Sababu ya kocha Simba SC kutomuingiza Kagere

Sababu ya kocha Simba SC kutomuingiza Kagere

KAGERE alipewa nafas ile gemu ya Al ahly away akaanza kabisa From 1st minute.

Alichokicheza mule kila mtu alikiona, Ni garasa mara 100 ya Mugalu.
Mugalu anapoteza nafasi kibao karibia kila mechi ila kocha anakomaa nae tu, kwanini asimbadilishe na Kagere kama yuko fair?
 
Kiukweli huu mjadala wa Kagere ni mpana sana kwa sababu hapa jamvini wapo wanaotazama mpira mpira kiufundi na wapo wanaotazama mpira kiushabiki. Kwa upande wangu ngoja nijaribu kuwatazama washambuliaji wote watatu wa Simba kwa jicho la tatu na natangulia kusema kuwa huu nimtizamo wangu na nipo tayari kukosolewa kwani ndio siri ya kujifunza zaidi.

Kagere ana "foot work" mbovu sana. Hanyumbuliki kabisa. Hawezi kupiga chenga, akiwa mshambuliaji wa mwisho hawezi "kuhold" mpira mpaka wenzake waje, hawezi kutoa pasi za mwisho vizuri na hana mbio/kasi. Magoli yake mengi mpaka atengenezewe kwenye njia, hajui "kujiposition. Ufanisi wake unazidi kushuka kadiri umri unavyozidi kwenda. Kagere wa mwaka huu sio yule wa mwaka juzi ambaye alikuwa moto. Sitaki kuamini kuwa benchi ndio limemfanya hivyo kwani hata kwenye mechi za ligi ya nyumbani anazopewa nafasi bado haonyeshi kiwango alichokuwa nacho misimu miwili/mitatu iliyopita na nimemshuhudia mara mbili akiokoa mipira iliyokuwa inaingia wavuni kwenye goli la timu pinzani badala ya yeye kumalizia kufunga. Kwenye mechi za CL mwaka huu alizopewa nafasi hakuwa tishio kabisa. Kagere wa sasa hivi analikimbia "box" wakati yeye ndio mshambuliaji wa mwisho wakati Kagere wa misimu miwili mitatu iliyoisha alikuwa anazunguka kwenye "box"la timu pinzani dakika zote 90. Mpira wa kisasa mabeki wakati ndio huanzisha mashambulizi kwa hiyo kitendo cha Kagere kukimbia "box" la timu pinzani kunawafanya waanzishe mashambulizi kwa nafasi na hivyo kusababisha Simba ishambuliwe.
Kagere ni mzuri sana kwa vichwa, mashuti yake mengi ni "on target", ana maamuzi ya haraka na hakati tamaa mpaka aidha aone mpira umetoka nje, umeingia golini au kipa kadaka. Na hili la kutokukata tamaa ndio linatakiwa kwa washambuliaji wote kwani Kagere ameshawahi kufunga magoli mengi ambayo watu walikuwa hawategemei kabisa. Na kikubwa zaidi ka Kegere ni ule uwezo wake wa kusoma mabeki wa timu pinzani wakati wanarudisha mipira kwa makipa wao wasipokuwa makini huwa wanakuta wamemtengea Kagere badala ya kipa wake. Kagere anapata shida sana kwenye mfumo wa kutumia mshambuliaji mmoja lakini ukitaka kuuona uzuri wa Kagere ni pale tu unapotumia washambuliaji wawili.

