Wakuu mimi ninajiuliza kwanini walioko kwenye ndoa wanataka kutoka na walioko nje wanataka kuingi wakti kilasiku wanasikia mikiki mikiki kilasiku kwenye vyombo vya habari hata kwenye mazingira tunayohishi wanaona! lakini wao wanakuwa kama Nyumbu??wanaenda tu!!:thinking:
Walioko ndani wanataka kutoka kwa sababu hawajui maana yaa ndoa nini na hawajui kupenda na kuvumilia maana ndoa si BF& GF wengi bado
wanadhani wameowa/kuolewa na watu wasiyokuwa chaguo la kweli kumbe hata wakipewa wengine kama kungekuwa na uwezekano bado watataka kutoka tu. Wanabaki kusema ''wewe umebaatika kumpata yule mnayependana'' bila kujiuliza hao wanapendana wanawezaje kuidumisha ndoa yao na kuishi kwa Amani. Hata hizo ndoa chungu zinasababishwa na wanandoa wenyewe na si mtu mwingine. Wanandoa wanadhani furaha, Upendo na Amani vimewekwa kwa watu baadhi kumbe ni kwa wote, watu tunapaswa kufanaya wajibu wetu na kukumbushana pale mmomoja anapojisahau maana sisi binadamu si malaika.(Zaidi Kumshirikisha Mungu na kuwa na Mwasailiano bora ndani ya wanandoa)