Sababu za Majaliwa Kuwekwa bench Mkutano wa Mabeberu

Chadema hakuna mpangilio mfano Joyce mukya akiwepo atakaa high table na mbowe
 
Siyo kweli. Kwenye mikutano ya namna hiyo ni nchi ndo inakaribishwa siyo kiongozi kwa cheo au jina kwa hiyo Meza Kuu mbele ya kila kiti kunakuwa na jina la nchi iliyokaribishwa na kukubali kuhudhuria. Nyuma yake kunakuwa na viti kwa ajili ya wasaidizi waliofuatana nae ndo maana ni muhimu kuwakilishwa na mtu mwenye hadhi ya mkutano husika. Marais wengi hasa wa Afrika hawajulikani kwa majina wala sura lakini nchi zinajulikana.
 
Kuna kitu hakijakaa sawa. Inamaana ikitokea saa 1 kabla ya mkutano rais akapata dharula na kulazimika kurudi nchini kwake huku akiwakilishwa na Waziri Mkuu pale pale na seat yake inabadilishwa?
 
Mkuu naomba kujuzwa kiitifaki kati ya Rais na mfalme nani anatakiwa akae mbele,kwa mfano umemualika King Mswathi III wa eSwathini na Rais Yoweri Mu7 wa Uganda ?

..wote[ Mswati na Mu7] ni HEADS OF STATE.

..kwa hiyo watafuata ni nani alimtangulia mwenzake kuingia madarakani.

..mkutano wa Russia ulihudhuriwa na Viongozi wengi ambao ni Head of State, sasa kwasababu Majaliwa siyo head of state wa Tz, ndiyo maana amewekwa back bench.
 
Acha upotoshaji,huoni mstari ule wa mwisho pia alisimama Rais wa Rwanda Paul Kagame?
 
Nadhani sasa CHADEMA wamekuelewa!

..Na itifaki hiyohiyo inatumika ktk kupata nafasi ya kuzungumza na kufanya majadiliano ya kui-market nchi yako.

..Ukipeleka uwakilishi wa ngazi ya chini, na wenyeji nao watakupata umuhimu mdogo kuonana na ujumbe wa nchi yako, na kusikiliza hoja zako.

..Magufuli kama ana nia ya kweli ya kubana matumizi aachane pia na utaratibu wa kuwakilishwa na VP Samia au PM Majaliwa.

..Tofauti ya GHARAMA za msafara wa Raisi na msafara wa Makamu au Waziri Mkuu nje ya nchi ni ndogo sana.



..Kwa maoni yangu, Raisi ana sababu nyingine za kutokusafiri nje, gharama siyo tatizo.
 
Hiyo order hufuatwa hata kama Kuna Marais wa dunia kama POTUS , Uchina , Russia ama PM wa UK? Yaani Mu7 ama KG akae mbele ya Trump ?
raisi wa usa na mataifa yote yaliyopo kwene UN security council huwa yanakuwa na veto power na mataifa yao huwa ni senior kwa mengine hivo maraisi wao kiprotokali uwa ni seniours
 
hahha zile nchi ndio huandikwa ila mpangilio wa kukaa sheria ya protokali na itifaki huchukua nafasi, wanawakilisha nchi sawa ila namna yakukaa au misafara kuingia na kutoka wanapokuwa viongozi mkubwa huwa uwaanza.....ndio protokali sio swala la nchi
 
Mkuu naomba kujuzwa kiitifaki kati ya Rais na mfalme nani anatakiwa akae mbele,kwa mfano umemualika King Mswathi III wa eSwathini na Rais Yoweri Mu7 wa Uganda ?
Kinachoangaliwa hapo ni kama mtu ni head of state au head of government, halafu mambo ya seniority.

Kwa mfano, Magufuli akienda kwenye kikao, halafu Waziri Mkuu wa Uingereza akawa katika kikao hicho pia, Magufuli anatakiwa apewe kipaumbele kwa sababu yeye ni Head of State, Waziri Mkuu wa Uingereza ni Head of Government tu, si Head if State.

Niliongelea mkutano wa Yalta na jinsi Winston Churchill alivyopata tabu kwa kuwa alikuwa Head if Government aliyekaa na Heads of State kina Roosevelt na Stalin.
 
Nilitegemea kusikia habari ya nini aliteta na "mabeberu uchwara" chenye manufaa kwa wanyonge wa Tz kumbe ni upuuzi tu wa nani alikaa wapi na upupu mwingine! Yana tija gani kwa wanyonge?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…