Sababu za msingi zinazopelekea 'afande' wa ulawiti asikamatwe ni hizi?

Kwa mujibu wa sheria aliyerusha risasi, mkuki, mshale au bomu ndiye mwenye kosa. Yule aliyemtuma yupo huru kisheria. Ukienda kumshtaki mtumaji atachomoa kesi misa ya kwanza tu.
Sheria Tanzania zinatusumbua sana ndio maana tunawalipa wahuni mabilioni kila kukicha na kukamata ndege zetu tpaul upo busy kutafsiri sheria kama vile ni mechi ya Yanga vs Azam...toa vifungu sio maneno ya misa
 
Umeongea jambo la msingi sana mkuu. Watu wanahemka tu wajati hawajui sheria za nchi zinavyokwenda
Bado hujasema yaan hapo akipelekezwa hachomoki rejea Ile kesi ya Jamaa waliomuua yule Mzungu wa Tembo pale masaki walidakwa wote mpaka aliewatuma na Wote Muda huu wapo ndani kwa hio point zako hazina mashiko labda useme Polisi wanaegemea upande wa Polisi mwenzao hapo utaeleweka Ila hizo bla bla zingine ni ujinga tu kwa kiufupi lile libibi limefanya makosa makubwa kutuma kundi la Vijana kwenda kubaka na kulawiti na km Sheria haipo basi Sheria zetu zifanyiwe marekebisho hii ni loophole hawa watu inabidi waozee Jela tena ikibidi wanyongwe mpaka kufa
 
Sheria zetu zifanyiwe marekebisho hii ni loophole hawa watu inabidi waozee Jela tena ikibidi wanyongwe mpaka kufa
Hapa umeongea kweli kabisa mkuu. Huwezi kumfunga mtu bila kufuata sheria. Sheria zetu ndizo zenye matatizo.
 
Kazi ya Polisi sio kuamua kama ana kosa ama la.Wao wsnatakiwa kumkamata na kumpeleka Mahakamani.Mahakama ndo inayohukumu
 
Ngoja tusubiri tuone. Inaonekana kuna maagizo kutoka juu, ndio maana majina ya wale maafande waliohusika kwenye ubakaji hawatajwi vikosi wanavyofanyia kazi. Mijitu ya CCM ni ya ovyo sana. Kila siku inapenda kufuga uovu.
 
Hoja ya msingi ya inayothibitishwa ni kweli binti alilawitiwa na kubakwa na kama kweli alilawitiwa na kubakwa je watuhumiwa waliokamatwa ndio waliomlawiti na kumbaka hizo porojo zingine mtu ambaye hana kibakio anakujaje kisa tu afisa wa Polisi angekuwa muuza mchicha sokoni tusingesikia watu wanataka kufanya vurugu za kisiasa Polisi wakiwazuia mnawaona wabaya na kuwachukia wakati wanasimamia sheria zilizotungwa na bunge.Na Bado spana ziko palepale hutaki kufuata sheria una jiona wewe ndio wewe Polisi ongezeni dawa mpaki akili za kutii sheria bila shuruti ziwajie.
 
Lakini kwa kuwa binti bado anatunzwa na polisi, anaweza akashawishiwa kutomtaja aliyeagiza afanyiwe ufiraji ule.
 
Mtumaji na watumwaji wote wana makosa kisheria. Tatizo evidence ipi kuwa huyo afande aliwatuma!!! Majina yake yametajwa na kina Vigogo, tatizo ni ushahidi wa kuonyesha kuwa walitumwa na huyo mama wataupata wapi.
 
Zombe alichomoka kwa vile mashitaka yalibadilika na kuwa kuua. Badala ya kushiriki mauaji kama ilivyokuwa mwanzo
 
Kama hivyo basi watu watakuwa wanaagiza wenzao wauawe, wabakwe n.k na watabaki salama kabisa uraiani.
 

Nikusahihishe kidogo upo sahihi japo kuna kitu ume miss, Conspiracy inakuwa kosa pale ambapo mmepanga kufanya uhalifu fulani lakini ule uhalifu mliopanga kuufanya haukutimia ndio tunaita conspiracy.

Turudi kwenye hoja ya msingi, ni kwamba mtoa mada amepotosha, sisi tunafuata mfumo wa sheria za common law japo kwenye swala la parties to offence (watu waliohusika kufanya uhalifu) tumetofautiana nao kidogo.

Ipo hivi kwa mujibu wa sheria ya kanuni za adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019, kifungu cha 22 na 387 tuna parties to offence wawili ambao ni Principal Offenders na Accessory after the fact.

Principal offenders kwa mujibu wa kifungu cha 22 ya sheria ya kanuni za adhabu kinasema, principal offenders ni yule mtu atakayeshiriki kwenye uhalifu kwa kufanya yafuatayo
1. Mtu yeyote aliyeshiriki utekelezwaji wa uhalifu huo mfano kwenye kuua ukamchoma mtu na kisu wewe unakuwa principal offender.
2. Mtu yoyote atakayefanya jambo au hatofanya jambo kwa lengo la kumsaidia mtu mwingine afanye uhalifu, mfano kwenye kuua mtu, wewe ukatoa bunduki itumike kumuua mtu ila sio wewe utakaye shoot, bado pia utakua principal offender mana umesaidia kutekeleza wa mauaji.
3. Mtu yoyote atakae saidia utekelezwaji wa uhalifu nae ni principal offender.
4. Mtu yoyote atakae shawishi au kutuma mtu afanye uhalifu kwa niaba yake atakuwa principal offender, hapa ndio huyo afande anaesemakana anaingia.
Ukisoma pia vizuri kifungu 22 (3) kimesema kabisa hao principal offenders haijailishi umeshiriki vipi kwenye huo uhalifu adhabu yenu ni moja.


Accessory after the fact, kwa mujibu wa kifungu cha 387 cha sheria ya kanuni za adhabu, huyu ni mtu ambaye atakuwa ametenda uhalifu pale ambapo atamsaidia mtu alietenda kosa kukimbia mkono wa sheria, ina maana hapa uhalifu unakuwa umeshetekelezwa alafu mtuhumiwa anajaribu kukwepa mkono wa sheria na ukamsaidia kukwepa unakuwa umetenda kosa hili.


Kwa mantiki hiyo sasa Tanzania tuna Principal Offenders na Accessory after the fact, na afande anaingia kwenye principal offenders.

Kuhusu kesi alizoelezea mtoa mada hapo juu naona alizielewa tofauti, arudi tena akasome upya tena kama hiyo kesi ya Msuya ndio kabisa kapotosha ni kwa namna gani yule mama alishinda ile kesi.
 
Hata mbinguni utahukumiwa kwa matendo sio maneno
 
Wazazi tunafunga mkanda tunawasomesha halafu mnakuja kuwa wajinga wajinga
Mtoa mada ni kilaza sana hapo hajui kuna makosa ya kula njama na kufadhili uhalifu na haikuwa najukumu yake ya kazi
 
Utumbo mtupu.
kesi zote mbili ulizosema NI RUSHWA ILIYOTEMBEA SIO SHERIA.
yaani finger print zao zikutwe kwenye kisu alafu useme hakuna mwenye uhakika kama wao ndo walioua.
Unajua kuwa finger print hazifanani?zilikuwa xinafanya nini kwenye kisu kilichomuua marehemu?
 
Huyo dogo nyundo ana onekana ana dharau sana.
Kavaa t-shirt imeandikwa.ZIGO
NI JEURI KWA MAMLAKA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…