Sababu Mbalimbali za Wakongwe hawa kuachana na Muziki

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Baadhi ya Wasanii Waliowahi Kutangaza Kuachana na Muziki

Suma Lee
Msanii huyu aliyetamba na wimbo wake wa "Hakunaga" alitangaza kuachana na muziki 2015 na kuamua kumrudia Mungu. Alisema nyimbo zake zilizobaki studio zisimame na zisitoke tena.

Mzee Yusuf
Alitangaza kuachana na muziki mwaka 2016. Alitoa ombi kwa watu wote wenye CD zake pamoja na vyombo vya habari kuacha kupiga nyimbo zake, kwani ameamua kumrudia Mungu.

Vanessa Mdee
Kupitia podcast yake ya "Deep Dive with Vanessa Mdee" alitangaza rasmi mwaka 2020 kuwa anaachana na shughuli zote za muziki. Alisema amekuwa akikabiliana na msongo wa mawazo kwa muda mrefu kutokana na shughuli za muziki.

Snura Mushi
Akizungumza na waandishi wa habari Julai 29, 2024, Snura aliomba nyimbo zake zisitumike kwenye vyombo vya habari pamoja na watu binafsi na pia kuacha kupost picha zake za zamani zisizo na maadili.
 
Hao ambao wanazuia tusisikilize nyimbo zao huwa wanakuwaje zikiendelea kusikilizwa? Wanaungua, wanawashwa wanaumwa majini yanawachapa bakora huwa ni nini!

Unamzuiaje mtu kutizama/kusikiliza kitu alichonunua kwa pesa yake kwa njaa zako?
 
Baadhi ya Wasanii Waliowahi Kutangaza Kuachana na Muziki

Suma Lee
Msanii huyu aliyetamba na wimbo wake wa "Hakunaga" alitangaza kuachana na muziki 2015 na kuamua kumrudia Mungu. Alisema nyimbo zake zilizobaki studio zisimame na zisitoke tena.

Mzee Yusuf
Alitangaza kuachana na muziki mwaka 2016. Alitoa ombi kwa watu wote wenye CD zake pamoja na vyombo vya habari kuacha kupiga nyimbo zake, kwani ameamua kumrudia Mungu.

Vanessa Mdee
Kupitia podcast yake ya "Deep Dive with Vanessa Mdee" alitangaza rasmi mwaka 2020 kuwa anaachana na shughuli zote za muziki. Alisema amekuwa akikabiliana na msongo wa mawazo kwa muda mrefu kutokana na shughuli za muziki.

Snura Mushi
Akizungumza na waandishi wa habari Julai 29, 2024, Snura aliomba nyimbo zake zisitumike kwenye vyombo vya habari pamoja na watu binafsi na pia kuacha kupost picha zake za zamani zisizo na maadili.
Hivi Snura naye ni mwanamuziki!!?? Hebu kuwa serious basi.

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom