Sababu ya Nyumba kuungua kwa tatizo la umeme na utatuzi wake

Sababu ya Nyumba kuungua kwa tatizo la umeme na utatuzi wake

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
SABABU YA NYUMBA KUUNGUA KWA TATIZO LA UMEME NA UTATUZI WAKE:

Napenda kuwakaribisha katika majadiliano ya tatizo hili ambalo limekuwa likisababisha majanga makubwa sana hapa kwetu Tanzania kutokana na hasa kuongezeka kwa matumizi ya umeme. Juu sheria ya umeme ya kimataifa IEE regulation.

Pia uchambuzi huu utazingatia British Standard of the IEE Wiring Regulations. Kwani mfumo yetu mingi ya umeme ya Kiafrika hata ule wa Tanzania ume-copy kutoka katika regulation hizi kubwa mbili duniani.

Na sababu ya kutumia IEE wiring regulation ambayo ni ya British standard 7671 ni kwa sababu inazungumzia sheria na kanuni za umeme wa kiwango cha 230V kwa single phase. Ambao ndiyo shirika la umeme Tanzania TANESCO linausambaza kwenye makazi ya watu.

1. MAKOSA YANAYO SABABISHWA NA MAFUNDI KWENYE KUFANYA WIRING
(a). Overload of power supply wire:

Hii husababishwa na line moja ya power supply kutoka katika main switch kutumika kusambaza umeme katika vyumba vingi.
Mfano nyumba nyingi mafundi hutumia 2.5 mm² wire kama supply ya kwenye vyumba,supply hii hutumika kama junction supply ya vyumba vingine.

Wire ya 2.5 mm² kitaalamu mwisho wake wa kupitisha current kiusalama ni 20Ampere ikitokea current zaidi ya ishirini ikalazimishwa kupita katika waya ya namna hii husababisha waya kupata moto,kama hali hii itakua kubwa sana waya uungua. Na huenda ukasababisha moto.

(b). Current ya Miniature Circuit Breaker(MCB) kuwa kubwa kuliko current ya wire
Mfano wire wa 2.5 mm² tumeona kuwa una uwezo wa kupitisha 20Ampere kiusalama Hivyo MCB yake inatakiwa iwe ya 20Ampere. Lakini mafundi wengine kwa kujua au kuto kujua hujikuta wanafunga MCB zenye current kubwa zaidi ya wire husika hali hii huweza kusababisha wire husika kuungua kwani MCB itashindwa kujizima hata pale wire itakapo kuwa imefikia kiwango chake cha mwisho cha kupitisha current. Matokeo yake wire husika unaweza kuungua na kusababisha moto.

Viwango sahihi vya MCB na size ya waya zake zinazo shauliwa kimataifa ni hizi hapa:
1.5 mm² cable - 15 amp miniture circuit breaker.
2.5 mm² cable - 20 amp miniture circuit breaker.
4 mm² cable - 25 amp miniture circuit breaker.
6 mm² cable - 32 amp miniture circuit breaker.
10 mm² cable - 40 amp miniture circuit breaker.

(c). Loose Connection
katika maungio ya waya na kwenye vifaa vinavyo funga waya kwa screw. Kama fundi hato kaza waya vizuri wakati wa kuziunga pamoja katika viungo vya screw au waya kwa waya ni chanzo kikubwa cha kutokea kwa cheche ambazo hatimaye huweza kuanzisha moto.

(d). Tabia ya mafundi umeme kukubali kuunga mfumo wa wiring wa nyumba nyingine dhidi ya nyumba nyingine
Kwa kawaida Tanesco huingiza umeme katika nyumba kutokana na plan pamoja na mahitaji ya kiwango cha umeme cha nyumba husika (Kilowatt Hour). Hili hujumuisha ukubwa wa size ya waya wa kuingiza umeme katika nyumba yako n.k.

Pia waya unao ingiza umeme kutoka katika meter kwenda ndani ya nyumba (tail wire) mara nyingi size yake hutegemea mahitaji ya nyumba husika. Hivyo nyumba inapo pewa umeme hua imejitosheleza kwa mahitaji yake binafsi kitaalamu.

Inapotokea nyumba nyingine ikaungwa katika mfumo huo wakati plan yake haikuhusishwa wakati wa kufunga umeme katika nyumba ya awali hali hii hupelekea OVERLOAD katika tail wire hali ambayo inaweza kupelekea wire hiyo kuungua na kusababisha moto.

