Nani asiyejua kuwa Mwinyi ndiye aliyepanda hii mbegu ya ufisadi inayolisumbua taifa? Bahati yake nzuri huwa hatajwi tajwi. Hata huu msukule wa Kikwere unaotusumbua aliuumba yeye alipoupa uwaziri. Ila wabongo wajifunze unapofika uchaguzi wasichague tena wababaishaji kama huyu tuliye naye. Yeye pesa ikiporomoka hajali bali kuendelea kutanua na shostie wake. Sarafu hata itokomee haimuhusu. Yake ni matanuzi.
mh kama aliukwa basi hatari huko boy n ahazina kila anayeshika ngazi hiyo lazima isemekane amaukwaa kwanza ama?
'Intelijensia' zilisema ni tatizo la kawaida tumbo kuleta tatizo unapokula vyakula usivyozoea!!!!
Kibona alikuwa ni Waziri wa fedha, naye Rutihinda alikuwa ni Gavana wa Benki Kuu.
Hawa jamaa wazalendo, walikataa kuprint fedha na kuziingiza kwenye system kwani walijua wakifanya hivyo mfumuko wa bei na ugumu wa maisha ungeongezeka.
Bwana mkubwa kwa hasira za kukataliwa ombi lake akawapeleka India, waliporudi kutoka huko wote wakaanza kuumwa, na bwana mkubwa akatueleza kuwa wamelishwa vyakula vya Kihindi hivyo basi, walikumbwa na tumbo la kuharisha kwa sababu ya ugeni wa chakula cha Kihindi.
Hawakukaa muda mrefu, wakafa. Je ni kweli walidungwa sumu iuayo taratibu? Au ndio kifo chao kilikuwa chakawaida tu?
Ingekuwa ndiyo hivi basi hata Mrema aliyekamata dhahabu airport angeshapotezwa
hili nalo neno la ukweli mnoNa kweli Mwinyi alitimiza matakwa yake baada ya kufa Rutihinda na Kibona kwani ndio wakati huo baada ya vifo vyao, akawateua Kighoma Alli Malima kuwa waziri wa fedha na Idris Rashid kuwa gavana wa benki kuu!!Huyu mzee alikuwa mchafu sana na ndiye aliyetuletea balaa zote hizi nchini mwetu na juu ya hayo anataka kumrithisha mwanae Hussein utawala wa nchi yetu; hilo haliwezekani waende wakale hizo pesa walizotuibia kupitia kwa Ladwa!!
They are dead already!mbona wanaosoma india hawafi?
Hi habari imekaa ki-Mtikilatikila, miaka ya '90 wakati wa siasa za uzawa na mageusi tuliizungumza sana kama propaganda dhidi ya watawala wakati huo, mitaani Dar watu walifikia kuamini kuwa hawa watu waliuliwa kwa sumu hadi walioianzisha nao wakafikiri ni ukweli.
Ukweli ni kwamba hawa marehemu ni miongoni mwa waathirika wa mwanzo wa HIV na wakati ule uelewa haukuwa mkubwa na kulikuwa na unyanyapaa sana kiasa cha kudhania waheshimiwa viongozi hawawezi kudhaniwa haka kaugonjwa.
yaliyopita si ndwele tugange yajayo
Hebu tupe zaidi kuhusu haya uliyoandika...Yako mengi mengi kidogo ya kutafiti. Vipi suala la kupunguza nguvu ya Wakristo?
Nani anayejua sababu ya Mzee (Marehemu sasa) Makweta kukwepa madaktari wa serikali badala yake wakawa wanatibiwa privately kabisa?
Nani anayeweza kujua mauaji ya watoto wa shule ya shauritanga na jinsi yule mpelelezi wa nje alivyouawa moshi kabla hajafika Dar kutoa report yake na nyaraka zake kupotea. Na halafu serikali ikatangaza kwamba ulikuwa moto wa mshumaa wakati hapo shuleni palikuwa na umeme muda wote na palikuwa na marufuku ya mishumaa na pasi mabwenini?
Nani mwenye kujua jaribio la kuchomwa kwa shule ya Karaeni na baada ya kuvuja kwa taarifa, watoto wote kujikuta wako nje ya bweni saa sita usiku, mabanda ya mifugo yakiwaka moto?
Nani anayejua yle mtoto Mwajuma, aliyekuwa amemnong'oneza rafiki yake juu ya kuwashwa shule usiku alipohojiwa alisema nini? Kutokana na habari za yle mtoto, nini kilijiri dar wakti watoto hao wakiwa likizo? Ni assignments gani walipewa?
Jamani nchi yetu hii!!!!!!!!!!!!!!!!!