Sababu ya Kain kumuua Abel ni upendo

Sababu ya Kain kumuua Abel ni upendo

Frustration

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,134
Reaction score
4,124
Habari wana jukwaa na poleni kwa mahangaiko ya kusaka ridhiki

NB: Mungu alimwambia Adam utakula kwa jasho lako na ww Hawa utazaa kwa uchungu (No mercy).

Pamoja na adhabu hii tunayoipitia ila hatukati tamaa na dunia yetu kwani tunaipenda.

Wengi wamekuwa wakiupotosha uma kwa kusema sababu ya Kain kumuua nduguye Abel ni wivu wa mapenzi. Hii sio sababu na hakukuwa na kitu kama hiki na hakipo popote duniani.

Sababu iliyopelekea Kain kumuua Abel ni baada ya Kain kuhisi amekosa upendo toka kwa wazazi wake pamoja na Mungu.

Kiuhalisia Kain alipata upendo ila alikuwa anafananisha na ule aliokuwa anapewa Abel.

Kwa shinikizo la shetani Kain alitekeleza mauaji yale peupeee shambani kwake kwa kumtanguliza Abel kwa lengo la kwenda kumuonyesha Abel mazao yake shambani.

Karibuni kwa pongezi na kuongeza nyama.

Copyright Frustration
 
Umejizungusha we lakini umekuja kwenye maana ile ile kuwa alimuua kwa wivu. Kwa maana ya kiswahili fasaha alimuonea kijicho mwenzake, ndio maana akamuua. Mungu anatupenda wote sawa, kama alivyompenda Cain na Abel. Ila Mungu alipenda sana sadaka za Abel kushinda Cain, kwa sababu Mungu anaona ndani yenu. .

Unaweza kutoa kitu hata kwa mtu ila usitoe kwa moyo au ukatoa kitu usichohitaji, sasa Mungu anapenda sadaka za kutoka moyoni. Cain alikuwa na Frustration zilizoletwa na wivu. .
 
Kanisani kwetu tulipokua wadogo tulipenda sana hilo somo la Kaini na Abel ninachojua Kaini alimuua nduguye sababu ya wivu, walivyotoa sadaka ya kuteketeza sadaka ya Abel ilipokelewa moja kwa moja mwenzake akamuonea wivu akamuua!!!!
 
Kanisani kwetu tulipokua wadogo tulipenda sana hilo somo la Kaini na Abel ninachojua jua Kaini alimuua nduguye sababu ya wivu, walivyotoa sadaka ya kuteketeza sadaka ya Abel ilipokelewa moja kwa moja mwenzake akamuonea wivu akamuua!!!!
Upo sahihi kwa kuwa Kain alihisi hapendwi. Ila kuna watu wanasema kisa alitaka amuoe aliyezaliwa naye na sio yule kutoka kwa Abel
 
Back
Top Bottom