Sababu za msingi zinazopelekea 'afande' wa ulawiti asikamatwe ni hizi?

Umetuingiza chaka mkuu.

Sheria inamhukumu hata mtu aliyeshiriki tu kupanga njama za uhalifu tena anaweza kuwa Principal offender ama accessory before/after the facts.

Kwasababu mfumo wa kisheria wa Tanzania unafuata legislation/statutes na common law basi under common law mtu aliyeshiriki kupanga njama za uhalifu anaweza kuwa Principal offender in the first degree, or Principal offender in the second degree ama accessory before or after the fact kutegemeana na role played in the commission of the offence.

Kwa ufupi afande aliyewatuma naye ni mhalifu kwa mujibu wa sheria mkuu.
 
Kwa hiyo nikiwalipa watu na kuwatuma waje kukufanyia uhalifu mimi sina kosa pindi wakubainika? 🤔
 
Siyo tu kukosekana kwa ushahidi lakini pia haki lazima izingatiwe unapotamani yule binti aliyefanyiwa ukatili atendewe haki pia usisahau kwamba pia hata hao wengine wanastahili haki tukiendekeza kupeleka watu mahakamani ili wakachomokee huko huku ikijulikana kwamba wanakwenda kuchomoka ni uonevu ni kwanini tunalazimisha kwamba anaye tajwa na Meya mtaafu ndiye muhusika? Je,ni kweli ana mume? Upelelezi wa kesi kama hii hauitaji mihemuko wala chuki binafsi kwa taasisi usiyoipenda kwasababu bado mtazunguka kwenye shamba ileile ya ukiukwaji wa haki za binadamu mfano mzuri RPC aliyenukuliwa kwa kuwekewa maneno ambayo hakuyakusudia imempa usumbufu mkubwa na kama binadamu haki yake haitajadiliwa ila mwandishi wa habari aliyemuhoji ataonekana wa maana huku akiwa ameharibu maisha ya mtu kwaajili ya maslahi binafsi kwa mwamvuli wa kuhabarisha umma.
Kila mwananchi anajichukulia sheria mikononi mwake na kujitwishwa mamlaka ya upelelezi bila kusomea fani hiyo ni sawa na watu kujifanya wanajua kila kitu mpaka kumkosoa DAKTARI aliyesomea na kubobea kwenye fani.
Matarajio ni kukuza mtafaruku katika jamii pia waandishi wa habari watakuwa katika wakati mgumu wa kupata taarifa maana wanautaalamu wa kubadilisha kinachosemwa na kuleta taharuki ili habari iuzwe bila kujali kama italeta athari gani katika jamii.
 
Unaeleza kama tuko kijiwe cha kahawa! Kwa mujibu wa sheria mpangaji na mtekelezaji wote ni wahusika na ikithibitika mahakamani wote watahukumiwa kwa mujibu wa sheria. Mengine ni ukiukwaji wa sheria na hayapaswi kutolewa mfano.
 
Upuuzi tu, mbona kwenye kuwakamata wapinzani hawatendi kisheria?

Kwenye suala la kukamata polisi wenzao utasikia sheria, kukamata wapinzani hakuna sheria.

Huyo mama angekamatwa tu aonekane.
 
Upuuzi tu umeandika.
 
Huyo mtu ni mbumbumbu wa sheria, analeta story za kahawani. Kwa mujibu wa sheri kula njama na kutekeleza uhalifu yote ni makosa.
Yah! Iyo topiki nimeikumbuka maana ilikua assignment ya group nikaachiwa nifanye mwenyewe...
Labda mleta mada ndio afande mwenyewe anajitetea😆..

Conspiracy occurs when two or more persons agree to commit a crime-an essential feature for committing organized crime. One purpose of the conspiracy offence is to extend liability "backwards" by criminalizing the planning (or agreement) stage of a criminal offence.
 
Pia usisahau upepelelezi dhidi ya kupigwa risasi Lissu ulisumbua sababu dereva hayupo hivyo kama afande hakutajwa kwa jina ni ngumu mnooo maana ni kama hayupo ila yupo ila kama haonekani. Najaribu kuwaza kiafande afande kulingana na akili ulizoonyesha hapa.
 
Mkuu usiwe buh lawyer. Unafikiri kwanini Zombe na mke wa Msuya au wahalifu waliotumwa na mke wa Msuya (na fingerprints zao zikapatikana kwenye visu vilivyotekeleza mauaji) hawakutiwa hatiani?
 
Mtoa mada pengine umesahau kipindi kesi ya zombe kuna mashahidi muhimu waliuawa ili kuficha ushahidi, bila baadhi ya mashahidi kufa ni vigumu sana kuchomoka ndiyo maana watu tunataka huyo afande apande kizimbani haijalishi atachomoka au anafungwa.
Hata huyo zombe hakuishi Kwa Amani Hadi anakufa Kwa kifupi ni kama alikuwa jela tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…