2. MAKOSA YA SHIRIKA LA USAMBAZAJI UMEME
(a).
Kuto funga Vilinda circuit wakati wa kufunga meter za umeme
Shirika la usambazaji umeme ni lazima lihakikishe linaweka vifaa vya kulinda nyumba husika dhidi ya matatizo ya umeme.
katika METER ya umeme au ndani ya nyumba Ufungaji wa vifaa hivi ulikua unazingatiwa sana zamani (sababu licha ya kuwa kama fuse CUT-OUT zilitumika kukata umeme katika nyumba pale mteja akishindwa kulipa bill ya umeme). Sasa baada ya kuingia kwa meter za LUKU imeonekana kama CUT-OUT hazina maana tena hivyo suala lake la kutumika kama kifaa cha kulinda mfumo wa umeme kama fuse limepuuziwa.

Kuna baadhi ya nyumba zimefungwa CUT-OUT hadi sasa licha ya kuwa zinatumia LUKU, pia kuna wenye bahati ambao mita zao zina Circuit breaker. Ufungaji wa umeme usio zingatia vifaa hivi,unaongeza uwezekano mkubwa wa kutokea short ya umeme yenye madhara.

Kama umeingiziwa umeme katika nyumba yako halafu vifaa nilivyo vitaja hapo juu hujafungiwa hata kimoja (yaani umeme umetoka katika bracket na kuingia katika meter moja kwa moja bila kupitia katika (CUT-OUT au CIRCUIT BREAKER ) mfumo wako wa umeme si salama ni haki yako kufungiwa vitu hivyo una haki ya kudai kwa usalama wa nyumba yako.
(b). Miundo mbinu mibovu ya shirika la ugavi wa umeme.
Hali hii hupelekea kukatika katika hovyo kwa umeme,hali hii huweza kuzalisha Electrical Surges ambazo huweza kuleta madhara kwa watumiaji wa umeme.

3. KUCHAKAA KWA WIRING ,VIFAA BANDIA NA VIFAA VIBOVU
(a) Circuit breaker mbovu au feki. Kuna circuit breaker nyingine mbovu au bandia ambazo zinashindwa kujizima pale short ikitokea,hakikisha unaijaribu circuit breaker yako mara kwa mara kwa kubonyeza “trip test” kuona kama inafanya kazi au la.

(b) Switch za umeme na extension cables ambazo ni mbovu au hazijakidhi vigezo(bandia)ni chanzo kikubwa cha moto katika makazi yetu. Vifaa kama vile switch ambazo zimesha haribika vibadilishwe ili kuepuka kutokea kwa moto. Pia epuka kutumia Extension cables ambazo ni bandia.

(c) Wiring iliyo chakaa huweza kusababisha kutokea kwa moto kutokana na kulegea kwa viungo vyake ambavyo husababisha chehe, pia wire zake huwa zimeshambuliwa sana na wanyama na wadudu hivyo zinaweza zikagusana na kusababisha short yenye kupelekea moto kutokea.

4. KUFANYA MATENGENEZO YA VIFAA VYA UMEME NA KUVITUMIA BILA KUWA NA UTAALAMU
Watu wengi wamekuwa wakifanya matengenezo ya vifaa vya umeme angali hawana utaalamu wa umeme.Vifaa vyote vya umeme ni lazima vikatengenezwa na mtu ambaye amesomea kazi hiyo. Mfano watu wengi hubadilisha fuse katika mifumo mbalimbali ya vifaa vya umeme pale zinapo ungua.Ubadilishaji wa fuse hizi mara nyingi hufanyika kiholela bila kuzingatia kiwango cha current cha fuse husika. Hali hii husababisha fuse husika kuto kukatika wakati short ikitokea hivyo huweza kupelekea waya kuuungua napengine kusababisha short ya umeme.

5. KUJAZA VIFAA VINAVYO TUMIA UMEME KATIKA EXTENSION CABLE KUZIDI UWEZO WAKE
Extension cable zimetengenezwa kwa uwezo tofauti tofauti.Hakikisha hauzidishi vifaa vya umeme vinavyo chukua umeme kupitia extension cable yako ili kuepuka uwezekano wa extension cable hiyo kuungua.

SOLUTION
1. 1. Makosa haya makubwa matano yanaweza yakaepukika kwa kila mmoja kufata utaratibu na kanuni za ndani ya nchi na za kimataifa zinazo simamia matumizi bora ya umeme.

2. 2. Walaji wa umeme wawe na utaratibu wa kukagua mifumo yao ya umeme mara kwa mara Kupitia wataalamu wa umeme ili kuthibitisha usalama wa mfumo wake wa umeme katika nyumba yake. Utaratibu huu wa ukaguzi ni muhimu ambapo mtaalamu atakagua kama wiring system yako imekidhi vigezo; ambapo mtaalamu wa umeme hutakiwa kuchukua vipimo maalumu na kuangalia kama mfumo wako wa umeme umekidhi kanuni na taratibu zinazo simamia mifumo ya umeme.

