Sababu za Kutoshuka kwa Bei ya Mafuta Bongo!

Sababu za Kutoshuka kwa Bei ya Mafuta Bongo!

Usedcountrynewpipo

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,636
Reaction score
2,728
Kwa wale wanaoota kuwa bei ya mafuta itashuka Bongo kwa vile bei kwenye soko la mafuta la dunia imeshuka kwa zaidi ya asilimia hamsini, they are 'day dreaming'! Sababu zifuatazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kutoshuka kwa bei hizo ni kama ifuatavyo:
1). WAFANYA BIASHARA
Wafanya biashara wengi wako profit driven. Hutumia kila loophole ya kuongeza faida zao. So inapotokea iyo loophole usidhani kama wataiachia. Iwapo Mamlaka ya udhibiti haiwakoseshi usingizi, usitegemee wakashusha bei.

2). SERIKALI
Serikali nayo huwa inachaji ushuru fixed (ad volerium tax) kwenye bidhaa nyingi za kimiminika kama vile mafuta. Kwa Bongo nadhani kila lita ya mafuta inachajiwa kwa kadri ya sh mia saba. Iwapo serikali haitashusha ushuru wake kwa bidhaa ya mafuta, kushuka kwa bei ya mafuta itakuwa ni ndoto za mchana.

3). RUNNING COST
Japo bei ya mafuta imeshuka, sidhani kama bei ya kusafirishia mafuta hadi kwa mlaji imepungua. Sidhani pia kama mishahara ya wafanyakazi wa makampuni ya mafuta yanayofanya distribution hapa nchini kama imepungua. So iwapo gharama za uendeshaji wa biashara ya mafuta kama mishahara, rent n.k haijapungua, kushuka kwa bie ya mafuta pia itakuwa ni ndoto.

kifupi bei ya mafuta iko hivi
Fuel Price = Fixed cost (60%) + Variable Cost (40%).
Iwapo kilichopungua ni variable cost let say kwa lita ni sh elfu mbili. Fixed cost in Tsh 1,200 na Variable cost ni Tsh 800, Hata bei ikashuka kwenye soko by 50%, ina maana kitakachopungua ni Variable Cost. Sasa Tuna Tsh 800 tayari kwenye equation yetu, so tutegemee bei itapungua kutoka kwenye Tsh 800 hadi Tsh 400 za variable cost na kufanya bei mpya ya mafuta iwe walau Tsh 1600, iwapo itapungua kwa asilimia hamsini, na sio kutoka Tsh 2000 hadi Tsh 1000 (kushuka kwa asilimia hamsini) kama wananchi wengi wanavyotegemea.

Kwa uchambuzi huu, naomba tu wananchi wasitegemee makubwa linapokuja swala la unafuu wa bei ya mafuta!
 
Uchambuzi wako ni fake. Punguzo lolote kwenye aidha fixed au variable cost lazima lipunguze bei ya kuuza (selling price). Kinachoendelea bongo ni uhuni.
 
naomba kuuliza swali la kizushi, kwa kuwa gharama za maisha ziliongezeka kutokana na kuongezeka bei ya mafuta katika soko la dunia na kwasasa bei ya mafuta imeshuka. Je ikiwa gharama za maisha zitashuka, wafanyakazi watakuwa tayari kwa mishahara yao kupunguzwa?
 
Back
Top Bottom