Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
"Sitisha mkutano wako na usifanye shughuli hiyo Hadi tamko la mlipuko wa Ugonjwa wa kuhara litakapotenguliwa" ilisema sehemu ya barua hiyo kutoka kwa OCD Arusha.
Mchungaji Ezekiel Mkazi wa Mombasa Nchini Kenya wiki hii alikuwa afanye mkutano mkubwa wa Injili katika viwanja vya shule ya Msingi Ngarenaro na aliahidi pia kusaidia ukarabati wa shule hiyo .
Akiongea mara baada ya kupokea amri hiyo, alisema kuwa hana kinyongo na zuio Hilo wala serikali ya Tanzania na anashukuru kupewa heshima kwa kuandikiwa barua hiyo juu ya kualifiwa uwepo wa Ugonjwa huo.
"Ninawaomba Radhi wale wote waliofika na kulala kwenye uwanja wa MKUTANO inaumiza moyo wangu sana hasa nikikumbuka yule mama aliyelia pale uwanjani, kumbuka watu walitoka maeneo ya mbali sana naamini itakuja siku nzuri zaidi"
Mch.Ezekiel aliwahi kuwa na msuguano na SERIKALI ya Kenya akihusishwa na mauaji ya halaiki, ya waumini wasio na hatia zaidi ya 300 yaliyofanywa na mchungaji mwenzake Paul Makenzie.