Sababu za msingi zinazopelekea 'afande' wa ulawiti asikamatwe ni hizi?

Mkuu hii tunayosema hapa ni kesi ya mauaji ya mdogo wake Msuya aliyeuawa na wauaji waliotumwa na mke wa Msuya (wifi wa marehemu). Watuhumiwa wote waliachiwa huru wapo mtaani wanakula bata.

Ndio maana unaambiwa unachagua mifano ile tu inayosapoti hoja yako. Huyu jamaa kakupa mfano wa kesi tofauti na zako mbili ambapo mtuhumiwa alikutwa na hatia ya kula njama na kufadhili mauwaji wewe unaanza tena kururusha maneno ili kuyumbisha mada. Unakosea sana kupotosha, maandishi yanaishi. Kwa wasojua watakuamini na utakuwa umechangia kuharibu jamii kwa kupandikiza maarifa feki.
 
Mimi sijaelewa,kwa nini huyo afande asikamatwe na wakati ukiangalia hawa watu walikua na common intention ya kufanya huo uhalifu wao, yani walikubaliana kutekeleza huo uhalifu either kwa huyo afande kuwalipa hao rapists or vinginevyo..huyo afande anachomokaje hapo yani na wakati yeye ndio ringleader wa huo uhalifu?
 
Kama haujataja hivyo vifungu vya sheria....nawe utakuwa sawa na hao wanaotaka mambo yaende kwa mihemko....

Hapo neno kisheria ,itakuwa inafuata nadharia ya sheria yako na maono yako na si sheria ya nchi....
Weka vifungu...
 
Hivi kumbe kuna kesi ukipanga uhalifu na ukafanyika lakini hukwenda kuutenda huo uhalifu hukutwi na hatia?
 
Kuhusu bageni kwanini asingesema alitii amri ya miubwa wa kazi kisheria?
 
Baadhi ya mambo nakubaliana nawe mkuu, kesi yoyote inayowahusu askari wa juu wa Jeshi la Polisi dhidi ya jamii huwa nafasi ndogo sana kupatikana haki.

Kwa kuwa, wao ndiyo wanaoandaa hati ya mashtaka, hivyo wanaweza kuiandaa kwa maslahi yao na mwisho wa siku kupata zawadi ya ushindi kortini.

Miongoni mwa mipango yao huwa inahusisha kuwatorosha watuhumiwa ambao maelezo yao yanaweza kufanya kesi iwe ngumu kwa askari hao.

Kwenye kesi ya akina Zombe, Saad Alawi na Rashid Lema walitoroshwa kwani, mmoja alitandika risasi na mwingine alipeleka miili muhimbili kwa hifadhi.

Saad hajarudi mpaka leo, ila Lema wazazi wake kwa hofu ya Mungu wakamlazimisha kurudi kuikabili kesi. Lakini, alikufa akiwa gerezani kabla ya kutoa ushahidi.

Zombe na wenzake wote wakaachwa huru, lakini kitu pekee kilichomponya Zombe ni kamapuni ya simu ya Vodacom kugoma kutoa ushahidi kortini.

Ni kwa kuwa, Zombe anasemekana alitumia simu (siyo radio call) kutoa maelekezo kwa Bageni ya 'kumalizwa' marehemu wale, na simu zilikuwa za Vodacom.

Hata serikali ilipokata rufaa ni Bageni tu ndiye aliyekutwa na hatia na kuhukumiwa kunyongwa. Ila kama Vodacom ingetoa ushahidi, Zombe angenaswa.

Vodacom walisema mtambo wao huwa unaharibu mazungumzo ya simu baada ya miezi sita tu tangu wahusika walipoongea kwa simu.

Kwenye kesi ya sasa, kutopatikana hao watuhumiwa wawili kunaweza kuwa kuko kimkakati pia kama Saad na Lema.

