Sababu ya Simba kutoanzia kwenye hatua ya awali kwenye michuano ya Klabu bingwa Afrika ni hii

Sababu ya Simba kutoanzia kwenye hatua ya awali kwenye michuano ya Klabu bingwa Afrika ni hii

changaule

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2020
Posts
6,039
Reaction score
10,151
Naona kuna watu wasioelewa kwanini Simba ipo kwenye timu 10 ambazo hazitoanzia hatua ya awali. Wengi wao wanasema kwavile Simba ipo kwenye kumi bora Africa ndio maana wamepata hiyo nafasi. Usahihi ni kwamba Simba wamepata nafasi kwavile timu zingine zenye nafasi zao zimeshindwa kifuzu kuingia michuano ya klabu bingwa mfano Kaizer Chiefs ila kwa upande wa rank ni kwamba Simba ni ya 16

Hii hapa rank za timu pamoja na points walizokusanya kwenye michuano ya kimataifa.View attachment leedrtkrzqgo4jawwrxr.pdf
 
Naona kuna watu wasiolewa kwanini Simba ipo kwenye timu 10 ambazo hazitoanzia hatua ya awali. Wengi wao wanasema kwavile Simba ipo kwenye kumi bora Africa ndio maana wamepata hiyo nafasi. Usahihi ni kwamba Simba wamepata nafasi kwavile timu zingine zenye nafasi zao zimeshindwa kifuzu kuingia michuano ya klabu bingwa mfano Kaizer chiefs ila kwa upande wa rank ni kwamba Simba ni ya 16

Hii hapa rank za timu pamoja na points walizokunya kwenye michuano ya kimataifa.View attachment 1893675
Ungesema tu kuwa Yanga ni ya 7 kutoka mwisho ungeeleweka zaidi...
 
Ungesema tu kuwa Yanga ni ya 7 kutoka mwisho ungeeleweka zaidi...
Mada ilikuwa ni kuweka sawa mawazo ya watu maana wengi walikuwa wanajiuliza na kisha kuzusha majibu ya vichwani mwao kuwa Simba imeshika nafasi ya 10 wakati ipo nafasi ya 16. Kuhusu Yanga ina hali mbaya kati ya timu zote zilizowahi kushiriki michuano ya kimataifa yeye wa 7 toka chini.
 
Hapana maelezo yako hayajashiba,swali linarudi palepale kwanini Simba,vigezo gani vilitumika Simba kupewa hiyo nafasi na isiwe timu nyingine zilizofufu kucheza CAFCL?
Lile pira biriani alilolisakata Simba linatosha kabisa kuwa kigezo cha Simba kupewa nafasi kwakuwa liliwapendeza viongozi wa wote wa CAF.
Kwa miaka mitatu Simba imefika katika hatua ya Robo fainali ya Club Bingwa Africa na msimu wa mwisho kuongoza ktkt kundi lake lililosheheni timu ngumu.
Kumbuka Robo Fainali ya Club Bingwa inatoa timu Nane tu ambazo ni bora hapa Afrika.
 
Hapana maelezo yako hayajashiba,swali linarudi palepale kwanini Simba,vigezo gani vilitumika Simba kupewa hiyo nafasi na isiwe timu nyingine zilizofufu kucheza CAFCL?
Kwasababu timu zilizo nafasi ya juu ya Simba ambayo ni Kaizer chiefs, Js Kabyile, As vital, pyramids, Berkane, Enyimba hazikufuzu kwenye ligi zao kucheza champions league msimu huu.
Simba ni ya 16 katika rank. Timu zilizopo kwenye rank ni9 tu ndio zimefanikiwa kufuzu kwenye nchi zao kucheza champions league lakini timu sita nilizozitaja hapo juu hazikuweza kufuzu kwenye ligi zao hivyo nafasi imepewa Simba ambaye anashika nafasi ya 16
 
Mbumbumbu fc kila wanapotaka kudanganya umma, umma unakua na taarifa za kutosha. Mbumbumbu wanajisikia vibaya.
 
Hii swala iliwapiga bumbuwazi watu wengi sana. Kuna jamaa ana page yake kabisa IG ni mshabiki wa Yanga katoa post kuwa CAF inapendelea inakuaje Simba apewe nafasi ya kuanzia hatua ya pili wakati kaizer chiefs waliofika hadi fainali wasipewe hiyo nafasi nikabaki kumshangaa, yaani kweli mtu huyu anafuatilia mpira kweli ama. Na wachumbuzi nao na wengineo wakatupeleka chaka kuwa Simba ipo kwenye kumi bora ya CAF kumbe rank ya CAF haipo hivyo.
 
Kwasababu timu zilizo nafasi ya juu ya Simba ambayo ni Kaizer chiefs, Js Kabyile, As vital, pyramids, Berkane, Enyimba hazikufuzu kwenye ligi zao kucheza champions league msimu huu.
Simba ni ya 16 katika rank. Timu zilizopo kwenye rank ni9 tu ndio zimefanikiwa kufuzu kwenye nchi zao kucheza champions league lakini timu sita nilizozitaja hapo juu hazikuweza kufuzu kwenye ligi zao hivyo nafasi imepewa Simba ambaye anashika nafasi ya 16
Hapa sasa umedadavua vizuri sana,Utopolo wasio elewa sasa wameelewa kuwa Simba ipo juu kwa sasa.
 
Naona kuna watu wasioelewa kwanini Simba ipo kwenye timu 10 ambazo hazitoanzia hatua ya awali. Wengi wao wanasema kwavile Simba ipo kwenye kumi bora Africa ndio maana wamepata hiyo nafasi. Usahihi ni kwamba Simba wamepata nafasi kwavile timu zingine zenye nafasi zao zimeshindwa kifuzu kuingia michuano ya klabu bingwa mfano Kaizer Chiefs ila kwa upande wa rank ni kwamba Simba ni ya 16

Hii hapa rank za timu pamoja na points walizokusanya kwenye michuano ya kimataifa.View attachment 1893675
Mtateseka saana na bado!
 
Back
Top Bottom