Sababu za kuwa na usingizi mwingi usioisha!

Dodoma moja

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Posts
307
Reaction score
182
Wakuu naomba msaada wenu siku za karibuni nimeandamwa na janga la usingizi mwingi usioisha yaani hata kama nikilala mchana lakini ifikapo saa 2 usiku naandamwa na usingizi hata siwezi kujizuia ukizingatia mimi ni mwanafunzi wa chuo hivyo nashindwa kusoma kabisa. Naombeni mnisaidie kama ni ugonjwa nijue pia matibabu yake ili hali hii iweze kuisha!
 

Naombeni msaada wakuu kwa anaejua
 
Utakuwa na tatizo la macho, na si ajabu huo usingizi unakuja kila unapoanza kusoma
 
Huenda umenenepa zaidi/uzito umeongezeka. Jitahidi kufanya mazoezi, km unapombeka punguza na angalia namna ya ulaji kwa ujumla.
 
Vip ukimka unajisikiaje viungo vya mwili??? Je vinakuwa vinauma??
 
Naombeni msaada wakuu kwa anaejua
.
je una dalili hizi?????
1. Kuwa na huzuni iliyopitiliza

2.kushindwa kufurahia kazi na mambo yaliyokupa raha hapo awali mfano tendo la ndoa
3 kukosa hamu ya kula au kula na kulala sana (usingizi kupita kiasi)
4.hali ya kukata tamaa na kujiona mwenye hatia (guity) au kujiona mtu wa kushindwa (a failure)
5.kuwa na hofu na hata kichefuchefu
6. Kuchoka mwili; maumivu ya kichwa na viungo
7. Mawazo ya kukata tamaa
8. Kukosa utulivu na kushindwa kufanya maamuzi hata madogo
 
Inawezekana umeongezeka uzito hiyo ni sababu kubwa ya kukufanya ujisikie uvivu na usingizi..lkn pia kama unafanya ngono au punyeto mara kwa mara lazima uchoke na hivyo kuhisi usingizi ni kawaida!..lkn pia unaweza kupima kisukari inaweza kuwa sababu!
 
Angalia maji unayokunywa, kama yana fluoride nyingi inaweza kuwa chanzo cha ugonjwa wako
Note: Sio watu wote wanaoathirika na fluoride ila kuna watu inawasumbua sana
If its true anza kunywa maji ya chupa yatapunguza kiwango cha fluoride unachotumia na maziwa tafuta scimmed milk. Isipokusaidia nenda hospital although I doubt kama utakutana na daktari wa kukupa ushaur huu
 

Ni kweli mkuu dalili hizo ninazo hivyo naomba unisaidie nifanyaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…