Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa Bunge Maalum jana na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,kupitia kwa aliyekuwa Mwenyekiti wake Jaji Joseph S Warioba, inapendekeza kuwe na mfumo wa Serikali tatu. Serikali hizo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Seikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Zanzibar. Wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikipendekezwa kuongozwa na Rais, serikali za Tanzania Bara na Zanzibar zinasubiri kuandikwa kwa Katiba zao ili Katiba husika ziseme aina,muundo na idadi ya uongozi.
Tume ya Jaji Warioba ilipokea maoni ya watanzania juu ya suala hili la muundo wa muungano. Na jana, Jaji Warioba ametoa takwimu na kuzirejea nyaraka mbalimbali zilizopendekeza muundo wa Serikali tatu. Watanzania wengi sasa wameelewa mantiki ya Tume ya Jaji Warioba kuhusu kwanini imependekeza mfumo wa Muungano wa Serikali tatu.
Ingawa yaweza kuwa imeshaelezwa na Jaji Warioba na wengine, naziona zifuatazo kuwa ni sababu za kuwa na Serikali tatu kwa Tanzania hii tuliyonayo:
Kwanza, Serikali tatu ni mapendekezo na matakwa ya watanzania wenyewe. Rejea hotuba ya Jaji Warioba kuhusu waliotoa maoni juu ya muundo wa muungano na asilimia zilizopendekeza Serikali tatu.Hivyobasi, si vyema kuyabeza maoni ya watanzania ambao mwisho mwishoni wataipigia kura Rasimu hii iliyosheheni maoni yao. Serikali tatu muhimu.
Pili, Serikali tatu zitaongeza ufanisi.Kila kiongozi wa Serikali zitakazokuwepo atajitahidi kuwahudumia wanamhusu katika masuala ambayo yeye ana mamlaka nayo. Aina hii ya ushindani itaibua ufanisi na umakini katika utendaji wa kazi na kuipeleka Tanzania mbele kimaendeleo.
Tatu, Serikali tatu zitatibu maumivu ya muda mrefu ya watanzania bara na ya wazanzibari. Kimekuwa kitu cha kawaida kwa wazanzibari na watanzania bara kia mmoja kwa wakati wake na nafasi yake kutaka uhuru wa kufanya mambo fulani fulani. Kwa Tanzania Bara,kuliwahi kuibuka kundi la G55 Bungeni Dodoma lililowajumuisha Wabunge mbalimbali kama Jenerali Ulimwengu na Njelu Kasaka ambao 'waliidai' Tanganyika (Tanzania Bara).
Na Zanzibar kila kukicha imekuwa 'ikilia na kuomba' kuruhusiwa kushiriki katika mahusiano fulanifulani na mashirikisho,taasisi,nchi na jumuiya bila ya mahusiano hayo kuingiliwa na kudhibitiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muda ndiyo huu kuweka Serikali tatu zenye mamlaka yanayoainishwa waziwazi ili malalamiko na maombi hayo yapate majibu sasa.
Nne, imekuwa sera na hoja ya Serikali ya CCM kuwa kugawa nchi katika mikoa,wilaya,tarafa,kata na kadhalika kwa wingi ni kusogeza huduma kwa wananchi na kuongeza ufanisi.Ndiyo maana mikoa ya Tanzania imeongezeka kutoka 25 hadi kufikia 30.Mikoa iliyoongezwa katika miaka ya karibuni ni Manyara,Geita,Simiyu,Njombe na Katavi.Pia zipo Wilaya nyingi tu. Hoja hii iendelezwe kwa kuweka mamlaka ya Tanzania Bara kwa watanzania bara wenyewe na mamlaka ya Zanzibar kwa wazanzibari wenyewe.
Tano, Serikali tatu zitapunguza matumizi ya Serikali. Kila Serikali itatengewa rasilimali zake ili ipate kujiendesha. Matumizi yake hayatazidi hapo.Italazimika kuweka idadi makini ya viongozi wake;kuweka taratibu safi za matumizi ya mapato yake;kusimamia kikamilifu ilichonacho.Hoja ya kwamba matumizi yatakuwa makubwa haina msingi hapa. Serikali tatu zaweza kuwa na viongozi wachache kuliko waliopo sasa katika Serikali mbili!
Itoshe kusema kuwa, sasa ni dhahiri shahiri kuwa Serikali tatu haziepukiki. Ni busara sasa kuendelea mbele tukianzia hapo...
cc Le Mutuz Buchanan Chris Lukosi Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3 Yericko Nyerere, Elli Crashwise Mungi Mingoi Mtela Mwampamba Juliana Shonza Zitto Tumaini Makene Mchange john Ben Saanane MsandoAlberto UJANJAUJANJA na wengineo kwa mjadala wa kujenga

Last edited by a moderator: