Sababu za msingi za kumpiga mwenzi wako!

kikubwa kinachowapelekea kumpiga mwenza wake ni wivu na sifa za kijinga ndio zinapelekea huko..

Kwa wivu siwezi kumchapa kwani siyo dawa ya kutibu tatizo. Ila akiniletea wenge na dharau Namtandika mpaka vumbi inatimka!
 
kweli kaka unayosema na wanapokosea hawataki kukiri kosa huwa wanabisha au kutopenda kuomba msamaha au kuonyesha kujutia kosa.

Ukimpiga ndio atajutia kosa? Let's be honest; lengo hasa la kumpiga ni nini?
 
its complicated...........

I know it is; na nafikiri ni muhimu tudadavue vyema ili tupunguze hili janga (if at all tunaona ni janga).

Pls dadavua kidogo!
 
I know it is; na nafikiri ni muhimu tudadavue vyema ili tupunguze hili janga (if at all tunaona ni janga).

Pls dadavua kidogo!

wapo wanawake,tena wengi tu

ambao wanaona kabisa kuwa mwanaume strong lazima awapige

na ni tatizo la malezi...mfano...

umelelewa na baba aliekuwa anampiga mama yako....na unampenda baba yako
na kumkubali ......unafikiri binti wa aina hiyo hataona its okay kupigwa?

tena asipopigwa atamdharau huyo mume.....ipo saana hii
 
Kwa wivu siwezi kumchapa kwani siyo dawa ya kutibu tatizo. Ila akiniletea wenge na dharau Namtandika mpaka vumbi inatimka!

So unamtandika just because you can au? Na una uhakika anakudharau au unajihisi? Nasense dalili ya insecurity na low selfesteem hapo!
 
unakuta mwanamke ambae ni msomi
na anajifanya mbeijing.anaona its okaay mtoto wake wa kiume kumpiga mkewe
but sio yeye kupigwa
 
unakuta mwanamke ambae ni msomi
na anajifanya mbeijing.anaona its okaay mtoto wake wa kiume kumpiga mkewe
but sio yeye kupigwa

The Boss sitaki kuamini kuwa unamaanisha wanawake wengi wanataka kupigwa! Hata habari za wakurya zimepungua kwa kiasi kikubwa; so unamaana mwanaume anampiga mkewe ili kumridhisha come on bwana!

Nakubaliana na malezi ila hasa kwa kuendeleza tabia za watoto wa kiume kuwapiga wake zao kwani walimuona baba akimpiga mama; na wakike kuvumilia coz mama alipigwa lakini akavumilia!

All in all; wewe unafikirije ni kitendo kinachofaa hivyo kivumilike or we gotta put a stop to that?
 
Kuna mambo hapa ningeongea lakini najua kuna wanaume watanishambulia na wengine watasema naongea kwa vile bado sijaoa maana siku hizi tumekuwa na ile tabia ya kusema kwamba wewe bwana haujaoa subiri uoe ndio utaelewa tunachosema kwa hali ambayo nimeiona kama watu watabishana na mimi sawa tu ila nachotaka kusema ni kuwa asilimia kubwa ya matatizo kwenye ndoa yanasababishwa ni sie wanaume anayekataa aendelee kukataa lakini that's how i feel.

Hakuna mtu mwenye mamlaka juu ya mwenzake hata kama ulitoa mahari isiwe kama vile tunafanya biashara ya utumwa kwamba nakumiliki hauna mamlaka ya kusema chochote, nakupiga nitakavyo kuna kitu kinaitwa low self esteem na insecurity, kuna wengine wamerithi hizi tabia kutoka kwenye familia zao, baba yake alikuwa akipiga mkewe basi na yeye anakua na idiology hiyo hiyo kuwa mwanamke hadi aelekezwe ni mtu wa kupigwa tu, msichana naye sababu amezoea kuona mama yake akipigwa basi naye akiolewa akipigwa na mumewe anaona ni sawa tu, imagine kati ya wanawake 10 wanaopigwa na waume zao ni wangapi wanaweza kutoka hadharani na kujitoa kwenye lindi hilo la mateso kwa hesabu ya haraka haraka unaweza kukuta ni wawili tu kati ya hao kumi.