Mugalu ana "foot work" nzuri sana. Ana umbo kubwa zuri sana linalohitajika kwa mshambuliaji wa kati. Anaweza kupiga chenga kiasi, akiwa mshambuliaji wa mwisho anaweza kuhold mpira mpaka wenzake wafike, anaweza kutoa pasi za mwisho vizuri ila na yeye hana mbio/kasi na hawezi kukokota mpira umbali mrefu. Hanyumbuliki kabisa yaani akigeuka ni mzima mzima. Magoli yake mengi na yeye mpaka atengenezewe kwenye njia kama mwenzie Kagere, ila najua sana "kujiposition" na huwa haondoki kwenye "box"la timu pinzani hili huwanyima nafasi mabeki wa timu pinzani kusogea mbele. Ufanisi wake unaanza kushuka kwa kasi sana kwani Mugalu aliyeanza msimu alikuwa anafunga sana tena akitokea benchi na kupewa dakika chache wakati mwingine hazizidi hata kumi lakini alikuwa anatupia. Mugalu alikuwa ana uwezo wa kufunga kwa miguu yote miwili na hata kwa kichwa. Alikuwa anauwezo wa kufunga kiufundi na hata kwa mashuti lakini huyu mwamba sijui kakumbwa na nini. Yaani sasa hivi anakosa magoli ya wazi kabisa ana amekosa kujiamini kabisa. Ana kata tamaa haraka sana hafiki kwenye mipira ya mwisho na hata mipira ya vichwa akiwa peke yake (fee header) bila kukabwa na beki wa timu pinzani inamshinda. Msaada mkubwa aliokuwa nao kwa sasa kwa Simba ni ule tu wa kuzuia timu pinzani zisianzishe mashambulizi kwa kutumia mabeki wa kati basi. Jukumu hilo amelitendea haki na kutoa mchango mkubwa kwenye mechi zote Simba alizocheza kwenye CL. Uwezo wake wa kuwazuia mabeki wa timu pinzani kusogea mbele ndio unampa nafasi ya kupangwa mara kwa mara na Gomes kwa sababu muda mrefu Boko alikuwa majeruhi. Huyu mwamba yeye mifumo yote miwili ya mshambuliaji mmoja au wawili kwake yeye poa.

John Boko yeye namuona kakamilika zaidi kuliko hao Mugalu na Kagere ila tatizo lake kubwa ni majeruhi na umri. Kwa takribani misimu mitatu mfululizo sasa John Boko amekuwa anapata majeraha yanayomuweka nje kwa miezi kadhaa na anaporudi inamchukua muda kiasi
(kupata match fitness) kurudi kwenye ubora wake. Ila akirudi kwenye kwenye ubora wake na gari likiwaka sawa sawa anakuwa msaada mkubwa sana kwa Simba. Uzuri wake yeye ananyumbulika vizuri, chenga anaweza, "kuhold" mpira mpaka wenzake wafike anaweza, ana kasi/mbio japo si sana lakini zinatosha kwa mshambuliaji wa wakti, anakaba kuanzia mbele, hakati tamaa kabisa wakati anafuata mipira ya mwisho mpaka utoke nje au kipa adake, anahama kwenye "box" kwa wakati na arudi kwenye "box" kwa wakati, anajua kupiga pasi za mwisho vizuri, mashuti anapiga vizuri na hata vichwa anaruka vizuri sana na analenga goli vizuri. Mapungufu kwa Boko ni pale anapokuwa uso kwa uso na goli kipa mara nyingi anakosa mbinu za kuwachmabua magolikipa. Boko wa miaka mitatu iliyopita alikuwa mchoyo wa pasi za mwisho akitaka kufunga mwenyewe hata kama mwenzake yupo kwenye nafasi nzuri lakini baada ya kupigiwa kelele sana somo likamwingia sasa hivi anacheza kwa ushirikano na wenzake pale kwenye fowadi ya Simba kiasi siku hizi sio ajabu tena kumuona Boko akitoa ässist" kwa wenzake. Kikubwa zaidi kwake ni aina yake ya uhamasishaji kwa wenzake akiwa uwanjani. Boko yeye mifumo yote miwil ya mshambuliaji mmoja au wawili yote anaiweza vizuri sana.

Kwa hali ilivyo sasa na "level" Simba ilipofika Boko ndiye mshambualiji anayetakiwa kubaki Simba. Lakini ni lazima Mo aache kununua gari la kifahari "Rolls Royce" kama alivyoahidi ili apatikane mshambuliaji mwenye sifa zifuatazo:-
1. Mwili kama wa Mugalu
2. Akili, unyumbulifu na chenga kama za Chama
3. Urefu kama wa Boko
4. Kasi kama ya Miquisone
5. Mashuti kama ya Ndemla
6. Kutokukata tamaa kama Kagere.
7. Pumzi kama za Muzamiru
8. Mbabe kama Lwanga
Akipatikana mshambuliaji mwenye muunganiko huo hapo juu (1 - 8) hata kwa asilimia 50% tu basi kuanzia hapo ndipo Simba itaanza kuzungumzia ubingwa wa Afrika. Kwani katika mechi dhidi ya Kaizer Simba ilikosa mtu wa kuimaliza ile mechi mapema kipindi cha kwanza.

