Sababu za msingi zinazopelekea 'afande' wa ulawiti asikamatwe ni hizi?

Basi sawa
Tutapambana naye huyo askari kivyetuvyetu
 
Kisheria, mtu anayewatuma wengine kutekeleza uhalifu anaweza kubeba jukumu la uhalifu huo. Hii inaitwa "ubia katika uhalifu" au "uandikishaji wa uhalifu." Sheria nyingi hutambua kuwa mtu anayepanga, kuagiza, au kushirikiana kwa njia yoyote na wengine katika kutekeleza uhalifu anaweza kushitakiwa kama mshirika au mhalifu mkuu, hata kama hakuhusika moja kwa moja katika kutenda uhalifu wenyewe.

Kwa hiyo, kutuma wengine kutekeleza uhalifu hakumuondolei mtu huyo hatia, na anaweza kushitakiwa na kufungwa sawa na wale waliotekeleza uhalifu.
 
Inabidi sheria zirekebishwe kwa kweli. Vinginevyo tutaendelea kuona watu wanawatuma watu kutenda uhalifu huku wakiendelea kula bata mtaani.
Hata ukiachiwa sio rahisi kivile msoto wa uhakika unaupata, kwahiyo ukifadhiri uhalifu uwe umejipanga na wakati mwingine mahakama ikigundua kuwa hiyo ni tabia yako utatafutiwa kifungu na unalamba mvua kama kawaida uje kuchomoka miaka kibao ilishapita.
 
Umeandika maelezo marrefu tena yanaashiria labda una ufahamu wa sheria japo kiduchu. Lakini umeshibdwa kuweka japo kifungu cha sheria kutetea hekaya uliyoweka hapa.

Hebu pata akili kwanza
 
Hakamatwi, hatakamatwa kwani "HAKAMATIKI" lbd ahamie Chadema, hapo "ATAKAMATWA"......
 
Ni wazi kwamba afande anajulikana isipokuwa hata kama atakamatwa hatakuwa na kesi ya kujibu, kwa kuzingatia mfano wa kesi mbili nilizozitaja hapo juu ambazo watumaji waliachiwa huru bila shuruti.
Mimi sita kuhoji kwa ujuzi wako wa sheria kama huu ndio ujuzi mnao fundishwa huko, sijui ni vyuo vya wapi hivyo; pengine "Jalalani" kama alivyo bainisha mmoja wenu.

Ila nakuomba utazame tu hayo maneno uliyo andika katika hiyo mistari miwili niliyo inyanyua hapo juu.
Unachosema wewe hapa, ni kwamba; hao wanaotakiwa kuwakamata watuhumiwa tayari wao wametoa hukumu nani atapatikana na kosa. Siyo kazi ya mahakama tena, bali ni kazi ya hao wenye mamlaka ya kufikisha watuhumiwa mahakamani.
Huu ni utaratibu gani tena?
Lakini pamoja na hayo yote, haya uliyo elezea hapa yangekuwa ndiyo sheria inayo jitosheleza, mbona tungekuwa nchi ya hovyo sana hii. Nina hakika kuna mifano mingi sana ya watu wanao kula njama kuwaumiza wengine, hata kama hawakuumiza moja kwa moja, lakini sheria inawabana. Wewe umetumia hiyo mifano miwili 'selectively' na kuiacha mifano inayopingana na hiyo ya kwako.
 
Katika kesi ya Msuya kama kumbukumbu zangu ziko sawa,Sharifu alihukumiwa kunyongwa au kufungwa maisha kwa kosa la kupanga njama na kufadhili mauaji ya Msuya.
Mkuu hii tunayosema hapa ni kesi ya mauaji ya mdogo wake Msuya aliyeuawa na wauaji waliotumwa na mke wa Msuya (wifi wa marehemu). Watuhumiwa wote waliachiwa huru wapo mtaani wanakula bata.
 
Huyo mleta mada, ni 'typical' kabisa wa hizi elimu za kushangaza sana zinazopatikana nchini wakati huu!
 
Inabidi sheria zirekebishwe kwa kweli. Vinginevyo tutaendelea kuona watu wanawatuma watu kutenda uhalifu huku wakiendelea kula bata mtaani.
Maana ya hiyo sheria, kama kweli ipo ni kwamba, aliye dhulumiwa/uawa au ndugu yake na yeye akijitahidi kumtafuta kichaa amfanyie kazi ya kumwondoa uhai huyo asiye patikana nahatia mahakamani kwa kuwatumia wengine; hii nchi itakuwa ya namna gani?
 
Mkuu hii tunayosema hapa ni kesi ya mauaji ya mdogo wake Msuya aliyeuawa na wauaji waliotumwa na mke wa Msuya (wifi wa marehemu). Watuhumiwa wote waliachiwa huru wapo mtaani wanakula bata.
Kwenye posti yako umedai "mtu anayepanga njama au kufadhili uhalifu sheria zetu hazimtii hatiani" ndio nikakukumbusha hiyo katika hiyo kesi ya mauaji ya bilionea Erasto Msuya,mtuhumiwa mmoja aitwae Sharifu alihukumiwa kwa kupanga na kufadhili mauaji ya bilionea huyo ingawa yeye mwenyewe hakwenda kwenye eneo la tukio la mauaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…