Sababu za msingi zinazopelekea 'afande' wa ulawiti asikamatwe ni hizi?

Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Wiki hii tumeshuhudia vijana 4 kati ya 6 waliofanya uhalifu wa kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakifikishwa mbele za Pontio Pilato na kusomewa mashtaka, ijapokuwa walikana kuhusika na kitendo hicho kibaya.
View attachment 3074754
Watuhumiwa 4 waliombaka na kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakiwa mahakamani

Jambo la kushangaza na ambalo watanzania wengi wanashindwa kupata majibu ni kwanini 'afande' aliyewatuma wale wahuni (na ambaye alisikika akiombwa msamaha na binti aliyekuwa akibakwa na kulawitiwa mubashara) hakamatwi? Swali la pili ni je, wale watuhumiwa 2 wa ulawiti waliobaki ni akina nani na kwanini hawakamatwi? Je, wana uhusiano wowote na huyo afande asiyekamatika? Hiki ndicho kitendawili ambacho watanzania wangependa kupata majibu yake.

Kabla ya kutoa majibu na kueleza kwanini afande hakamatiki, naomba nirejee kesi 2 zinazofanana na hii ya afande zilizowahi kufikishwa mahakamani na kugonga mwamba.

Kesi ya kwanza ni ile ya aliyekuwa kamanda wa upelelezi wa Dar es Salaam, ndugu Abdallah Zombe ambaye aliwatuma askari polisi kuwaua wafanyabiashara wa madini na kuwapora mamilioni ya fedha. Kwa ufupi, kesi ilipotinga mahakamani, wale askari waliotumwa kuua walijitetea kuwa walifanya mauaji yale kwa kutii amri ya mkubwa wao wa kazi, ndugu Zombe. Baada ya kesi kuunguruma kwa muda mrefu, huku wananchi wakidhani Zombe hachomoki kwenye kesi ile, hatimaye aliachiwa huru. Wale askari waliohusika na mchakato wa mauaji wakahuhumiwa vifungo vya maisha na kunyongwa. Lakini baadaye askari wale walikata rufaa na baadhi yao kufanikiwa kujichomoa. Aliyekutwa na hatia ni mmoja wao anayeitwa Bageni, ambaye alihukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Katika kesi hii kuna facts mbili za kisheria zilizotumika. Fact ya kwanza ni ile ya mtu mzima mwenye akili timamu kutumwa na mtu mwingine kutekeleza uhalifu. Sheria haimhukumu aliyetuma bali humhukumu mtumwaji, hata kama mtumaji anajulikana na yeye mwenyewe kukiri kuwa kweli aliwatuma. Ndio maana Zombe aliachiwa huru bila shuruti.

Fact ya pili katika kesi hii ni uhusika wa mtu binafsi katika kutenda uhalifu. Baadhi ya askari waliachiwa huru kwa kuwa hawakuhusika kuwapiga risasi wafanyabiashara. Aliyehusika kufyatua risasi na kuua ni mmoja tu, naye ni Bageni. Ndio maana askari wengine waliachiwa huru, akahukumiwa Bageni tu.

Turejee kwenye kesi ya pili iliyomhusu mke wa Bilionea Msuya kuwatuma watu kumuua wifi yake (mdogo wake bilionea Msuya). Mahakamani ilithibitika kweli mke wa bilionea Msuya aliwatuma watu kufanya uhalifu. Na pia kisu kilichotumika kufanya mauaji kilipatikana na alama za vidole za wahalifu. Lakini mahakama ilitumia busara za kisheria kuwaachia huru watuhimiwa wote, akiwemo mke wa Msuya. Kwanini? Kwa sababu mtumaji hana kosa kisheria. Pia hata kama fingerprints za wahalifu zilionekana kwenye kisu, hakuna mtu mwenye uhakika kama kweli wao ndio waliua. Umeona eeh?

Sasa turejee kwenye hoja yetu ya msingi. Kuna baadhi ya mitandao ya kijamii (sio JF) imemtaja na kumuonesha hadharani afande aliyewatuma wale wafiraji kumdhulumu binti wa watu haki yake ya msingi. Pia haiwezekani binti aliyedhulumiwa amuombe afande msamaha hadharani halafu polisi wasimuombe awapeleke nyumbani kwa afande ili wamkamate. Haiwezekani.

