Sababu kuu zenye Mantiki zilizowafanya na zinazowafanya Wayahudi wengi Wasimuamini Yesu Kristo

Yesu mbona kauokomboa tayari ulimwemgu kwa wale watiifu kondoo wake ila wale wakaidi mbuzi hajakombolewa na majina yao hayapo katika kile kitabu..so pemgine mtoa mada na mimi ni muda wetu sasa wa kumfuatisha yesu na kuubeba msalaba wetu wenyewe km ambavyo yeye ameubeba msalaba wake .
 
Uislamu umetengenezwa na roman catholic.
 
Nyuzi za hivi hata ujibiwe namna gani, ligi itaendelea tu.

Tuwaache wayahudi na dini yao ya kiyahudi.
Mkiri kristo rohoni mwako si lazima mpaka uone wayahudi wamemkubali na wewe ndio umkubali.
 
Labda nianze na swali hili...

Mtu anaye mjua Mungu anakuwa na vigezo gani, utajuaje kama namjua MUNGU?

Hata Adamu aliumbwa akiwa hajui jema na Mabaya.
Hili ndio lilikuwa lengo la MUNGU binadamu asijue jema au baya.
Maana yake adamu asingekula tunda kamwe asingeweza kutambua jema au baya, na wanae(ambao ni sisi) wangekuwa hawajui jema au ovu.

Kujua kwetu maovu na mabaya (sisi binadamu wa leo) ni sababu adamu ali asi.

Hapa nakufungua kua kujua jema au baya siyo utashi wako wala akili yako ya saivi... Bali mema au mabaya unayajua toka ukiwa tumboni kwa mama.

Vizazi vyote vya adamu baada ya kuasi vyote vinajua mema na mabaya haijalishi kina akili au hakina.
Vivyo hivyo na kumjua Mungu akili na utashi havitumiki bali utamjua tu haijalishi una akili au hauna.
 
Nyuzi za hivi hata ujibiwe namna gani, ligi itaendelea tu.

Tuwaache wayahudi na dini yao ya kiyahudi.
Mkiri kristo rohoni mwako si lazima mpaka uone wayahudi wamemkubali na wewe ndio umkubali.

Tunachoangalia ni hoja zao, Kwa nini wamkatae,
Kisha tunaangalia hoja zao zinamashiko au wameghafilika.
Hilo ndio lengo la Mjadala.

Huwezi kukubali au kukataa kitu pasipo kukijadili, kukichambua, na kuona ubora na madhaifu.

Je Wayahudi wanahoja?
Au je Wakristo wako na hoja?
 
Acha hadithi za kusadikika jibu hoja.

Labda hao wayahudi wako kama walianzisha Ukristo na uyahudi lakini sisi waislam baba yetu wa imani ni nabii Ibrahim ambaye asili yake ni mkurudi kutoka Iraq na sio mayahidi.
 

Sasa mbona unasema kujua Mema na Mabaya ndio unakuhusisha na kumjua Mungu?

Yaani ukiibiwa au ukichukuliwa MKE au Mume kunauhusiano gani na kumjua Mungu?
Ilhali mambo hayo yapo automatically kulingana na maumbile ya Mwanadamu.

Kitendo cha kusema tuu unamjua Mungu au MTU yeyote akisema hivyo tayari anaingia kwenye kundi la Watu waongo. Tena waongo Wakubwa.

Huwezi mjua MTU ambaye hujawahi kumuona, kumsikia Sauti yake, kumgusa wala usiye na namna ya kumuelezea. Huo ni Uongo.
 
Duh! Huyu jamaa alitudiss Sana 🤔
 
Sio kweli.wapo Watu hawaamini na hawajui kuwa kuna MUNGU.
Yaani hata hiyo dhana tuu ya Mungu hawajawahi hata kuisikia. Watu wa hivyo wapo.

Watu wangekuwa wanamjua Mungu tangu wakiwa wadogo zisingekuwepo Dini
Kwahiyo uwepo dini ndio sababu ya kushawishi kuwa watu wanazaliwa hawamjui MUNGu... Sababu hiyo haina mashiko hata kidogo.

