Naomba kujua yafuatayo..
> Umri wako na huyo binti?
> Shughuli unayofanya nje ya masomo(umesema utamtibu kwa gharama yoyote)
> Yeye anaishi kwa nani yake na ana shughuli gani ya kiuchumi?
> Je uliwahi kwenda naye hospitali kuhakikisha kwamba ni kweli ana tatizo alilokuambia?
> Ikiwa umemtambulisha kwenu, je kwao aliwahi kukutambulisha kama ni mtu wake wa karibu?
> Umewahi kupeleleza kwa ndugu au watu wake wa karibu ikiwa ni kweli ana tatizo alilokuambia?
> Unadhani alipokuambia usimwambie mtu kama mmeachana alikuwa na maana gani kwako?
> Je ulimuelewa vipi alipokuambia kwamba, muachane tu, ila akipona tatizo lake la kizazi atakujulisha ili muendelee kimahusiano?