Baada ya vipimo mtaalamu huyo hutakiwa kuandaa ripoti yenye taarifa ya ukaguzi na kutoa matokeo ya ukaguzi huo wa mfumo wa umeme katika nyumba yako.

Mkaguzi atatoa majibu makuu matatu kulingana na sheria na kanuni za mifumo ya umeme majumbani kuwa mfumo wako wa umeme ni (Salama,Salama kidogo unahitaji marekebisho au si salama).Report hiyo ataisaini na kukukabidhi.

1. 3. Ufungaji wa vifaa vinavyo tambua ishara ya kutokea kwa moto (fire sensor)
1. 4. Kuepuka kufanya matendo ambayo yatapelekea kutokea kwa tatizo la umeme ambalo linaweza kusababisha moto.
1. 5. Kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika majumba yetu.

Not always electrical fault will give you a chance to correct your mistake. BE CAREFULLY!
 
Hiyo namba 1B ni tatizo kubwa sana sana. likitatuliwa litapunguza sana hii shida.

Mimi ni fundi umeme na pia nimebahatika kujenga nyumba yangu, nimefanya wiring moja ya kisomi sana.

Shida inaanzia kwamba mtu akinunua DB anataka atumie zile miniature ambazo zipo mle ndani hataki kununua mpya ambqzo zitaendana na sizing zake.

Mfano mtu anatumia miniature CB ya 6A wakati huo huo ana taa 15 za watts 9 ambazo ni sawa na na 0.6A.

sasa unajiuliza Circuit ya 1 Amp inalindwaje na MCB ya 6A [emoji847] unakuja kuoana ni upuuzi tuu. ndio maana short inatokea na MCB inaona ni load ya kawaida tuu

Mimi kwenye DB yangu utashangaa sana

Lighting circuit 1 - 2A Mcb
Lighting circuit 2 - 2A Mcb
Power socket Sebuleni 3A Mcb
Power socket Vyumbani 10A Sababu ya heater
Jikoni 25A
Water heater 16A

Very simple and calculated design

Sasa mafundi huko mtaani wanazishona MCB za 32A utafikiri ni kiwandani [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sasa unajiuliza hivi MCB ya 32 itatripi lini?? [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Hiyo namba 1B ni tatizo kubwa sana sana. likitatuliwa litapunguza sana hii shida.

Mimi ni fundi umeme na pia nimebahatika kujenga nyumba yangu, nimefanya wiring moja ya kisomi sana...
Ndo hivyo mkuu matatizo hayo yanafanya kuwepo kwa ajali nyingi zitokanazo na Umeme
 
Hiyo namba 1B ni tatizo kubwa sana sana. likitatuliwa litapunguza sana hii shida.

Mimi ni fundi umeme na pia nimebahatika kujenga nyumba yangu, nimefanya wiring moja ya kisomi sana....
Mkuu unaweza nifanyia wiring kama yako huku kwangu Mbezi, bei yoyote utakayotaja nitakulipa, tuwasiliane DM tafadhali.
 
Asante ndugu mleta mada tumejifunza kitu chenye ubora kwa kiasi kikubwa , Muhimu Ni kuzingatia tu.
 
Tumuombe tu Mungu atunusuru,maana haya makosa kuyakwepa ni ngumu sana,ingawa yapo yanayoepukika...
 
Kosa la kutoweka cut out kwa Tanesco limekua sugu, juzi kati nimeenda kutatua fault mahali na tatizo lilikua la tail wire ilikua imechubuka inagusana na body ya Main switch hapo ilibidi kuwa makini zaidi maana mita ipo juu ya nguzo.
 
Ndo hivyo mkuu matatizo hayo yanafanya kuwepo kwa ajali nyingi zitokanazo na Umeme
kwa hili jibu 'rahisi' hapa ni wazi kwamba huna ufaham na maswala ya umeme

no offense

ilo bandiko ume-kopi uka pesti , basi weka hata credits kwa chini pale
 
kwa hili jibu 'rahisi' hapa ni wazi kwamba huna ufaham na maswala ya umeme

no offense

ilo bandiko ume-kopi uka pesti , basi weka hata credits kwa chini pale
😠😠😠
Sawa mkuu ndo hivyo tu.
 
Kosa la kutoweka cut out kwa Tanesco limekua sugu, juzi kati nimeenda kutatua fault mahali na tatizo lilikua la tail wire ilikua imechubuka inagusana na body ya Main switch hapo ilibidi kuwa makini zaidi maana mita ipo juu ya nguzo.
Japo juzi TANESCO walipewa zawadi kwa kupunguza ajari lakini naona bado sana.
Inatakiwa elimu itolewe kwa mafundi pamoja na watu wengine.
 
Mpangaji unampangisha nyumba umeijenga kwa gharama, alafu analeta haya matatizo. Wengi wetu hatuna BIMA za nyumba.
 
Back
Top Bottom