Dini ni mpango wa Binadamu kumtawala binadamu mwenzie, fikria dini ilifikaje Afrika.
Dini ni kwa ajili ya kunufaisha wachache wenye akili.

Leo watu wanajazana kwenda hija uarabuni, huoni jinsi gani watu wa uarabuni waliweka hija iwe kwao tu ili akili chache wapeleke hela zao kwa wananchi wa uarabuni?
Walijua wakiweka hija kwao kwanza wataongeza watalii kila mwaka na Mashirika yao ya ndege yatakuza biashara.

Kwahiyo lengo la dini ni kushikria akili yako ili utumike kwa ajili ya kuwanufaisha walio anzisha.
 

Naomba unipe maana ya msingi ya istilahi "DINI"
Achana na nadharia kuhusu Dini.
 
Kama ni uongo, nashindwa kuelewa sababu za kuleta uzi huu tujadili mambo ambayo ni uongo.
In short futa thread...

Huu Uzi hauhusu kumjua MUNGU Mkuu!
Embu usome VIZURI.
Uzi unahusu Wayahudi, Yesu Mnazareth na Unabii wa Masihi.
 
Acha hadithi za kusadikika jibu hoja.

Labda hao wayahudi wako kama walianzisha Ukristo na uyahudi lakini sisi waislam baba yetu wa imani ni nabii Ibrahim ambaye asili yake ni mkurudi kutoka Iraq na sio mayahidi.
Nabii Mussa je?Haruni? Nabii Suleman? Nabii Jona, Nabii Yusuf, Nabii Elisha, Nabii Eliah, Nabii Ezekiel, Nabii Yakobo(Israel mwenyewe), Mfalme Daudi, mfalme Sauli, Nabii Issa, Mariam na wengine wengi tu.
hawa ni wayahudi ndani ya Quran.

I mean Quran inataja wana waisrael mara nyingi kuliko hata inavyotaja waislam. Ni chizi tu atakayebisha influence ya uyahudi kwenye uislam.

Utaniambia Ibrahim ndio baba wa iman wa waislam lakini ukija uzao wa Ishmael hata haujulikani, ila uzao wa Isaka na yakobo unajulikana na umejaa kwenye Quran.
 

Mwambie Quran inawataja Wayahudi Kwa 90% kuliko huyo Ibrahim, Muhammad mwenyewe na jamii yoyote hapa Duniani.
 
Ndio wako sahihi kwa imani yao na jinsi wao walivyotafsiri maandiko.

Na ndio maana hata huu ukristo una madhehebi kibao kulingana na jinsi kila watu walivyoitafsiri biblia. Na kila mmoja yuko sahihi kwa kile anachoamini.

Labda useme tujadili kuhusu hicho wanachoamini na kwa nini wanaami ila kwenye usahihi, wako sahihi kulingana na mapokeo yao.
 
Dini na fasihi ni vitu viwili tofauti. Kwa taarifa yako mitume wote 12 walikuwa wayahudi. Manabii walikuwa wanapewa dokezo la kimungu nao wanaliandika au kulihubiri kibinadamu.
 
Huu Uzi hauhusu kumjua MUNGU Mkuu!
Embu usome VIZURI.
Uzi unahusu Wayahudi, Yesu Mnazareth na Unabii wa Masihi.
Unajitekenya then unajicheka.

Ni kipi alishindwa kuhakikisha kila binadamu anayezaliwa automatically, amjue Mungu na habari zake pasipo kufundishwa na yeyote, ili kuepusha kile kiitwacho uongo na habari zake kuingiziwa hadithi za Uongo. Huo ungekuwa muujiza mzuri na wala asingewapa Wanafunzi wake kazi ya Kutangaza habari zake na habari za Mungu

Hoja zangu nililenga kupinga hapo...
Wala sishughuliki na wayahudi tatizo lao ni lingine "hawana imani.*
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…