Sababu za kuwa na Serikali Tatu

Sababu za kuwa na Serikali Tatu

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa Bunge Maalum jana na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,kupitia kwa aliyekuwa Mwenyekiti wake Jaji Joseph S Warioba, inapendekeza kuwe na mfumo wa Serikali tatu. Serikali hizo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Seikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Zanzibar. Wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikipendekezwa kuongozwa na Rais, serikali za Tanzania Bara na Zanzibar zinasubiri kuandikwa kwa Katiba zao ili Katiba husika ziseme aina,muundo na idadi ya uongozi.

Tume ya Jaji Warioba ilipokea maoni ya watanzania juu ya suala hili la muundo wa muungano. Na jana, Jaji Warioba ametoa takwimu na kuzirejea nyaraka mbalimbali zilizopendekeza muundo wa Serikali tatu. Watanzania wengi sasa wameelewa mantiki ya Tume ya Jaji Warioba kuhusu kwanini imependekeza mfumo wa Muungano wa Serikali tatu.

Ingawa yaweza kuwa imeshaelezwa na Jaji Warioba na wengine, naziona zifuatazo kuwa ni sababu za kuwa na Serikali tatu kwa Tanzania hii tuliyonayo:

Kwanza, Serikali tatu ni mapendekezo na matakwa ya watanzania wenyewe. Rejea hotuba ya Jaji Warioba kuhusu waliotoa maoni juu ya muundo wa muungano na asilimia zilizopendekeza Serikali tatu.Hivyobasi, si vyema kuyabeza maoni ya watanzania ambao mwisho mwishoni wataipigia kura Rasimu hii iliyosheheni maoni yao. Serikali tatu muhimu.

Pili, Serikali tatu zitaongeza ufanisi.Kila kiongozi wa Serikali zitakazokuwepo atajitahidi kuwahudumia wanamhusu katika masuala ambayo yeye ana mamlaka nayo. Aina hii ya ushindani itaibua ufanisi na umakini katika utendaji wa kazi na kuipeleka Tanzania mbele kimaendeleo.

Tatu, Serikali tatu zitatibu maumivu ya muda mrefu ya watanzania bara na ya wazanzibari. Kimekuwa kitu cha kawaida kwa wazanzibari na watanzania bara kia mmoja kwa wakati wake na nafasi yake kutaka uhuru wa kufanya mambo fulani fulani. Kwa Tanzania Bara,kuliwahi kuibuka kundi la G55 Bungeni Dodoma lililowajumuisha Wabunge mbalimbali kama Jenerali Ulimwengu na Njelu Kasaka ambao 'waliidai' Tanganyika (Tanzania Bara).

Na Zanzibar kila kukicha imekuwa 'ikilia na kuomba' kuruhusiwa kushiriki katika mahusiano fulanifulani na mashirikisho,taasisi,nchi na jumuiya bila ya mahusiano hayo kuingiliwa na kudhibitiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muda ndiyo huu kuweka Serikali tatu zenye mamlaka yanayoainishwa waziwazi ili malalamiko na maombi hayo yapate majibu sasa.

Nne, imekuwa sera na hoja ya Serikali ya CCM kuwa kugawa nchi katika mikoa,wilaya,tarafa,kata na kadhalika kwa wingi ni kusogeza huduma kwa wananchi na kuongeza ufanisi.Ndiyo maana mikoa ya Tanzania imeongezeka kutoka 25 hadi kufikia 30.Mikoa iliyoongezwa katika miaka ya karibuni ni Manyara,Geita,Simiyu,Njombe na Katavi.Pia zipo Wilaya nyingi tu. Hoja hii iendelezwe kwa kuweka mamlaka ya Tanzania Bara kwa watanzania bara wenyewe na mamlaka ya Zanzibar kwa wazanzibari wenyewe.

Tano, Serikali tatu zitapunguza matumizi ya Serikali. Kila Serikali itatengewa rasilimali zake ili ipate kujiendesha. Matumizi yake hayatazidi hapo.Italazimika kuweka idadi makini ya viongozi wake;kuweka taratibu safi za matumizi ya mapato yake;kusimamia kikamilifu ilichonacho.Hoja ya kwamba matumizi yatakuwa makubwa haina msingi hapa. Serikali tatu zaweza kuwa na viongozi wachache kuliko waliopo sasa katika Serikali mbili!

