Sababu ya CHADEMA kutokuwa na mvuto kwa wafadhili wa mataifa ya nje

Sababu ya CHADEMA kutokuwa na mvuto kwa wafadhili wa mataifa ya nje

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Chama chochote cha siasa huwa na agenda yake ambayo huwa ndio roho ya chama

Chadema kipindi cha Dk Slaa kilikuwa na agenda tena nzito ambayo ilikubalika na ilitikisa ndani na nje ikipigiwa makofi ndani ya nchi na nje ya nchi.La kujifunza kwa Dk Slaa ni kuwa Dk Slaa hakutetea maslahi binafsi alijikita kwenye hoja moja kuu mno ya kupambana na mafisadi wa ndani wezi Wa pesa za wafadhili na wakopeshaji wa nje.

Wafadhili na wakopeshaji wa nje wakaiona Chadema kama chama bora kinachohakikisha mikopo na misaada ya wafadhili wa nje haifujwi ndani ya nchi kikapata uungwaji mkubwa wa ndani na nje .Wafadhili na wakopeshaji wakaiona Chadema kama jicho lao ndani ya nchi la kuhakikisha pesa zao haziibiwi wala kufujwa.

Sasa hivi Chadema kimebaki tu chama cha majungu na vitu hewa vya kutunga.

Hawana agenda wamekaa tu kudakia dakia vitu na matukio tofauti na kipindi cha Dk Slaa ambaye kwake agenda kuu haikuwa kupambana na serikali, bali kupambana na wezi mafisadi wa fedha za wafadhili na wakopeshaji wa nje.

Kama mbwa koko bila agenda yeyote ya maana ya kisiasa ya kueleweka ndani ya nchi na nje ya nchi akawa focused na serious kwenye hili bila kuyumba, akasaidia hadi CCM kujisafisha na kuwapiga mateke nje mafisadi papa akina Lowassa.

Chadema ya sasa agenda yao ya maana in ipi anayeijua, tafadhali Mimi naiona haina agenda yoyote zaidi ya kudakia dakia tu matukio na kuyatolea matamko.

Sio siri Chadema choka mbaya ikihitaji wabadili uongozi waweke damu mpya zenye fiktlra mpya pengine zingekuja na new agenda ya kueleweka kwa wananchi na wafadhili na wakopeshaji.
 
Waziri kafariki ghafla akiwa ni mbunge watatu ndani ya wiki mbili kufariki ghafla. Wewe badala utoe ushauri watanzania tufanye nini kuangalia hili jambo, unaamka na mada za kukuwasha kuhusu CHADEMA. Ila Lema na Mdee walisema kina Kibajaju na Msukuma wakawatukana. Bado wiki mbili.
 
Alafu kibaya zaidi inawafuata wao
Mtoa post trend kubwa sahizi duniani ni corona.
Dunia nzima inahangaika kutuliza hii hali kwa gharama na njia yotote ile.
Toka jana naona unajitahidi sana kuanzisha nyuzi za siasa ili kuwahamisha watu kutoka kwenye lengo. Uzuri mmoja wamekushtukia.
Tafuta njia nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app

In God we Trust
 
Ukisema Dr Slaa alikuwa hapambani na serikali anapambana na mafisadi wa pesa zinazokuja kwa ajili ya maendeleo ya nchi mzee nikikuuliza hizo pesa za miradi ya nchi huwa zinashikiliwa na nani utanijibu nini?

Walokuwa wanakula hizo pesa ni nani kama siyo watumish wa Serikali ambao kimsingi ndo serikali yenyewe umepuyanga boss, afu tuoneshe andiko lolote na popote ulipowahi kumsifia Dr Slaa wakati yupo CHADEMA anapambana na hao jamaa au ndo kwa kuwa katoka huku ndo umeamua kumtumia kama reference?

Swali la mwisho so tangu Dr slaa kaondoka CHADEMA hakuna kitu imefanya,imekemea,imekosoa chenye mashiko?..upuuzi na unafki juzi tu wametoka kushauri habari ya LOCKDOWN mkabisha ina tunavyopukutika, Leo balozi Mahige hatujui kesho na keshokutwa nani..acha unafki
 
Back
Top Bottom