Hatujui Lema kama 'alilishwa mjusi' ama vipi? Maana alikufa katika siku ambayo alikuwa akisubiriwa kortini ili atoe ushahidi. Na Saad kapotea mazima.

Labda ingeundwa tume kama ya Jaji Kipenka, kwani polisi huwa hawawezi kujichunguza na kujipeleka kortini, hii ni kama asili kwa 'wadepo'.

Kwa hali hiyo, kazi ya kufanya hapa ni kulazimisha kutimia kwa watuhumiwa pamoja na 'afande' mahakamani. Ila kwa hawa wanne tu. Sijui?!

Ova
 
Tuna sheria za kipuuzi mno, zinazotoa mianya kwa wahalifu. Katika nchi zinazojitambua, mazingira haya yangeweka mapitio ya sheria ili kuhakikisha wahalifu hawakwepi mkono ww sheria.
Hayo mazingira bila shaka ni ya kimkakati kuwanasua wateule.
Rejea kesi ya Gekuli... Ghafla DPP akakacha.
Alafu huyo mume wake sasa. Siyo kama unavyojua. In brackets ni muendelezo wa upinde 🌈🌈🌈.
 
Hili sakata kama haikutendeka haki litatukatisha tamaa wengi.
Haki haitotendeka kama DPP atahusika kufungua kesi ya msingi.
Jingine usikute hata binti na wanafamilia wanasumbuliwa ili wajanja waseti mianya ya kujinasua.
Alafu jingine kubwa... Hii kesi ni uthibitisho kuwa upinde 🌈 🌈 umeota mizizi miongoni mwa mijimama.
 
Mku7 naona bado unarudi palepale. Kwani sheria za nchi zinabagua kati ya askari na raia?
Sheria za jeshi ni kwa ajili ya wanajeshi/askari ndio maana wana mahakama zao na zinatoa adhabu kuanzia za vifungo hadi kifo. Adhabu hizo huwa zinatekelezwq ili huku uraiani mnaweza msifahamu na hakuna mahakama yeyote ya kiraia inaweza kutengua au hata kusikiliza tu.

Kama yule mwanajeshi katika kesi hii ya ubakaji ingekuwa alitumwa na mkuu wake wa kijeshi. asingeshtakiwa uraiani na pia asingehukumiwa kwa kubaka labda kama alivujisha video angeshtakiwa kwa usaliti kijeshi na adhabu yake ni kifo.
 
Kumbe ukiamzisha na kulifadhiri genge la majambazi wakawa wanaua watu na kubaka na kulaeiti sio kosa kisheria?
Sheria zetu ni za ovyo sana. Huwezi kuamini zinawalinda walawiti, wafiraji, wabakaji na majambazi. Hii nchi ni ngumu sana.
 
Kuna kitu kinaitwa "lengo" la huo uhalifu. Hapa ndio huyo Afande anapoingia. By the way kuhusu Bageni, yeye alihukumiwa maisha na Wala hakuwapiga Risasi wale jamaa, kwa kuwa yeye ndiye aliyeongoza msafara wa kwenda kule mabwepande. Kiaskari Mkuu ndiye kiongozi wa msafara hivyo huko mabwendande walikokwenda kuuawa na yeye ndiye aliyeagiza waende huko kwani alikuwepo.
 
Kwenye kesi uchwara ya Ugaidi ya Mbowe unakumbuka kilichotokea!? Kwa nini walihangaika naye!?
 
Kama haujataja hivyo vifungu vya sheria....nawe utakuwa sawa na hao wanaotaka mambo yaende kwa mihemko....

Hapo neno kisheria ,itakuwa inafuata nadharia ya sheria yako na maono yako na si sheria ya nchi....
Weka vifungu...
Kama unadhani ni maoni yangu unakosea sana mkuu. Hizo references nimezitoa kwenye hukumu za mahakama za hapa nchini na zilizohukumiwa kwa kutumia sheria za nchi hii. Kama huamini hata matukio ya kweli, basi hilo ni tatizo lako binafsi mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…