Ni wazi kwamba afande anajulikana isipokuwa hata kama atakamatwa hatakuwa na kesi ya kujibu, kwa kuzingatia mfano wa kesi mbili nilizozitaja hapo juu ambazo watumaji waliachiwa huru bila shuruti. Kwa hiyo, polisi wanaona hata kama wakiamua kumpeleka afande mahakamani wataambulia patupu. Illmradi wahalifu wamekamatwa, hakuna haja tena ya kusumbuka na afande kwa kuwa hata akipelekwa mahakamani, hana kesi ya kujibu.

Sheria inatambua kwamba mtu mzima unapotumwa kutenda uhalifu nawe ukakubali kufanya hivyo, sheria itakuangukia wewe uliyetenda uhalifu na wala sio mtu aliyekutuma. Kwa hiyo, watanzania, hasa wale msiojua sheria, tulizeni mumkari na muendelee kuwa watulivu wakati wabakaji na wafiraji waliohusika kumdhalilisha binti wa Yombo Dovya wakishughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Nawasilisha.
Kwa mchanganuo huu was kipimbi sisi Kama taifa tinasafari ndefu Sana ya kupambana na ujinga! Hivi neno "kula njama " peke yake ni kosa ! Ieleweke kwamba kupanga mipango ya kufanya uhalifu ndio kwa lugha ya kimahakama ndio wansema kula njama! Sasa huyo afande aliepanga hiyo mipango ya kubaka anatokaje kwenye hii case ??
 
Asante sana kwa nondo hii muhimu sana mkuu. Ubarikiwe mno.
unasifiana ujinga kwa kujiona wajuaji kumbe vilaza tu, kula njama ni kosa kisheria usichojua au kwa makusudi hutaki kujua ni kuwa si kila anaye shitakiwa mahakani atatiwa hatiani zombe na mke wa msuya hawakutiwa hatiani kwa kukosekana ushahidi usitia shaka juu ya uhusika wao kwenye makosa waliyoshitakiwa lkn sio kwa sababu ukituma mtu kufanya kosa wewe uhusiki waliendesha mashitaka walishindwa kudhibitisha kama kweli wao waliwatuma wale waliotekeleza yale mauaji.
 
Mkuu umetoa ufafanuzi uliojitosheleza. Mtoa hoja huenda ana maslahi na kesi hii. Huenda ana ujamaa na huyo afande mtuhumiwa. Kwani hata akipelekwa mahakamani na kwa bahati akachoomoka, polisi watapata hasara gani. Huwa wanawambabikiza kesi viongozi wa upinzani kwa makesi ya kijinga ambayo huwa hayana mashiko mahakamani.
Pamoja sana mkuu.
 
Polisi wanapaswa kujua kwamba Amri yoyote inatolewa na kiongozi wake wa kazi haijalishi ana cheo gani ya KUUA/KUBAKA/KULAWITI/KUTEKA Raia wa TANZANIA ni AMRI BATILI.

Na msalad ukibumburuka utadakwa wewe ulitekeleza hio amri sio aliyeitoa.

Yeye atahamishwa tu kutoka ofisi Moja kwenda nyingine.

Wewe utaenda kunyea DEBE/MTONDOO.

So kabla ya kutekeleza amri za kikatlli fikiria kwanza.

Ni heri ukufuzwe kazini Kwa kutotii amri BATILI kuliko ugeuzwe status kuitwa mfungwa/mtuhumiwa/muuaji na hatis haitokuacha ikiwa utamwaga damu ya watu.

HATA POLISI WANAPASWA TAMBUA KUWA HAWAPO SALAMA ANYTIME MSALA UTAKUPATA WATZ WAKIAMUA

utaicha familia kitaa Raia wanakusaidia mkeo.

Usiwe baba au mama mpumbavu.
Hii inamkumbusha jkt tulkua na afande mkuda alkua ananletea ukuda na chuki aisee......
Kuna rafiki yangu ni magereza alnpigia last month ananambia yule afande ni mfungwa wake saivi(Kuna Yuko walfanya)
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Wiki hii tumeshuhudia vijana 4 kati ya 6 waliofanya uhalifu wa kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakifikishwa mbele za Pontio Pilato na kusomewa mashtaka, ijapokuwa walikana kuhusika na kitendo hicho kibaya.
View attachment 3074754
Watuhumiwa 4 waliombaka na kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakiwa mahakamani

Jambo la kushangaza na ambalo watanzania wengi wanashindwa kupata majibu ni kwanini 'afande' aliyewatuma wale wahuni (na ambaye alisikika akiombwa msamaha na binti aliyekuwa akibakwa na kulawitiwa mubashara) hakamatwi? Swali la pili ni je, wale watuhumiwa 2 wa ulawiti waliobaki ni akina nani na kwanini hawakamatwi? Je, wana uhusiano wowote na huyo afande asiyekamatika? Hiki ndicho kitendawili ambacho watanzania wangependa kupata majibu yake.

