Sababu za Majaliwa Kuwekwa bench Mkutano wa Mabeberu

Sababu za Majaliwa Kuwekwa bench Mkutano wa Mabeberu

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
Uwanja wa Diplomasia tumefuatilia baadhi ya mijadala mitandaoni na kuona watu wakiuliza kwa nini Waziri Mkuu alikaa nyuma ikiwa yeye alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika Mkutano wa Russia-Africa pale Sochi?

*JIBU NI HILI.*

Kwa mujibu wa mpangilio wa kikanuni yaani itifaki (Protocol) hasa kwa kuzingatia Mkutano Mkubwa kama huo ambao Marais wengi walihudhuria sambamba na Makamu wa Rais mbalimbali na Mawaziri Wakuu marais hupangwa pamoja kwa kuzingatia nani wa kwanza kuingia madarakani kabla ya wenzake wote, hufuatia yule aliyefuata mpaka wa mwisho ambaye ameingia hivi karibuni madarakani (Hii huitwa order of precedence).

Kwa lugha nyingine, mpangilio wa order of precedence huzingatia viongozi wa kada moja (Mfano Marais peke yao, Makamu wa Rais peke yao, Mawaziri Wakuu peke yao n.k) kwa kuangalia ni mwaka gani kwa mara ya kwanza kiongozi aliingia madarakani na tangu wakati huo mpaka muda wa tukio bado yupo madarakani.

Zingatio ni kwamba huyo kiongozi aliyeingia madarakani awe hajaondoka madarakani toka wakati alipoingia mpaka muda huo wa tukio.

Order of precedence huzingatia pia:

(1) Muda ambao kiongozi alikula kiapo (Nani wa kwanza kula kiapo)

(2) Historia ya kuwepo madarakani kwa mfano kwa hapa Afrika Mashariki (EAC) Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda yupo madarakani tangu mwaka 1986.

Hivyo mpangilio unampa yeye nafasi ya kwanza isipokuwa kama Mwenyekiti wa Jumuiya wakati wa Mkutano wa EAC si yeye.

(3) Nani wa kwanza kuwasilisha hati kwa Rais (Hii ni kwa mabalozi).

Wanaofuata kupangwa ni Makamu wa Rais wa nchi mbalimbali ambao nao hufuata utaratibu huo wa nani wa kwanza kuingia madarakani mpaka yule aliyeingia madarakani hivi karibuni.

Baada ya hapo hufuata Mawaziri Wakuu nao hupangwa kwa utaratibu huo huo.

Hapo ndipo unapoona Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa akikaa pale alipopangiwa.

Mpangalio mchanganyiko kama wanavyoonekana kwenye picha Marais, Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu kwa ujumla wake huitwa Order of Seniority.

Order of Seniority huzingatia ukubwa wa viongozi kimamlaka (hierarchy) kwa viongozi wa kada mbalimbali wanapowekwa pamoja.

Mpangilio huu huwa tunauona sana kwenye matukio ya Serikali Tanzania mfano Sherehe za Uhuru wa Tanzania bara, Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na Muungano ambapo huwa kuna mchanganyiko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Spika wa Bunge la Jumhuri ya Muungano wa Tanzania na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa ufupi, Order of Seniority huzingatia:

(1) Umri wa kuwepo madarakani

(2) Muundo wa kazi au utumishi

(3) Mchanganyiko wa uwepo wa viongozi wa kada mbalimbali mfano, Wafalme na Malkia, Marais, Wakuu wa Serikali (Kwa nchi ambazo ni za monarchy kama Ethiopia na Uingereza)

Ni imani yetu tumeelewana.

Abbas Mwalimu (Facebook & Instagram)
 
Hao mabeberu hawana nia njema na Africa
Hata Majaliwa asingeenda Hakuna faida
Wanashirikiana na CCM, chama cha kikomunisti cha korea, kilitufundisha namna ya kuiba kura kwenye chaguzi, ndicho kilitupa magari ya msaada KORANDO na mpaka leo wanafundisha jeshi letu wakisaidiana na CHINA, hawa nao si mabeberu?
 
Mkuu naomba kujuzwa kiitifaki kati ya Rais na mfalme nani anatakiwa akae mbele,kwa mfano umemualika King Mswathi III wa eSwathini na Rais Yoweri Mu7 wa Uganda ?
Museven atakaa mbele kwakuwa amekaa madaakani muda mrefu zaidi, tangu 1986.
Mswati hana muda huo kama museven.

Haiwezi na haijawahi kutokea viongozi wakachaguliwa siku moja, mwaka mooja na ikitokea hivyo hawawezi kuapishwa siku moja, so bado itifaki itazingatiwa
 
Magufuli because of his incompetence anashidwa kufanya kazi yake ya kuiwakilisha nchi kwa kisingizio cha gharama while kila siku akiwa live hata katika mambo yasiyo ya msingi
 
Asante kwa elimu. Tupiapo na kiambatisho Cha picha
Alikuwa nyuma sana, hakuonekana na baada ya kilio cha wengi hasa MATAGA kuanza kumchongea kwa Jiwe kuwa katumwa mkutanoni akaenda shopping ndio maana nikaamua kuleta hapa elimu
 
Bongo MNA maneno nilidhani unatujuza nini kimeongelewa kumbe nani kawa wa kwanza, jamani mb zangu mbona Hanna huruma
 
Hiyo order hufuatwa hata kama Kuna Marais wa dunia kama POTUS , Uchina , Russia ama PM wa UK? Yaani Mu7 ama KG akae mbele ya Trump ?
 
Back
Top Bottom