Kulupango
JF-Expert Member
- Mar 19, 2020
- 288
- 545
Kundi fulani kukataliwa kwa kisiasa, kama vile utiaji mgongo kwa makusudi ikiwemo ukosefu wa haki za kisiasa, kunatoa motisha nyingine inayofaa ya kuamua kufanya vurugu. Machafuko mengi hutokea kama vikundi (lakini huwa ni vikundi vya kisiasa ambavyo vinataka uhuru wa utawala kwenye serekali. Mfano ni Vita vya Indochina (1946-75) na Vita vya Uhuru vya Algeria (1954-62).
Mara nyingi serekali yenye nguvu ikitishiwa utawala wake kuanguka basi hutumia nguvu ya dola ili kuwezesha kushinda kwa kupitia kampeni za dhuluma. Sasa inapofikia hatua hii, kundi moja kunyanyaswa na lingine likiachiwa huru, basi yale makundi ya kisiasa yaliyodhulumiwa huwa yanatumia nguvu na yenyewe ili kusimika utawala wao ndani ya majimbo yaliyo chini ya himaya yao, ni kama vile serekali ndani ya serekali.
Kitendo hicho cha kikundi cha kisiasa kilichodhulumiwa kuamua kudhibiti jimbo hupelekea dola kukiangamiza kikundi hicho, sasa mbaya zaidi unakuta kikundi kinapata nguvu kutoka nchi washirika, husaidiwa silaha na mambo mengine kupitia kiongozi wao wa kisiasa na hapo ndio vita huanza rasmi.
Kikundi hichi hupatiwa majina mengi mabaya ikiwemo kikundi cha kigaidi au waasi, na endapo kitapata nguvu ya umma basi kikundi hichi huweza kuendelea kuteka majimbo mbalimbali na kuiangusha serekali, na endapo kisipofanikiwa kuiangusha serekali, basi kitaendelea kufanya mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya shughuli za serekali, na hapo ndipo nchi inakuwa haina amani tena.
Kwanini tunadhibiti maandamano?
Ni kwasababu maandamano yenye shinikizo la kisiasa katika serikali zisizo na kidemokrasia hutoa muktadha mwingine ambao vurugu zinaweza kutokea. Kwa kawaida serikali ambazo hazina demokrasia hukataa nafasi ya raia kufanya shughuli za maandamano ya kisiasa, na mara nyingi serekali hutumia nguvu kuyadhibiti hayo maandamano, ambayo kwa upande mwingine yanaweza kuhamasisha vurugu na kugeuka kuwa kundi la uhalifu au kundi la uasi.
Maandamano dhidi ya serikali dhalimu, hubadilika kuwa vurugu na wakati mwingine husababisha migogoro endelevu, ambayo kuitatua ni gharama kubwa sana.
Kwa wale raia wema ambao hawana uwezo wa kupigana au hawana silaha za kujilinda itawalazimu kukimbia miji yao kwa kuogopa kifo, na hali ikiwa mbaya zaidi hukimbia nchi yao na kwenda uhamisho kama wakimbizi.