Kabla ya kutoa majibu na kueleza kwanini afande hakamatiki, naomba nirejee kesi 2 zinazofanana na hii ya afande zilizowahi kufikishwa mahakamani na kugonga mwamba.

Kesi ya kwanza ni ile ya aliyekuwa kamanda wa upelelezi wa Dar es Salaam, ndugu Abdallah Zombe ambaye aliwatuma askari polisi kuwaua wafanyabiashara wa madini na kuwapora mamilioni ya fedha. Kwa ufupi, kesi ilipotinga mahakamani, wale askari waliotumwa kuua walijitetea kuwa walifanya mauaji yale kwa kutii amri ya mkubwa wao wa kazi, ndugu Zombe. Baada ya kesi kuunguruma kwa muda mrefu, huku wananchi wakidhani Zombe hachomoki kwenye kesi ile, hatimaye aliachiwa huru. Wale askari waliohusika na mchakato wa mauaji wakahuhumiwa vifungo vya maisha na kunyongwa. Lakini baadaye askari wale walikata rufaa na baadhi yao kufanikiwa kujichomoa. Aliyekutwa na hatia ni mmoja wao anayeitwa Bageni, ambaye alihukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Katika kesi hii kuna facts mbili za kisheria zilizotumika. Fact ya kwanza ni ile ya mtu mzima mwenye akili timamu kutumwa na mtu mwingine kutekeleza uhalifu. Sheria haimhukumu aliyetuma bali humhukumu mtumwaji, hata kama mtumaji anajulikana na yeye mwenyewe kukiri kuwa kweli aliwatuma. Ndio maana Zombe aliachiwa huru bila shuruti.

Fact ya pili katika kesi hii ni uhusika wa mtu binafsi katika kutenda uhalifu. Baadhi ya askari waliachiwa huru kwa kuwa hawakuhusika kuwapiga risasi wafanyabiashara. Aliyehusika kufyatua risasi na kuua ni mmoja tu, naye ni Bageni. Ndio maana askari wengine waliachiwa huru, akahukumiwa Bageni tu.

Turejee kwenye kesi ya pili iliyomhusu mke wa Bilionea Msuya kuwatuma watu kumuua wifi yake (mdogo wake bilionea Msuya). Mahakamani ilithibitika kweli mke wa bilionea Msuya aliwatuma watu kufanya uhalifu. Na pia kisu kilichotumika kufanya mauaji kilipatikana na alama za vidole za wahalifu. Lakini mahakama ilitumia busara za kisheria kuwaachia huru watuhimiwa wote, akiwemo mke wa Msuya. Kwanini? Kwa sababu mtumaji hana kosa kisheria. Pia hata kama fingerprints za wahalifu zilionekana kwenye kisu, hakuna mtu mwenye uhakika kama kweli wao ndio waliua. Umeona eeh?

Sasa turejee kwenye hoja yetu ya msingi. Kuna baadhi ya mitandao ya kijamii (sio JF) imemtaja na kumuonesha hadharani afande aliyewatuma wale wafiraji kumdhulumu binti wa watu haki yake ya msingi. Pia haiwezekani binti aliyedhulumiwa amuombe afande msamaha hadharani halafu polisi wasimuombe awapeleke nyumbani kwa afande ili wamkamate. Haiwezekani.

Ni wazi kwamba afande anajulikana isipokuwa hata kama atakamatwa hatakuwa na kesi ya kujibu, kwa kuzingatia mfano wa kesi mbili nilizozitaja hapo juu ambazo watumaji waliachiwa huru bila shuruti. Kwa hiyo, polisi wanaona hata kama wakiamua kumpeleka afande mahakamani wataambulia patupu. Illmradi wahalifu wamekamatwa, hakuna haja tena ya kusumbuka na afande kwa kuwa hata akipelekwa mahakamani, hana kesi ya kujibu.

