Na mimi naomba mheshimiwa, kuongeza yafuatayo:
1. Kama Upinzani unavyokosa umoja nje ya serikali hivi sasa ukiingia serikalini utakuwa pia hauna umoja kama vile tunavyoona huko Kenya na Zimbabwe;
2. Hawa ni watu wenye njaa kali na hivyo tutegemee ufisadi mkubwa zaidi kuliko uliwahi kutokea huko nyuma;
3. Baadhi ya viongozi wa upinzani wanaonesha picha za ngono kwenye migahawa au klabu zao na hivyo kuonesha ni wapi watakapowapeleka wasichana na wavulana wetu wakishika madaraka;
4. Karibu kila kiongozi wa upinzani ananunulika kwa bei fulani, hili linaonesha pia wakiwa viongozi wa umma bado wataendelea kununuliwa na hasa wale wenye pesa ndani na nje ya nchi;
5. Karibu viongozi wote wa upinzani hawajui kusoma, kutafakari na kuandika taarifa na hoja mbalimbali za msingi, kwa hiyo wakija madarakani tutakuwa na uongozi wa wajinga;
6. Viongozi wa upinzani isipokuwa kwa Ndesamburo kule Moshi, Kilimanjaro hakuna aliyewahi kuanzisha mradi binafsi au wa kikundi wa maana hapa nchini kwa hiyo wakiingia madarakani wachache sana watakuwa na akili ya ujasiriamali, uwekezaji na uendelezaji watu kutokana na rasilimali walizonazo;
7. Kama walivyo viongozi waliopo madarakani viongozi wa upinzani wanoona pia bughudha au usumbufu kukutana na watu wa hali ya chini na masikini kwa ujumla ili kusikiliza matatizo yao na hivyo hawajui shida na matamanio na matarajio ya wale wanaotaka kuwaongoza kama walivyo wenzao leo kwa hiyo hapa hapatakuwa na mabadiliko yoyote. Utatoka uongozi unaojali maslahi yake yenyewe kwanza, ukaingia uongozi ambao pia unajali maslahi yake kwanza na siyo yale ya wale waliowatuma;
8. Hakuna mwanasiasa wa upinzani hata mmoja, ukimuondoa Maalim Seif, ambaye anakubali kukaa kijijini kwao kwa mwezi mmoja au zaidi, wote wako mjini kwa hiyo wakija madarakani nao pia wataendeleza miji na sio vijiji;
9. Hakuna Chama Chochote cha Upinzani kilichokubali kufanya makao yake makuu kuwa Ddoma kikiwemo hicho kipya cha CCJ. Kwa hiyo kama yalivyo mambo mengi mengine vyama hivi ni vya wajanja wachache wa mjini Dar es salaam kutaka kuila nchi toka jiji la maraha;
10. Hakuna chama chochote isipokuwa CHADEMA kilichozungumzia kuipa mikoa haki na uhuru wa kujitawala yenyewe kiuchumi na kijamii kwa maendeleo ya haraka ya mikoa husika. Hii ina maana serikali ya upinzani nayo itataka na itakubali ukiritimba wa kuitawala nchi hata kama haipelekwi mbele kutokea Dar es Salaam.
Nimezungumza, wengine nao wazungumze- Mwalimu Jr.