Kuhusu Kagere na Mugalu lazima Simba ivunje benki ili ipate pesa za kuachana na mmojwapo na Kocha ndio aamue nani aende kati ya hao wawili na mmoja abaki. Lakini Simba nao wajitahidi kumpa nafasi Miraji (ana kasi na jicho la goli) na kumrudisha Ilanfya (ana nguvu na anajua kufunga) ili baadae waje wamrithi Boko kwani umri wake umeenda sana sasa hivi anatakiwa awe anapata mapumziko badala ya kumtegemea msimu mzima.
 
Simba kwa kuwa wameijuliaa uwanja wao wa nyumbani bas katk mech zingine cjazo wahakikishe kuwa magoli ya away yaziwe Zaid ya mawili tu Zaid Sana moja tu ili ikija dsm uwanja wake ifanye mambo lait Kama Simba kaliwa mbili kule bondeni bas leo angepita kirahisi Sana Leo ingekuta Ni sherehe had yule aliyefiwa na bb ake angesherekea tu
Inawezekana na hao wageni nyumbani kwao wakajipanga kwa mbinu na mikakati kama ilivyo kwa Simba akiwa nyumbani kwake pindi wakikutana na timu ya Simba. Kaizer chief kwanzia huu mwaka uanze hakufahi jushinda goli nne hata mara moja hata kwenye ligi ya kwao huko kashindwa kaja kuipatia Simba unyonge wa kumbugiza goli nne
 
Kikosi kilichoanza unakikumbuka alicheza na kina nani? Unamuhukumu vipi mchezaji kwa gemu moja? Game ngapi mugalu ni mashuzi tu?

Yote 9, 10 ndio mfungaji wetu bora misimu miwili ama mi3 mfululizo.. Nyongeza kwa dk chache alizopewa nahisi ana wastani wa magoli mengi kuliko mugalu.
Mfungaji bora kwenye ligi ya ridhaaaa


Masihara haya
 
Kifupi coach hampemdi kagere tuseme..

Subs zilikiwa hazijaisha.. Ana matatizo mahali, ama tuseme alikiwa kavurugwa bemchi la ufundi lilipaswa limkumbushe, pamoja ma yoote kagere ndio mfungaji wetu tegemeo kwa misimu kadhaa, na msimu huu ni nafasi tu kanyimwa lakini mie naamini katika uwezo wake.
Naambiwa Sub zimeongezwa toka 3 mpaka 5 kwa masharti, sharti linatakiwa ukifanya Sub 5 uwe umezifanya ktk mikupuo mi 3!!Yaani uingize 1, 2, 2 jumla watano, au 1,1,2 jumla wanne.

Simba sub ya kwanza Mzamiru/Morisson, ya pili Lwanga/Nyoni, ya Tatu Onyango/Kennedy mikupuo mitatu ikaisha.

Kama Lwanga na Onyango wangetoka pamoja tungekuwa na mikupuo miwili ungebaki mkupuo mmoja tungeweza kuinhia mchezaji mmoja au wawili kwa Pamoja.

Naomba kuwasilisha
 
Naambiwa Sub zimeongezwa toka 3 mpaka 5 kwa masharti, sharti linatakiwa ukifanya Sub 5 uwe umezifanya ktk mikupuo mi 3!!Yaani uingize 1, 2, 2 jumla watano, au 1,1,2 jumla wanne.

Simba sub ya kwanza Mzamiru/Morisson, ya pili Lwanga/Nyoni, ya Tatu Onyango/Kennedy mikupuo mitatu ikaisha.

Kama Lwanga na Onyango wangetoka pamoja tungekuwa na mikupuo miwili ungebaki mkupuo mmoja tungeweza kuinhia mchezaji mmoja au wawili kwa Pamoja.

Naomba kuwasilisha
Hili silifahamu chief. Sijui kama ni kweli ama lah.
 
Nimetafakari kwa muda sababu ya msingi kwanini kocha hakumuingiza Kagere nikapata sababu mbili.

