Sababu ya Kuvunjika EAC-I, Kuundwa Upya EAC-II,"The Coalition of The Willing" Kujimwambafay na Jinsi JK Alivyoiokoa Jumuiya Isivunjike Kwa Kujishusha!

Sababu ya Kuvunjika EAC-I, Kuundwa Upya EAC-II,"The Coalition of The Willing" Kujimwambafay na Jinsi JK Alivyoiokoa Jumuiya Isivunjike Kwa Kujishusha!

Vipi kuhusu itikadi za kisiasa miongoni mwa nchi wanachama Tz (ujamaa), Kenya(Ubepari) je haikuwa sababu ya kuvunjika hii jumuiya ?
Mkuu Proved
Kuvunjika kwa jumuiya ya kwanza ya Afrika Mashariki, kulitokana na sababu nyingi ila sababu kubwa ya kwanza ni tofauti za kisiasa, kiitikadi na mifumo ya uchumi baina ya nchi wanachama. Tanzania tulifuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea wakati Kenya iliendelea na mfumo wa uchumi wa kibepari na soko huria ilio urithi kutoka katika uchumi wa kikoloni, Uganda ilitawaliwa kidikiteta na nduli Idi Amini Dada hivyo kutaifisha kila kitu kuwa mali ya umma.

Paskali
Kitakachoikwamisha hii jumuiya ya Sasa ni mzozo baina ya nchi wanachama hasa Rwanda na jirani zake Drc na Burundi, isitoshe imeonyesha udhaifu mkubwa kwa kushindwa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa huo mzozo.
Mizozo yote itakwisha tutakapo fikia stage ya political federation.
Mizozo ya kisiasa ndani ya nchi wanachama hasa nyakati za uchaguzi ni mtihani mgumu kwa hii jumuiya, hasa pale inapoonekana hakuna nchi inayoonekana imeweza kuepuka hili kwa kuheshimu mchakato wa kidemokrasia.
True political federation pia hili italifuta.
Mzozo wa ndani wa miaka mingi wa Drc huku nchi wanachama wa EAC wakitajwa kuwa wahusika wakubwa ni mtihani mwingine uliyokwisha kuishinda jumuiya.
Huu unakwisha naturally baada ya kuuingiza DRC kwenye EAC, hata Somalia itatulia.
Hili ni jumuiya ya kuwakutanisha viongozi na taasisi zao tu ila mengine .....
Itabadilika
P
 
Back
Top Bottom