Sababu tano za kufa kwa Bongo movie

ShyaRuwa

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2015
Posts
7,895
Reaction score
13,643
1.MAPENZI NA NGONO:Ngono ni moja kati ya sababu kubwa za mtu hasa wanawake kuingia kwenye industry.Kama mdada ana makalio makubwa, nyonyo za kueleweka na factors nyingine zenye kuamsha tamaa za mwili basi huyo amefuzu kuwa actress hata kama hana kipaji chochote.Unapotumia ngono kama chujio kwenye interview, unakusanya makapi na wenye vipaji wanachujwa kisa sababu ya mionekano yao.

2.TAMAA NA UBINAFSI:Unakuta movie moja ambayo mtu mmoja ndiye: Star, director, editor, producer, script writer and so forth. Yaani akili ya mtu mmoja inaongoza positions zaidi ya tano.Siku ikitokea huyo mtu amepatwa na tatizo, karibu kampuni yote inatikisika.Kwanini wasitafute watu tofauti tofauti kwenye positions mbalimbali ili kuingiza akili nyingi na mawazo ya watu wengi kwenye production?

3.UWEZO MDOGO WA KIAKILI:Kubali au kataa lakini asilimia kubwa ya waigizaji wa bongo movie ni wale wenye uwezo mdogo kiakili, ambao walijishawishi kuwa hawakupewa akili za darasani ila vipaji vya sanaa, wasijue akili ndio mzizi wa kila kitu.Matokeo yake ni kukosa fertile imaginations, creativity, and other mental fore steps zinazotumika kwenye sanaa.Mbadala wake wameishia kukopiana kazi zao, ku-reflect matukio ya kwenye jamii kama vile mauaji ya maalbino na vikongwe, ndoa na uasaliti na mapenzi kwa ujumla.Vitu ambavyo havimsisimui hadhira maana alishavizoea.

4.MADAWA YA KULEVYA:Madawa ya kulevya ni sababu na ni matokeo ya kufa kwa bongo movie.Ni sababu kwa maana wakishatumia madawa uwezo wa kazi unapungua.Wanakuwa wamesizi kwa muda mrefu zaidi ambao walitakiwa wafanye kazi, pia wanatumia pesa nyingi kununulia unga.Ni matokeo kwa maana wakishafulia kwenye uigizaji wanabakiwa na jina bila pesa.Ili kuendelea ku-keep reputation yao wanakubali kuwa punda wa kubebea unga ili wapate namna ya kuishi mjini.

5.KUTUMIKA KISIASA:Kama nilivyosema, hawa watu uwezo wao kiakili ni mdogo.Wanajiingiza kwenye chama cha siasa kama industry yote bila kujali hadhira wao ni vyama tofauti tofauti na wengine hawana vyama.Hawajui kwamba kama tasnia kujiingiza kwenye chama wanaonekana kama vile ni kitengo cha chama fulani.Ikiwa hadhira ana chuki na chama mlichojiunga nacho, basi ile chuki inasambaa hadi kwenu na mwishowe hakutakuwepo na wa kununua kazi zenu.Baada ya kutapeliwa kwenye kampeni za 2015 na kutengwa na wananchi walio wengi, leo hii hakuna anayewataka, si hadhira wala chama na serikali yake. Wamekufa kibudu kama TBC na sasa wanatumia mabavu kulazimisha watu wanunue kazi zao.
 
Movie inaanza watu wanakumbatiana na kupelekana gesti wanalala wakitoka wanapanda noah au range rover wanaenda beach wakirud wanakaa kwenye masofa movie inaishia hapo watch out part 2 hivi makonda unamshawishije mtu kununua hizi movie uchwara za kibongo
 
CHARMILTON,

Spot on!

Kila binti aliyeshiriki umiss lazima aingie Bongo Movie

Akina Mercy Johnson, Uche Jombo walishiriki wapi umiss?

Si kila mtu anaweza Director au script writer mzuri
 
Spot on!

Kila binti aliyeshiriki umiss lazima aingie Bongo Movie

Akina Mercy Johnson, Uche Jombo walishiriki wapi umiss?

Si kila mtu anaweza Director au script writer mzuri
Unaona? yaani wao wanatumia physical appearance kama kigezo cha kuigiza ilihali uigizaji unahitaji mental ability.
 
CHARMILTON,
Sababu zako zina ukweli kwa kiasi kikubwa lkn hakuna ubabe unaotumika kulazimisha kazi zao zinunuliwe bali wanataka fair ground ya kuuzia kazi zao. Kwa mfano maduka ya kkoo wamefunga wenyewe ili wapaze sauti zao kwa serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…