Uchaguzi 2020 Sababu kwanini CCM itashinda kwa kishindo

Sadock Kabuko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
1,166
Reaction score
1,075
Wakuu Heshima Kwenu.

Kwa hali ya siasa na kampeni zinavyoendelea ni wazi kabisa CCM itashinda kwa kishindo, kwa CCM mpya chini ya Dkt Magufuli CCM imesukwa vya kutosha iko imara na kwa uchaguzi huu CCM itashinda kwa kishindo zipo sababu kadhaa zitakazopelekea CCM kushinda kwa kishindo

1. Udhaifu wa upinzani Tanzania
Ni dhahiri kabisa upinzani wetu sio haujajikita kuchukua dola badala yake wamejikita katika kufanya majaribio ya kushika dola, sera na hata imani kwa wananchi ni dhaifu sana, wananchi wengi hawawamini wapinzani, ikiwa tu wameshindwa ndani ya vyama vyao kuaminiana na kuwa kitu kimoja, na wameshindwa kuungana na kusimamisha mgombea mmoja ni dhahiri kabisa upinzani hauko imara. Ikiwa wameshindwa hata kupeleka fedha za kuendeshea ofisi za wilaya na mikoa chama licha ya kuwa na ruzuku ni ukweli usiopingika wananchi hawawezi kuamini vyama vya namna hiyo.Kwani kuongoza nchi sio majaribio na kupitia sababu hii CCM itashinda kwa kishindo na wapinzani wataishia kulalamika kwamba wameibiwa kura kama ilivyo kawaida yao.

2. Uelewa wa wananchi kuhusu siasa
Wananchi wengi siku hizi ni waelewa na wanajua kuchambua mambo wanajua mbichi ni ipi na mbivu ni ipi hakika Rais Magufuli ameeleweka sana kwa wananchi, wananchi wamelewa sana siasa zake, ambazo ni za kuleta maendeleo watanzania, kwa nchi ilipokuwa imefikia tulihitaji siasa za CCM mpya chini ya Dkt Magufuli ili tuweze kupata maendeleo. Kitendo cha wanasiasa wengi kuhamia CCM imedhirika wazi kabisa na kila mwananchi anaelewa kabisa ni chama kipi kinachoweza kumletea maendeleo ya kweli, Aidha Raisi Magufuli ametuonesha sura halisi za wapinzani wengi wao ni wa roho wa madaraka na upinzani tanzania umeshikiliwa na watu wachache wenye masilahi yao binafsi.

3. Sera dhaifu za wapinzani
Kwa kampeni hizi zinazoendelea ni wazi kabisa wapinzani hawana sera za kumfanya mwananchi wa kawaida kuwaamini na kuwachagua mfano mzuri ni Mgombea kupitia CHADEMA ndg. Tundu Lissu, hakuna mwananchi ambaye hajui kwamba Tundu Lissu alipigwa risasi na hakuna aliyefurahia kitendo kile ndio maana hata viongozi wa CCM wakiongozwa na makamu wa Raisi Mh. Samia Suluhu walifika hospitali kumuona, kila mtu alifurahi kuona amelejea akiwa na afya njema.

Kwanini nimemtolea mfano ni miongoni mwa wagombea ambao hawana sera za kumshawishi mwananchi wa kawaida kumchagua kwa sababu sera zake nyingi zimejikita kukosoa maendeleo ambayo yameletwa na Raisi Magufuli, karibia nusu ya kampeni zake haelezi nini atawafanyia watanzania badala yake amejikita kueleza namna alivyopigwa risasi, kitu ambacho hakimshawishi mwananchi wa kawaida kumchagua. Kushindwa kwa wapinzani kuweka bayana mambo ambayo watawafanyia wananchi badala yake sera zao zimelenga kukosoa mema yaliyofanywa na CCM kwa kuyageuza kuwa mabaya.

4. CCM kukubalika miongoni mwa vijana
Baada ya Mh. Magufuli kuchagulia na kuisuka CCM, chama hiki kimeleta mvuto sana miongoni mwa vijana hii ni baada ya Magufuli kutekeleza yale ambayo vijana wengi walikuwa wakitamani kuyaona yakitendeka ndani ya chama, hivyo kupelekea vijana wengi kujiunga na CCM na kukiunga mkono chama. Aidha miaka ya nyuma ilikuwa ni dhambi kwa kijana kuvaa sare za chama, lakini kwa sasa vijana wengi hujivunia sana na kuona fahari kuwa wana-CCM. Sababu hii pia itakipa ushindi mkubwa

