Sababu kuu zenye Mantiki zilizowafanya na zinazowafanya Wayahudi wengi Wasimuamini Yesu Kristo

1.Hoja za Kiyahudi na wewe pia zimekaa kiulimwengu zaidi na waliamini hivyo kumbe haiko hivyo.
2.Yesu alijaribu sana kuwafanya waelewe - lkn Wayahudi walikua ni watu wa nje zaidi.Ukisoma biblia kuna sehemu nyingi sana ambazo Yesu amewachallenge kuhusu mambo yote hayo uliyouliza.
3.Yesu alikuwa mwanafalsafa/mtu wa tafakuri ambaye alijaribu kuwaonesha watu upande mwingine wa uhalisia na ukweli wa maandiko.
4.Utawala unaosemwa kwenye vitabu vya dini za kale sio utawala kama wa CCM - ni utawala wa Kimungu - watu waokoke, waache maovu, waishi kwa amani, wapendane..
5.Yesu hakuja kwa ajili ya Wayahudi lkn alipitia middle east - uyahudi, palestina kwa sababu kipindi kile ndo eneo pekee lililokua hot cake ambalo kupitia hapo ulimwengu mzima ungepata kuelewa taarifa zake.Hapo palikuwa na Romans, Greeks, Wayahudi wenyewe- wazurulaji hawa - Arabs, Waafrika, Wazungu - pale watu wote walikuwa wapo..tofauti na kama angeibukia China, East Africa,Europe...n.k bado kungekwama sana.Yesu kutokea Middle East ilikuwa strategic..sio bahati mbaya.
6.Mungu hafungwi kabisa na mawazo ya wanadamu...jinsi unavyowaza wewe, hao wayahudi, sisi ni tofauti kabisa..Mungu hayupo kabisa kwenye hizi dimensions zetu - Yesu ambaye ni nafsi ya pili ya Mungu - alijitahidi sana kuonesha hilo jambo..mfano..Hivi what is CCM mbele ya Mungu?? (Hawa ndo watawala, na ndo ulitamani Yesu awe mtawala).Ili ujue kuwa tawala za binadamu ni kujilisha upepo...Wako wapi: ROMAN EMPIRE, BRITISH EMPIRE, OTTOMAN EMPIRE, RUSSIAN EMPIRE,GERMAN EMPIRE,NAPOLEON, HITLER, MUSOLLIN,STALIN, LENIN, MOMGOLIANI EMPIRE, JAPANESE EMPIRE, CHINESE EMPIRES n.k..vyote vilifutika - mambo yanabadirika - ni mambo ya kibinadamu na wala hayambabaishi Mungu - na Mungu anashangaa viumbe vya nyama hivi vinavyojitutumua..Ni kama tu ubavyoona polisi wanalaumiwa kwa upotevu wa watu n.k.(Utawala wa kidunia)...-Mungu hayupo huko na YESU hakuja kuwa polisi au Emperor wa hii dunia - yeye alikuja kuwakumbuka watu juu ya ufalme wa Mungu - watu waache dhambi - uasherati, uzinzi, wizi, ufisadi, uonevu, usengenyaji, uchoyo n.k tukifanya hivi ndo tunapata ufalme wa mbinguni sio bunduki n.k
6.Wakatoliki wanafalsafa moja kuwa :Kama kweli haya mambo ni ya Kimungu basi hata tuyapinge vipi yataendelea kuwepo tu, na huyo Yesu habari zake zitaendelea kuwepo miaka yote - sasa hivi ni more than 2000 yrs..ma wala hakuna mtu anashikiwa upanga....otherwise kama ni uwongo litajiishia jenyewe tu - hakuna haja ya jihad walakukatana vichwa...
 
Unaeleweka sana mkuu
 
Mimi nina swali dogo tu. Nilishawahi kufika Israel kikazi ni kweli hawakubaliani kabisa na Ukiristo sasa haya makanisa wanayoweka bendera ya Israel wanajua wanachofanya>?
 
Mimi ni Muislamu LAKINI amini nakwambia achana kabisa na huyo mtu aitwae Yesu. He is something else.
Yesu atabaki kuwa Yesu.

Kuhusu Wayahudi kutokumkubali isikuchanganye SANA mkuu, hata Yesu mwenyewe alisha sema Nabii hakubaliki kwao.
NABII HAKUBALIKI KWAO
 
Basi tu kwa vile tumezaliwa tukazikuta dini na imani zipo, otherwise kuna maswali mengi yanye majibu ya utata sana. Hawa wanaaamini utatu mtakatifu, hawa wanamwamini M.Mungu na mtume wake Muhammad S.A.W. Shida tupu!!

Kama ilivyo kwa demokrasia, dini pia imejengwa kwenye misingi ya utamaduni, desturi na mila. Afrika tunateseka sana kwa kuwa dini kuu za bara la Afrika zimetoka kwa watu. Hivyo ni desturi za kigeni zimeingia barani kwa kivuli za dini. Ndiyo maana kila dini hizo hutaja mitume wao wa kutoka kwenye maeneo yao na si Afrika. Pia huongea lugha zao na mazoea mengi ya huko inakotoka dini. Afrika inapata shida kuiga desturi ambazo siyo zao.
 
Ni sahihi Kabisa.
Leo tunajadili Imani ya Wayahudi kumhusu Myahudi mwenzao,

Sisi Afrika tunateseka kwa sababu watu wetu wa zamani hawaku document mambo muhimu kuhusu imani yetu. Hatukuandika mambo makuu kuhusu imani na mitume wetu. Matokeo yake imani yetu ilikufa kwa kukosa misingi ya rejea.
 
Sisi Afrika tunateseka kwa sababu watu wetu wa zamani hawaku document mambo muhimu kuhusu imani yetu. Hatukuandika mambo makuu kuhusu imani na mitume wetu. Matokeo yake imani yetu ilikufa kwa kukosa misingi ya rejea.

Kwa kweli tunasikitisha
 
Hiv
Hivi wayahudi original wanasali siku gani? Wanasali kanisani,msikitini,sinagogi au hekakuni
 
Ndo maana catholic kipaumbele chao ni katika imani yao ni bikira maria ambaye huwakilisha Mungu jike wa kirumi.
 
Nimechelewa kuiona hii, lakini naiweza kuijibu hata kwa uelewa wangu mdogo kabisa nilioupata kipindi najifunza biblia utotoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…