1. Nimehisi sub zinazotakiwa mwisho ni tatu, japo wapo wanaosema sababu ya Corona zinatakiwa sub mpaka wachezaji watano, kwasababu kama bado kocha alikuwa na nafasi ya kumuingiza Kagere baada ya Mugalu kuonekana amepwaya kule mbele, sioni kwanini hakufanya hivyo.

2. Sababu yangu ya pili inayoendana na ile ya kwanza ni kuumia kwa Lwanga, hii ilisababisha nafasi ya kumuingiza Kagere iwe imeshajazwa kwa aliechukua nafasi ya Lwanga (ambae ni Nyoni) hivyo kuondoa nafasi ya Kagere kuingia.

Kama hizi sababu zote mbili sio za kweli, maana yake kocha alikuwa na nafasi ya kumuingiza Kagere lakini hakufanya hivyo, kitendo chake cha kuonesha mahaba kwa mchezaji aliekosa ubunifu kule mbele kimechangia Simba SC kuondoshwa, hasa nikizingatia uwezo wa Kagere kwenye kuzifumania nyavu, kama ambavyo alikuwa mfungaji bora wa ligi yetu misimu miwili mfululizo.
Jana sub ziliisha kwa jinsi inavyotakiwa kufanya sub kwa wachezaji watano. Sub unatakiwa kufanya wachezaji watano lakini kwa awamu tatu. Simba ilifanya hivyo kulingana na kwamba zilikua sio sub za kiufundi zilikua za lazima
 
Hili silifahamu chief. Sijui kama ni kweli ama lah.
Ni sahihi nilitaka nilielezee yuko sahihi.pale walipogongana lwanga na onyango,Onyango alirudi kuendelea na mchezo halafu akatolewa akawa ameshaiua ile nafasi ya mwisho ya mabadiliko mipira ina vitu vingi ambavyo watu hawavielewi
 
Naambiwa Sub zimeongezwa toka 3 mpaka 5 kwa masharti, sharti linatakiwa ukifanya Sub 5 uwe umezifanya ktk mikupuo mi 3!!Yaani uingize 1, 2, 2 jumla watano, au 1,1,2 jumla wanne.

Simba sub ya kwanza Mzamiru/Morisson, ya pili Lwanga/Nyoni, ya Tatu Onyango/Kennedy mikupuo mitatu ikaisha.

Kama Lwanga na Onyango wangetoka pamoja tungekuwa na mikupuo miwili ungebaki mkupuo mmoja tungeweza kuinhia mchezaji mmoja au wawili kwa Pamoja.

Naomba kuwasilisha
Acha kupotosha wala haipo hivyo, jana Kaizer wamefanya sub kwa mikupuo mi4, dk. 46, 59, 60, 72 na 88. Gomez aliamua tu kutofanya sub kwasabab anazojua yeye.
 
Kifupi coach hampemdi kagere tuseme..

Subs zilikiwa hazijaisha.. Ana matatizo mahali, ama tuseme alikiwa kavurugwa bemchi la ufundi lilipaswa limkumbushe, pamoja ma yoote kagere ndio mfungaji wetu tegemeo kwa misimu kadhaa, na msimu huu ni nafasi tu kanyimwa lakini mie naamini katika uwezo wake.

Pitia kanuni, hakuwa na nafasi ya kufanya sub tena.
Double sub first half ilitu cost....
 
Simba bahati haikua yetu leo, hata angeanza MK14 mtu wa kazi. Ukiangalia magoli mengi wachezaji waliyokosa ni mengi sio Mugalu tu hata, Boko, Chama na Morison. Pia kuna mchezaji wa Kaizer alishika ndani ya box lakini refa kapotezea.

Simba ni timu bora sana ingawa imetolewa lakini kazi imefanyika ya kiwango cha kimataifa.

Simba nguvu moja.
Usiseme bahati sema uwezo uliishia pale.
 
Vyema ampe nafasi na Kagere kuliko kukomaa na Mugalu muda wote no matter what.
Mugalu ndio striker anayefanya vizuri sana mazoezini. Makocha wana taratibu zao za kuamua nani apangwe, na mipango huanza mazoezini
 
Ndio maana makocha wa timu hawakai. Sijui kwa nini mashabiki na wachambuzi wana upiga mwingi kwenye kazi za watu badala ya kuwaacha wenyewe wafanye maamuzi
 
Back
Top Bottom