5. Upinzani kudanganywa na wanamitandao
Hakuna asiyejua kwamba wapinzani wengi hutegemea taarifa na propaganda za mitandaoni kama sehemu yao ya kupima uungwaji mkono jambo ambalo huwatanganya kwani asilimia kubwa ya wapiga kura hawana asses na mitandao ya kijamii, aidha wanapropaganda wengi hutumia lugha ya matusi,kejeli n.k kama njia mojawapo ya kuwafurahisha wamiliki wa vyama vyao. Kwanini CCM itashinda kupitia udhaifu huu hakuna asiyejua CCM imejikita sana kumsaidia mwananchi wa kawaida ambaye yeye maji,barabara,afya na umeme ndio kipaumbele kikubwa sana kwake. CCM kupitia Raisi Magufuli wamethubutu kuyatekeleza hayo. Vyama vya upinzani kwa kutengemea wafuasi wao ambao wamejawa na matusi na kejeli kupitia mitandao ya kijamii na wengi wao sio wapiga kura ni wapiga ramli watashindwa sana katika uchaguzi huu.

NB; Siku zote dawa hata kama ni chungu kubali kuinywa ili upone
 
CCM mnahangaika sana,

kura yangu ni LISSU.

Wauaji, watekaj, wasiojulikan,propaganda kam hiz, ukosef wa ajira, biashara kufa, watishia kuvunja amani wasipochaguliw,
kitaelewek mwak huu.
 
Watu tuliosoma sana wenye masters tunatumia Jf pia wale wa darasa la 7 wanatumia Facebook kwa wingi ebu jaribu kufatilia ugundue kitu Magufuli hatoboi safari hii.
 
CCM mnahangaika sana,
kura yangu ni LISSU.
Wauaji, watekaj, wasiojulikan,propaganda kam hiz, ukosef wa ajira, biashara kufa, watishia kuvunja amani wasipochaguliw,
kitaelewek mwak huu.

Wanachadema wana nguvu kubwa ajabu ila ni nyuma ya keyboards tuu..... wataongeaaa, watatukana, watatishia, watajiapiza kufanya mambo hahaha sasa subiri utekelezaje


Ndio utajua hili ni kundi la wasanii
 
Nadhani majibu unaanza kuyapata kwa sisi wachangiaji..kifupi CCM ni chama Chakavu, sera zake ni za Kisoshalisti. Lissu anachukuwa nchi mapeema kabla kuku hazijarudi ndani!
 
CCM mnahangaika sana,
kura yangu ni LISSU.
Wauaji, watekaj, wasiojulikan,propaganda kam hiz, ukosef wa ajira, biashara kufa, watishia kuvunja amani wasipochaguliw,
kitaelewek mwak huu.
Mpe tu huyo Msaliti Lissu wako kwani kuna mtu amekukataza kumpa?
 
Wanachadema wana nguvu kubwa ajabu ila ni nyuma ya keyboards tuu..... wataongeaaa, watatukana, watatishia, watajiapiza kufanya mambo hahaha sasa subiri utekelezaje


Ndio utajua hili ni kundi la wasanii
Wee mke Wa Baba D acha kuweweseka!
 
Bao la mkono na hila ndio ngao ya ccm.
 

Hizi propaganda zako ziko kila siku humu, tofauti yako na wenzako ni kwamba ww umeziandika kwa kuweka paragraph. Ccm sio chama imara, ila kimepata mwenyekiti mwenye cheo cha urais, na anatumia madaraka hayo vibaya kukibeba chama chake. Na anachofanya kupitia madaraka yake, ni kushurutisha yeye na chama chake kuonekana kinakubalika fullstop.
 
Yaani kuna nyuzi nyingine ukiziina unajua kabisa huyu aliyeandika ni mchumia tumbo,kanjanja au mtu furani hivi aina ya Firauni( kibri). Huwa nawalaani sana watu kama hawa wanafiki Mungu awaongezee adhabu !
 



nlikwambia 6, hawa hata siwajui ila jipangen
 
Wanachadema wana nguvu kubwa ajabu ila ni nyuma ya keyboards tuu..... wataongeaaa, watatukana, watatishia, watajiapiza kufanya mambo hahaha sasa subiri utekelezaje


Ndio utajua hili ni kundi la wasanii
maandamano ya Mange?wacha porojo wewe.
 
Mwaka 2012 Mnyika wa CHADEMA alisema rais Kikwete ni dhaifu


Mwaka 2015 Kikwete akaleta rais ambaye siyo dhaifu; CHADEMA wakalia faulo kwa nini CCM imebadilisha kibao
 
Mwaka 2012 Mnyika wa CHADEMA alisema rais Kikwete ni dhaifu


Mwaka 2015 Kikwete akaleta rais ambaye siyo dhaifu; CHADEMA wakalia faulo kwa nini CCM imebadilisha kibao
CHADEMA kuwa elewa lazima uwe na degree ya upumbavu na urofa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…