Sababu za msingi zinazopelekea 'afande' wa ulawiti asikamatwe ni hizi?

Sababu za msingi zinazopelekea 'afande' wa ulawiti asikamatwe ni hizi?

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Wiki hii tumeshuhudia vijana 4 kati ya 6 waliofanya uhalifu wa kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakifikishwa mbele za Pontio Pilato na kusomewa mashtaka, ijapokuwa walikana kuhusika na kitendo hicho kibaya.
1000099332.jpg

Watuhumiwa 4 waliombaka na kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakiwa mahakamani

Jambo la kushangaza na ambalo watanzania wengi wanashindwa kupata majibu ni kwanini 'afande' aliyewatuma wale wahuni (na ambaye alisikika akiombwa msamaha na binti aliyekuwa akibakwa na kulawitiwa mubashara) hakamatwi? Swali la pili ni je, wale watuhumiwa 2 wa ulawiti waliobaki ni akina nani na kwanini hawakamatwi? Je, wana uhusiano wowote na huyo afande asiyekamatika? Hiki ndicho kitendawili ambacho watanzania wangependa kupata majibu yake.

Kabla ya kutoa majibu na kueleza kwanini afande hakamatiki, naomba nirejee kesi 2 zinazofanana na hii ya afande zilizowahi kufikishwa mahakamani na kugonga mwamba.

Kesi ya kwanza ni ile ya aliyekuwa kamanda wa upelelezi wa Dar es Salaam, ndugu Abdallah Zombe ambaye aliwatuma askari polisi kuwaua wafanyabiashara wa madini na kuwapora mamilioni ya fedha. Kwa ufupi, kesi ilipotinga mahakamani, wale askari waliotumwa kuua walijitetea kuwa walifanya mauaji yale kwa kutii amri ya mkubwa wao wa kazi, ndugu Zombe. Baada ya kesi kuunguruma kwa muda mrefu, huku wananchi wakidhani Zombe hachomoki kwenye kesi ile, hatimaye aliachiwa huru. Wale askari waliohusika na mchakato wa mauaji wakahuhumiwa vifungo vya maisha na kunyongwa. Lakini baadaye askari wale walikata rufaa na baadhi yao kufanikiwa kujichomoa. Aliyekutwa na hatia ni mmoja wao anayeitwa Bageni, ambaye alihukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Katika kesi hii kuna facts mbili za kisheria zilizotumika. Fact ya kwanza ni ile ya mtu mzima mwenye akili timamu kutumwa na mtu mwingine kutekeleza uhalifu. Sheria haimhukumu aliyetuma bali humhukumu mtumwaji, hata kama mtumaji anajulikana na yeye mwenyewe kukiri kuwa kweli aliwatuma. Ndio maana Zombe aliachiwa huru bila shuruti.

Fact ya pili katika kesi hii ni uhusika wa mtu binafsi katika kutenda uhalifu. Baadhi ya askari waliachiwa huru kwa kuwa hawakuhusika kuwapiga risasi wafanyabiashara. Aliyehusika kufyatua risasi na kuua ni mmoja tu, naye ni Bageni. Ndio maana askari wengine waliachiwa huru, akahukumiwa Bageni tu.

Turejee kwenye kesi ya pili iliyomhusu mke wa Bilionea Msuya kuwatuma watu kumuua wifi yake (mdogo wake bilionea Msuya). Mahakamani ilithibitika kweli mke wa bilionea Msuya aliwatuma watu kufanya uhalifu. Na pia kisu kilichotumika kufanya mauaji kilipatikana na alama za vidole za wahalifu. Lakini mahakama ilitumia busara za kisheria kuwaachia huru watuhimiwa wote, akiwemo mke wa Msuya. Kwanini? Kwa sababu mtumaji hana kosa kisheria. Pia hata kama fingerprints za wahalifu zilionekana kwenye kisu, hakuna mtu mwenye uhakika kama kweli wao ndio waliua. Umeona eeh?

Sasa turejee kwenye hoja yetu ya msingi. Kuna baadhi ya mitandao ya kijamii (sio JF) imemtaja na kumuonesha hadharani afande aliyewatuma wale wafiraji kumdhulumu binti wa watu haki yake ya msingi. Pia haiwezekani binti aliyedhulumiwa amuombe afande msamaha hadharani halafu polisi wasimuombe awapeleke nyumbani kwa afande ili wamkamate. Haiwezekani.