Itoshe kusema kuwa, sasa ni dhahiri shahiri kuwa Serikali tatu haziepukiki. Ni busara sasa kuendelea mbele tukianzia hapo...

cc Le Mutuz Buchanan Chris Lukosi Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3 Yericko Nyerere, Elli Crashwise Mungi Mingoi Mtela Mwampamba Juliana Shonza Zitto Tumaini Makene Mchange john Ben Saanane MsandoAlberto UJANJAUJANJA na wengineo kwa mjadala wa kujenga
 
Last edited by a moderator:
sikiliza wewe ndugu yangu, UFUMBUZI HAPA NI SERIKALI MOJA AU KUVUNJA MUUNGANO, KWA SABABU KAMA ULIMSIKILIZA VIZURI JAJI WARIOBA WAKATI ANAONGEA JANA ALISEMA WANANCHI WENGI KWA UPANDE WA ZANZIBAR (63% kama sijakosea) WANATAKA MUUNGANO WA MKATABA, KWA SISI WENYE AKILI TUMEELEWA KUWA WAZANZIBARI HAWAUTAKI TENA MUUNGANO, KWANZA KAMA UNAKUMBUKA VIZURI, BAADA YA MAPINDUZI YA ZANZIBARI NA KARUME KUWA RAISI WA ZANZIBARI HALI YA NCHI KIUSALAMA ILIKUWA MASHAKANI SANA KWA HIYO SABABU HASA YA KARUME KUJIUNGA NA TANGANYIKA ILIKUWA NI KWA SABABU YA KUTAKA KUJIIMALISHA KIMADARAKA HARAFU BAADAYE AKIISHA IMARISHA VYOMBO VYAKE VYA KIUSALAMA AJITOE, LAKINI IKASHINDIKANA. SASA UTAONA KUWA WANAJIHISI KAMA WANALAZIMISHWA. UKWELI NI KWAMBA MUUNGANO HUU UNALAZIMISHWA NA SISI WATANGANYIKA.
 
Mkuu, sehemu gani ya rasimu ya katiba ya jamhuri ya muungano imependekeza kutakuwa na serikali ya Tanzania Bara!? Au umeongeza yako!? Kama vipi edit huu uzi wako tuende sawa
 
Kwanini tusivunje muungano?
 
Mkuu, sehemu gani ya rasimu ya katiba ya jamhuri ya muungano imependekeza kutakuwa na serikali ya Tanzania Bara!? Au umeongeza yako!? Kama vipi edit huu uzi wako tuende sawa
N i Ibara ya 57 ambayo inaainisha muundo wa Muunganoo Mkuu.Zinatajwa Serikali tatu: Serikali ya Jamhuri ya Muungano,Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.Ndipo Serikali tatu zinapopendekezwa Mkuu WAHEED SUDAY
 
Last edited by a moderator:
Mi naona ni dalili ya kuvunyika kwa muungano huu sasa... serikari tatu n nn? Inamaanisha kila nchi itakuwa na kiongozi mkuu( rais) wa nch husika na atakuwa na madaraka na mamlaka kamili juu ya nchi yake. Kuwepo kwa serikali ya muungano ni gelesha ya kuziba ukweli kwamba muungano umevunjika! Kwahiyo Tanzania na Zanzibar zitakuwa zikitambuliwa kama nchi mbili sasa katika taasis za kimataifa na nchi za kigeni sasa!"""" Then mantiki ya muongano ni ip? Au iko wap? Ifike wakati tukubali kwamba muungano umevunjika! Yann tujidanganye na serikali ya muungano wakati mioyo na macho yetu vinashuhudia udhahiri wa muungano kuvunjika sasa! Ndugu watanzania wenzangu" asiye kubali kushidwa si mshindan" Hata ukienda vitan altenative zote zikishindikana dhidi ya mpinzan wako inabid unyooshe mikono juu" surrender" unaweza kupona..
 
Kama hatuwezi kuujenga Muungano basi watanganyika na wazanzibar % kubwa wapo tayari uvunjike!!
Isipokuwa CCM na wanachama wao wanagwaya muungano ukicollapse hali ya ulaji itakatika!
Wananchi ndo namba 1, wasipuzwe...
 
To be honest sioni sababu ya kupigana ngumi kwasababu ya kukataa Tanganyika isiwepo, msimamo wangu ni huu, tuwe na serikali MOJA ya TANZANIA au serikali 3, huu upuuzi eti mmeungana lakini mmeungana na nani hakuna anayejua....ni upuuzi, tena upuuzi zaidi ya upuuzi.
 
Back
Top Bottom