Juma alianza kuvuta bangi akiwa form 2. Ilianza kama utani wa marafiki — kuvuta mara moja baada ya shule, kisha ikawa kawaida. Baadaye akaanza kuwafundisha wenzake kuvuta. Wengine walimuona kama “mjanja” na mwenye connection. Haikuchukua muda akaanza kuwauzia kidogo kidogo ili apate hela ya matumizi.
Stanley yeye hakuanza kwa kuvuta sana, bali kwa kutamani maisha aliyoyaona kwenye muziki. Alikuwa anasikiliza nyimbo za wasanii kama Future na Rick Ross wakisimulia maisha ya pesa, magari na nguvu mitaani. Taratibu akaanza kuona biashara ya madawa kama njia ya kufika “level” fulani ya maisha.
Luka alikuwa na shida ya pesa nyumbani. Ada, kodi, na mahitaji mengine vilimlemea. Rafiki akamshawishi ajaribu kuuza “mara moja tu” ili atoke kwenye mkwamo. Alifanya hivyo, akapata faida ya haraka. Alijiahidi haitarudia — lakini alirudia.
Baada ya muda, kila mmoja wao alijikuta ameingia zaidi ya alivyotarajia. Na hapo ndipo swali linakuja: kwa nini ni vigumu kuacha?
Kuuza dawa za kulevya huwa ngumu kuacha kwa sababu hizi:
Unaanza kudaiwa “favors.” na wenzako fanya hiki na kile ili ubaki kwenye mtandao
Ukijaribu kuacha, unaweza kuonekana huna tena thamani, ukiacha kutoa rushwa huna cha maana tena
Badala ya kuacha, unajikuta umefungwa kwenye mfumo wa kimya kimya wa kulindana na kuogopana.
Kuacha si tu kuacha pesa — ni kuacha nafasi ambayo wengine watachukua.
Wengine hurudi kwa sababu hawataki kuonekana wameshindwa.
Kuacha ni kama kupoteza ngazi ya nguvu aliyokuwa ameifikia.
Na kwa watu wengi, kupoteza heshima ni jambo gumu kuliko kupoteza pesa.

1. Pesa ya haraka na kubwa
Biashara ya dawa mara nyingi:- Ina faida kubwa kwa muda mfupi
- Haina kodi
- Haina taratibu ndefu kama biashara halali
2. Mtego wa wateja (customer cycle)
Hata ukiwa independent:- Wateja wanakutegemea
- Wanakutafuta mara kwa mara
- Ukiacha, wanakuuliza au wanakushinikiza
3. Uraibu wa nguvu na udhibiti
Si pesa tu. Wengine huzoea:- Hisia ya kuwa na mtandao
- Watu kukutafuta
- Kuonekana “mwenye connection”
4. Hofu ya madeni au suppliers
Hata ukiwa huna gang:- Unaweza kuwa na mtu anayekuuzia mzigo
- Unaweza kuwa na madeni
- Unajua njia na watu
5. Psychological trap
Mara nyingi mtu hujiambia:Lakini:“Nitafanya kidogo tu nimalize malengo fulani, halafu nitaacha.”
- Malengo hubadilika
- Mahitaji huongezeka
- Kiwango cha maisha hupanda
6. “Favors” na rushwa.
Wakati mwingine mtu akikamatwa:- Husaidiwa kwa njia za panya kunasuka
- Huwaga sio bure, huwa kuna favors, ufanye kitu flani
Unaanza kudaiwa “favors.” na wenzako fanya hiki na kile ili ubaki kwenye mtandao
Ukijaribu kuacha, unaweza kuonekana huna tena thamani, ukiacha kutoa rushwa huna cha maana tena
Badala ya kuacha, unajikuta umefungwa kwenye mfumo wa kimya kimya wa kulindana na kuogopana.
7. Kuonekana Kama Tishio Ukiacha
Hata kama huna gang rasmi:- Watu wanajua unajua mambo
- Unajua suppliers
- Unajua njia za usambazaji
Na hofu hiyo inaweza kukufanya uendelee kimya kimya ili usionekane tishio.“Ataongea?”
“Atabadilisha upande?”
8. Ushindani na Vita ya Soko
Biashara ya madawa ina ushindani mkali:- Wauzaji wapya huingia
- Bei hubadilika
- Eneo linaweza kuvamiwa
Kuacha si tu kuacha pesa — ni kuacha nafasi ambayo wengine watachukua.
Wengine hurudi kwa sababu hawataki kuonekana wameshindwa.
9. Adventure na Msisimko wa Maisha ya Hatari
Kwa baadhi ya watu hatari inaanza kuwa kivutio- Kucheza na mipaka ya sheria huleta msisimko
- kukimbizana na polisi
- Kuishi kwa siri hujenga hadithi binafsi ya “niko tofauti”
10. Kulindwa na kujuana na “Big Players”
Wakati mwingine mtu anapanda ngazi:- Anaanza kusalimiana na watu wakubwa
- Anahisi yuko karibu na watu wenye nguvu
- Anapata ulinzi au taarifa za mapema
Kuacha ni kama kupoteza ngazi ya nguvu aliyokuwa ameifikia.
11. Heshima ya Mtaa
Katika baadhi ya mazingira:- Watu wanakuogopa
- Wanakuheshimu kwa sababu ya pesa
- Wanakuona kama mfano wa mafanikio ya haraka
Na kwa watu wengi, kupoteza heshima ni jambo gumu kuliko kupoteza pesa.
12. Kukosa Njia Mbadala
Baada ya muda:- CV haina historia halali
- Hakuna uzoefu wa kazi rasmi
- Hakuna mtandao wa kitaaluma