Sijaoa na kati ya vitu ambavyo ninamuomba Mungu ni kuwa hata ikitokea nimekosana na mke wangu hata siku moja isije ikatokea nikampiga hata kofi kwa kuwa Mama yangu ameishi maisha ya heshima bila kupigwa na marehemu Baba yangu hata kama walikuwa wanatofautiana sijawahi kuona hata siku moja Mama yangu ana makovu au kavimba uso sababu ya kupigwa sasa kama ndio hivyo why should i do that to my wife?? Eee Mungu nisaidie.
 
Hakuna sababu ya kumpiga mkeo. Kama watu wazima mnaona kuna kosa ni vizuri kujadili kuliko kuanza kurushiana ngumi.
Mi naona kumpiga mkeo ukihisi ndio namna nzuri ya kumrekebisha unazidi kujenga matatizo.
Naomba mungu nisipate mume wa hivyo maana sitovumilia hata kofi moja.
 
Thank you The Finest; Keep it up na endelea kuwaelimisha vijana wenzako. Ukiwaelimisha hata wawili tu; that is a big achievement; though kwa upande wetu pia tuna kazi sana ya kuwacouncil watu kama Angela ambao wameathirika na hawajaweza kurecover!

Ubarikiwe!
 
nimesema hapo juu its complicated

the finest msingi wake mkubwa ni baba yake

sasa wale ambao wamekua wakiona baba anampiga mama utawalaumu??????

hiki kitu kiko deep mno.....ingawa tunatakiwa kukipiga vita saana

but ni vizuri tukapunguza lawama tukaanza kuangalia chanzo.ambacho most of time nimalezi.....

sio tu kwa wavulana,hata kwa wasichana....binti akiona its okay
mama yake kupigwa,anakuwa anaamini kuwa mwanaume akikupiga its okaay
 

Mungu atakusaidia utampata mume kama The Finest; ila nawe usimtie pressure mdogo wangu TF! LOL

U right Hussy hata mimi so far sijaona sababu yoyote imlazimishayo mume kumpiga mke, zaidi ya insecurity ya wanaume! Si unajua adhabu zinazotukomeshaga wanawake ambazo wanaume wenye busara huitumia eeh....... That dark silence... Umekosa na unajua mumeo amegundua then hasemi chochote! Ge'ez that hurts kuliko anything! It is shame stupid psychopath r not smart enough to use that; they end up being physical tu!
 
The Boss kwa hapo juu nakubaliana na wewe! What kind of parenting do we provide kwa watoto wetu ndio itakayozaa wababa na wamama wakesho! Na ni kweli iko deep kwani ni lazima tuwajengee confidence!

Sasa kama sisi wenyewe twapigana; tukanana na hatuna maadili maana yake twalea watoto wawe kama sisi. Nakiri hata mimi sijaona wala kusikia baba yangu akimpiga mama though alikuwa mywaji; nafikiri ndio maana niliachana na abusive relationship!
 
Akikupiga niambie mimi naita FFU kabisa inakuja kumchukua lol

Thanks Kaunga kama tukijenga familia bora, tukiheshimiana na kuthaminiana pia kumshirikisha Mungu kwenye kila jambo binafsi naamini tutajenga familia bora sana pamoja na magumu ambayo tutakutana nayo

The Boss observation yako nakubaliana nayo kabisa, malezi in one way ir the other pia yanachangia
 
hakuna uhalali wa kumpiga mke, ni ujinga na ubabe wa kishamba wa baadhi ya wanaume (ambao mara nyingine wanawake wengine wanauendekeza na kulea maradhi)

Mimi naamini pale mwanamke anapoleta dharau za kujirudia mbele za watu anastahili kibondo mnapokuwa faragha!!
 

kuna rafiki yangu akimkosea tu mchumba wake anakula kichapo.
Sipati picha akishaolewa itakuwaje.
Sometimes nahisi sisi wanawake tunawaendekeza hawa watu. Kuna wanawake wamekuwa wanyenyekevu sana.
 
kuna rafiki yangu akimkosea tu mchumba wake anakula kichapo.
Sipati picha akishaolewa itakuwaje.
Sometimes nahisi sisi wanawake tunawaendekeza hawa watu. Kuna wanawake wamekuwa wanyenyekevu sana.

sio kuwaendekeza
kuna kitu kinaitwa sub conscious..
its deep..........
 
Akikupiga niambie mimi naita FFU kabisa inakuja kumchukua lol

hahahaha! Ataanzia wapi kwanza.
Kaunga ananiombea niwe na mume kama the finest wakati the finest mwenyewe ngumi mkononi.
 
Kaunga sijui huyu Hussy kasikia, weee Husninyo umesikia usinitie presha lol!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…