Ni wazi kwamba afande anajulikana isipokuwa hata kama atakamatwa hatakuwa na kesi ya kujibu, kwa kuzingatia mfano wa kesi mbili nilizozitaja hapo juu ambazo watumaji waliachiwa huru bila shuruti. Kwa hiyo, polisi wanaona hata kama wakiamua kumpeleka afande mahakamani wataambulia patupu. Illmradi wahalifu wamekamatwa, hakuna haja tena ya kusumbuka na afande kwa kuwa hata akipelekwa mahakamani, hana kesi ya kujibu.

Sheria inatambua kwamba mtu mzima unapotumwa kutenda uhalifu nawe ukakubali kufanya hivyo, sheria itakuangukia wewe uliyetenda uhalifu na wala sio mtu aliyekutuma. Kwa hiyo, watanzania, hasa wale msiojua sheria, tulizeni mumkari na muendelee kuwa watulivu wakati wabakaji na wafiraji waliohusika kumdhalilisha binti wa Yombo Dovya wakishughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Nawasilisha.
 
Hili ndo nilikuwa nasema watu wanataka watu wapandishwe kizimbani kwa mihemko tu hawajui mahakamani ni ushahidi usio shaka ndo unasimama, kwa hiii kesi kumkuta na hatia huyu mama ni kazi sana maana inabidi ueleze kinaga ubaga chain yake na hao watu na uthibitishe kuwa yeye aliwatuma jambo ambalo si rahisi. Hii dunia ya mitando ni ngumu sana kwenda nayo maana kila mtu ni mtaalam na hisia ni bora zaidi kuliko ukweli
 
Hili ndo nilikuwa nasema watu wanataka watu wapandishwe kizimbani kwa mihemko tu hawajui mahakamani ni ushahidi usio shaka ndo unasimama, kwa hiii kesi kumkuta na hatia huyu mama ni kazi sana maana inabidi ueleze kinaga ubaga chain yake na hao watu na uthibitishe kuwa yeye aliwatuma jambo ambalo si rahisi. Hii dunia ya mitando ni ngumu sana kwenda nayo maana kila mtu ni mtaalam na hisia ni bora zaidi kuliko ukweli
Umeongea jambo la msingi sana mkuu. Watu wanahemka tu wakati hawajui sheria za nchi zinavyokwenda
 
Polisi wanapaswa kujua kwamba Amri yoyote inatolewa na kiongozi wake wa kazi haijalishi ana cheo gani ya KUUA/KUBAKA/KULAWITI/KUTEKA Raia wa TANZANIA ni AMRI BATILI.

Na msalad ukibumburuka utadakwa wewe ulitekeleza hio amri sio aliyeitoa.

Yeye atahamishwa tu kutoka ofisi Moja kwenda nyingine.

Wewe utaenda kunyea DEBE/MTONDOO.

So kabla ya kutekeleza amri za kikatlli fikiria kwanza.

Ni heri ukufuzwe kazini Kwa kutotii amri BATILI kuliko ugeuzwe status kuitwa mfungwa/mtuhumiwa/muuaji na hatis haitokuacha ikiwa utamwaga damu ya watu.

HATA POLISI WANAPASWA TAMBUA KUWA HAWAPO SALAMA ANYTIME MSALA UTAKUPATA WATZ WAKIAMUA

utaicha familia kitaa Raia wanakusaidia mkeo.

Usiwe baba au mama mpumbavu.
 
Kwaiyo angewatuma kumbaka first lady wa tz pia hangekua hana kesi ya kujibu mngekamata wabakaji tu na sio mtumaji......shuaniiiiii and rubbish..........
Sheria za nchi hazitambui mtu kutumwa mkuu. Hata ukituma wahalifu kumuua mtu na wahalifu kutekeleza mauaji, wewe mtumaji huna hatia hata kidogo.
 
Hili ndo nilikuwa nasema watu wanataka watu wapandishwe kizimbani kwa mihemko tu hawajui mahakamani ni ushahidi usio shaka ndo unasimama, kwa hiii kesi kumkuta na hatia huyu mama ni kazi sana maana inabidi ueleze kinaga ubaga chain yake na hao watu na uthibitishe kuwa yeye aliwatuma jambo ambalo si rahisi. Hii dunia ya mitando ni ngumu sana kwenda nayo maana kila mtu ni mtaalam na hisia ni bora zaidi kuliko ukweli
Kwa maana hiyo, kufadhil ugaidi sio, kufadhili mauaji sio kosa, kufadhili uhaini siyo kosa au
 
We useme tu aliewatuma ni mtu wao wanamlinda na sio porojo ulizoandika, kesi zote ulizo refer zimekuq na uonevu na ukakasi.

Swali, vijana wangerusha bomu kwrnye msafara wa kiongozi, polisi wasingetaka kujua master minder wa hiyo issue?

Acheni polojo, semeni tu aliewatuma ni mtu wao wanalindana
 
Back
Top Bottom