Kwa mtizamo wangu, Zanzibar Chadema kutokuenea siyo kuwa kuna ajenda fiche wala udini ni swala la kihistoria tu. Kabla ya uhuru ni vyama viwili ndivyo vilikua na nguvu sana visiwani ASP na ZPP hivyo kupelekea vyama hivyo kutawala siasa za Zanzibar. Baada ya kuja mfumo wa vyama vingi wazanzibari wengi walijiunga na CUF, siasa za vyama vingi ikawa ni CCM na CUF zinachuana karibuni nusu kwa nusu, pamoja na uwepo wa vyama vingine lakini vyama hivyo havikua na nguvu. Baada ya mvurugano wa chama cha CUF wafuaasi wake karibuni wote wakahamia ACT.
Baada ya Maalim Seif kuhamia ACT kilichotokea ni kukifanya hata CUF yenyewe kuwa chama cha kawaida sana Zanzibar, je hapo unaweza kusema CUF kiliponzwa na ajenda iliyojificha au udini? jibu ni hapana. Siasa za Zanzibar ni kama marekani Republican dhidi ya Democrats. Hayo ndiyo maoni yangu kwa ufupi kuhusu Chadema kutokuenea Zanzibar. Si kuna vyama vilivyo anzishwa na wazanzibari wenyewe lakini havina nguvu mfano kina Jahazi Asilia, ADC nk.