na mtoto akikosea unamfanya nini? Wewe ukikosea anakulamba makofi?
Wanawake mnaanza kupigwa kdg kdg leo kofi moja kesho mawili mtondogoo ngumi, mwishowe atakucharanga na visu
Anayekuudhi/aliyekuudhi duniani ni mkeo tu? Mwalimu wako hajawahi kukuonea, utawala wa sasa hujawahi kuudhi? Hujawahi kunyimwa haki zako? Je kwanini huwanasi vibao hao wengine?
Unamnasa kibao mkeo kwakuwa wamliki, au kwakuwa hawezi jidefend? Mimi nakuona weak; n u take all ur trouble to the vulnerable and defendless being like mkeo!
sasa mtoto utamlinganisha na mtu mzima? kwa bahati mbya/nzuri cjawahi kumkosea.
hapo kwenye red mkuu naona bado unaongelea wanawake wa kipindi cha mama zetu co hawa wa dot.com
Two Wrongs dont make a Right...
Hakuna sababu hata kubwa vipi inayo-justify kumpiga mwenzako..., au kupigana sababu akikuanza kukupiga ukamrudishia thats kupigana.., kama hamuwezi kukaa pamoja bila makonde its better mmoja akachukua hamsini zake cause ugomvi wenu unaweza kuleta athari kwa watoto...
Kuhusu sababu ya kufanya hivyo sio moja wala sio general kwa wote ;
tabia; addiction ya kupiga na kudhani bila kupiga hawatapata wanachotaka; mila na desturi; ni njia rahisi ya baadhi ya watu kutoa hasira zao; domination tendencies; low self esteem; insecurity n.k.
unazungumzia kumpiga mke kwa vp,say amekosa/amefanya maudhi au basi tu wajisikia kumpiga. wangu alishawahi kuniudhi nilimnasa vibao viwili na later aligundua kuwa ni kweli alikosa. hii nayo utasema ni nn?
sasa mtoto utamlinganisha na mtu mzima? kwa bahati mbya/nzuri cjawahi kumkosea.
inawezekana unaamini mwanamke akipigwa ndo anajua kapendwa? Hv unampiga huyo ni mtoto? Na pale mwanaume anapokosea,mwanamke ashushe kipigo au kwa kuwa wao hawana nguvu? Mie nadhani ukimpenda mke/mume na kumthamini huwezi kunyosha mkono wako juu yake, mtazungumza kama watu wazima na kumaliza tofauti. Kumpiga mwenza wako ni dharau ya hali ya juu.
Mwanamke hapigwi ngumi, anapigwa na kitenge tena wax original
Ninavyo fahamu hakuna sababu maalum ya kumpiga mwenzi wako
Ukiondoa hali ya hasira iliyoshindwa kudhibitiwa
Au hali ya uanaumelism
Au kutoka kushuka
Au kutochukuliana n.k
Mke wangu nilishawahi kumdunda alinijibu vibaya mbele ya mama mzazi nikampeleka chumbani tukajadiliana akakiri kutorudia tena akaja akanijibu tena vibaya mbele ya dada yangu nilimwita chumbani nikampa za ndosi tangia siku hiyo heshima mbele
Kwanini wanataka kuonesha ubabe? Ina maana hawajiamini au? Na kama ndivyo hiyo ndiyo njia pekee yakuonesha wako ontop?
Najua wengi hamjaishi kwenye ndoa ila mara nyingi wanawake ni watu ambao hawawezi kustand by their own wanataka kila kitu wasimamiwe au wakumbushwe so kwa wale ambao hatuwezi vumilia actions must take placeHivi ulijiuliza kwanini anakujibu vibaya? Na unauhakika hicho kilichomfanya akujibu kunya kimeisha?
kaunga hapo wkenye red umeniliza dada. kweli watoto wetu tunawaweka kwenye wakati mgumu sana. Jamani hii thread mbona inatufanya tufunguke kuliko?? imenikumbusha rafiki yangu mwanae wa mwaka na nusu enzi hizo alikimbilia kabatini akilia baada ya kuona baba yake anataka kumpiga mama yake............ bahati nzuri wote wawili walijikuta kwa wakati mmoja wanamkimbilia na kuanza kumbembeleza. But ni picha mbaya sana tunayowapatia wenetu.Nailyne you can say it again!
Sikutaka kumjibu maana nilimuona mbishi tu; especially anaposema kuwa hajawahi kumkosea mwenzie! Huo ni ubabe tu na kutojiamini; huenda pia amekulia kwenye abusive home, baba kumpiga mama yake ilikuwa ni sehemu ya maisha! Na kwakweli hii ni mbaya kwani watoto wanajifunza toka kwetu!
Nakumbuka mimi mtoto wangu alimuuliza stepdad wake; kwamba kwanini unampiga mama? Aisee ilipofikia hivyo nikasema enough kwani sikutaka mwanangu aathirike kisaikolojia!
Najua wengi hamjaishi kwenye ndoa ila BAADHI ya wanawake ni watu ambao hawawezi kustand by their own wanataka kila kitu wasimamiwe au wakumbushwe so kwa wale ambao hatuwezi vumilia actions must take place
Baba Erick bana........kumbe kile kiapo cha kitakupenda katika shida na raha, ugonjwa na afya.......nikupende, nikulinde, nikutii huwa kinamaanisha nini?
................Mimi nina mtaamo tofauti kidogo kuwa kama ni hacra ndo inakupelekea kureact namna ile nitakuelewa yaani ile mnaita reflex action.......imetokea ghafla ukajikuta tu umerusha kibao kwa kuwa kakuudhi! But eti unamwita mpaka chumbani hujaweza tu kudhibiti hacra zako??
Wanasema kama unajijua kuwa una hacra, jifunze kuwalk out of an argument!