza, roho ya kifalme ilikuwa juu yake. Kwahiyo kwa namna yoyote ile ni lazima angekuja tu kuwa Mfalme..

Je! Unajua kuwa Yusufu baba yake Yesu angepaswa awe mfalme wa Israeli kwa kipindi kile, kulingana na ahadi Mungu aliyomahidia Daudi?…Lakini kutokana na dhambi zao, Taifa la Israeli lilikatwa na uzao wa Daudi wa kifalme ukasimamishwa katika kutawala na ulisimamishwa kipindi gani?..

Kama ukisoma kitabu cha Wafalme, baada ya Daudi kufa, akafuata mwanawe Sulemani akawa mfalme kweli kulingana na ile Ahadi lakini naye pia akafa, na ikaendelea hivyo hivyo, kwa wajukuu na vitukuu vya Daudi, mpaka mfalme wa mwisho aliyetawala Yuda aliyeitwa Sedekia, ambaye alikuwa ni kitukuu cha 20 cha Daudi, huyu ndiye mfalme wa Mwisho kutawala Yuda, baada yake yeye, ndio Watu wakapelekwa Utumwani Babeli, hiyo ndiyo siku waliokatwa na waliporudi kukawa hakuna mfalme tena katika Israeli…vitukuu vya Daudi vilivyozaliwa baada ya Sedekia Mfalme wa Mwisho kufa, wakawa ni watu tu wa kawaida, kama watu wengine…

Ndio maana Yusufu baba yake Yesu alikuwa ni mtu wa kawaida tu maskini, ingawa alikuwa ni mwana wa kifalme…(Kwa urefu fuatilia ukoo huu wa Yesu kwenye kitabu cha Mathayo 1:1-17), laiti Israeli asingeasi na kupelekwa utumwani, Yusufu baba yake Yesu angekuwa mfalme wa Yuda, na Kristo angezaliwa huko…

Hivyo Israeli iliendelea kuwa kama mti uliokatwa baada ya kutoka Babeli…Wayahudi wakakaa mamia ya miaka bila mfalme….kukawa hakuna dalili yoyote ya Mfalme kunyanyuka katika uzao wa Daudi,..kwani Utawala wa Rumi ulikuwa umekamata dunia nzima, na Warumi waliwaweka watu wao kwenye makoloni yao yote, mpaka Israeli ilikuwa ni koloni la Warumi..Hivyo mtawala aliyetawala koloni la Israeli alikuwa ni Mrumi…jambo hilo liliendelea kwa miaka mingi…lakini Biblia ilitabiri katika Isaya Mlango wa 11 kuwa litatoka chipukizi katika shina la Yese….Kumbuka Yese alikuwa ni Baba yake Daudi, kwahiyo ni sawa na kusema litatoka chipukizi katika shina la Daudi au katika uzao wa Daudi. Tunasoma hayo katika…

Isaya11:1 “ Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda.

2 Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana”.
 
Tumekuelewa.
 
Mkuu nina mambo nilikuwa nayatafakari na katika andiko lako nimepata majibu niliokuwa najiuliza,,,umeenda deep kama msomi mzuri wa biblia,,,ubarikiwe...
 
Noted.🙏🙏
 
Tuliopata neema ya kumjua Yesu, tushikilie sana hiyo imani. Kwa mimi niliyewahi kushikwa mkono na Yesu, na akaongea nami moja kwa moja, itoshe tu kusema nimekuamini bwana, ninapoanguka ni udhaifu wangu tu na nashukuru kwakuwa hujawahi kuniacha nipotee. Hakuna alternative fact inayoweza kutolewa kwangu nikaamini otherwise kwakuwa nimeona mengi, tena ya ajabu! Usalama katika mikono ya huyu Yesu ni promised! Kila kitu kikiwa complimented na Roho mtakatifu kama alivyoahidi Yesu mwenyewe! Ni kitu gani kinachoweza kunitenganisha nawe Bwana, hakuna! Ombi langu ni uguse mioyo ya wale ambao bado hujawagusa! Waonje na kuuona wema wako! Amina!
 
MAANA YA YESU KULETA UPANGA NI KULETA NENO LA MUNGU.

Mathayo 10:34
“Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga.

Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
Waefeso 6:17

12 Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Waebrania 4:12

YESU ALIAHIDI KULETA AMANI.

27 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.
Yohana 14:27
 
ALIEKUJA NI MUNGU SIO NABII HIVYO NABII WA WAYAHUDI BADO HAJAJA BADO TUNA MSUBIRI KWA MADA HII NITAWAUNGA MKONO
 
Kama unaamini katika imani yako ,achana kabisa na mambo usiyoyajua au yasiyokuhusu kwanza kutokanq na maelezo yako moja kwa moja mimi siwezi kukujibu chochote maana tayari uko na majibu yako!!
 
Na endapo neno la uzima lingeshushiwa marekani sijui ingekuwaje kwakweli maana...! Wayahudi walitaka Mungu awaletee masihi wanaomtaka wao. Kumbuka magugu na ngano vipo pamoja, namna yakuvitenganisha ndio shida. Na hapa biblia haijahimiza kwamba Kuna uwezekano wakushepu magugu kuwa ngano hapana! Bali magugu ndiyo yanayohoji zaidi juu ya uhalisia wa Mambo lkn ngano inajua chakufanya.
 
Hongera hata Mimi amewahi ongea na Mimi maranyingi tu, na huwa nawashangaa ambao hawajapata neema hiyo lkn bado niwabishi sijui wataipataje. Kikiubwa Ni utii tu.
 
Anafikiri kwamba mtu ukifa basi Mungu anahuzunika Kama sisi wanadamu. Hahaha ukifa Mungu anafurahi kwakuwa unakuwa umetimiza adhabu yake, japo anasema sikifurahii kifo Cha mtu mwovu.
Ila kweli ukifikiria vizuri mungu angekuwepo asingeruhusu mtoto azaliwe amekufa au kilema
 
Nakukosoa kidogo japo Ni wa imani yangu, kabla yakula tunda adamu na Hawa sio kwamba walikuwa hawajui mema na mabaya hasha! Walikuwa wanajua mema tu. Ndivyo maandiko yanavyosema.
 
Mafundisho ya yesu yalibadilishwa sana.
Na huyu yesu anavyotukuzwa na kuhubiriwa leo Makanisani ni kinyume hata na mafundisho yake yeye mwenyewe.

Yesu hana uspesho wowote, uspesho wake ni kuwa alikuwa wa kwanza kujitambua kuwa yeye ni spesho, yani yeye ni mwana wa Mungu, lakini pia alitambukumbusha sisi sote ni wana wa Mungu.. hivo yeye ni spesho kwa kutuonesha kuwa binadamu wote ni spesho.

Wakatoliki waliamua kusema kuwa uspesho wa Yesu unaishia kwa Yesu peke yake....yeye pekee tu ndiye mwana wa Mungu hakuna mwingine.
Hapo ndiyo confusion na mchanganyiko unaoonekana leo uliooanzia.
 
Hoja unayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…