Sheria inatambua kwamba mtu mzima unapotumwa kutenda uhalifu nawe ukakubali kufanya hivyo, sheria itakuangukia wewe uliyetenda uhalifu na wala sio mtu aliyekutuma. Kwa hiyo, watanzania, hasa wale msiojua sheria, tulizeni mumkari na muendelee kuwa watulivu wakati wabakaji na wafiraji waliohusika kumdhalilisha binti wa Yombo Dovya wakishughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Nawasilisha.
Thank you. This is well put (umeiweka vizuri sana) hata mm kuna jinsi sikuwa nimeeleza hizo kesi mbili now i understand. Ndio maana watu wengi wanawatukana mahakimu na majaji lakini ulivyo elezea ni kuwa hatujui sheria vizuri. Na pengine sheria zinahitaji kupitiwa vizuri ili hata mtuhumiwa wa kutuma aweze kupata naya adhabu, na ushahidi fulani uweze kumtia hatiani na si kumwacha huru. Manake hii sheria inaweza kuongeza wahalifu kwa kujua tu mwisho wa siku atakutwa hana hatia wakati tunajua alituma na kufadhili hayo mauji ama huo uhalifu. Thank you again.
 
Mimi sio mwanasheria lakini nafahamu mambo ya kisheria kidogo mkuu

Huhitaji kusema kuwa wewe siyo mwanasheria kwani andiko lako linaonyesha kabisa kuwa unajaribu kuandika kitu usicho na ujuzi nacho kabisa, na unapotosha sana.
 
Thank you. This is well put (umeiweka vizuri sana) hata mm kuna jinsi sikuwa nimeeleza hizo kesi mbili now i understand. Ndio maana watu wengi wanawatukana mahakimu na majaji lakini ulivyo elezea ni kuwa hatujui sheria vizuri. Na pengine sheria zinahitaji kupitiwa vizuri ili hata mtuhumiwa wa kutuma aweze kupata naya adhabu, na ushahidi fulani uweze kumtia hatiani na si kumwacha huru. Manake hii sheria inaweza kuongeza wahalifu kwa kujua tu mwisho wa siku atakutwa hana hatia wakati tunajua alituma na kufadhili hayo mauji ama huo uhalifu. Thank you again.
Alichoandika ni UONGO na mifano aliyotoa si sahihi,nashangaa unapomsifia kwa UONGO na UPOTOSHAJI,nadhani nimeweka clear Kesi ya Zombe,soma utaelewa sababu za Zombe kuachiwa na Bageni kuhukumiwa
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Wiki hii tumeshuhudia vijana 4 kati ya 6 waliofanya uhalifu wa kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakifikishwa mbele za Pontio Pilato na kusomewa mashtaka, ijapokuwa walikana kuhusika na kitendo hicho kibaya.
View attachment 3074754
Watuhumiwa 4 waliombaka na kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakiwa mahakamani

Jambo la kushangaza na ambalo watanzania wengi wanashindwa kupata majibu ni kwanini 'afande' aliyewatuma wale wahuni (na ambaye alisikika akiombwa msamaha na binti aliyekuwa akibakwa na kulawitiwa mubashara) hakamatwi? Swali la pili ni je, wale watuhumiwa 2 wa ulawiti waliobaki ni akina nani na kwanini hawakamatwi? Je, wana uhusiano wowote na huyo afande asiyekamatika? Hiki ndicho kitendawili ambacho watanzania wangependa kupata majibu yake.

Kabla ya kutoa majibu na kueleza kwanini afande hakamatiki, naomba nirejee kesi 2 zinazofanana na hii ya afande zilizowahi kufikishwa mahakamani na kugonga mwamba.

Kesi ya kwanza ni ile ya aliyekuwa kamanda wa upelelezi wa Dar es Salaam, ndugu Abdallah Zombe ambaye aliwatuma askari polisi kuwaua wafanyabiashara wa madini na kuwapora mamilioni ya fedha. Kwa ufupi, kesi ilipotinga mahakamani, wale askari waliotumwa kuua walijitetea kuwa walifanya mauaji yale kwa kutii amri ya mkubwa wao wa kazi, ndugu Zombe. Baada ya kesi kuunguruma kwa muda mrefu, huku wananchi wakidhani Zombe hachomoki kwenye kesi ile, hatimaye aliachiwa huru. Wale askari waliohusika na mchakato wa mauaji wakahuhumiwa vifungo vya maisha na kunyongwa. Lakini baadaye askari wale walikata rufaa na baadhi yao kufanikiwa kujichomoa. Aliyekutwa na hatia ni mmoja wao anayeitwa Bageni, ambaye alihukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Katika kesi hii kuna facts mbili za kisheria zilizotumika. Fact ya kwanza ni ile ya mtu mzima mwenye akili timamu kutumwa na mtu mwingine kutekeleza uhalifu. Sheria haimhukumu aliyetuma bali humhukumu mtumwaji, hata kama mtumaji anajulikana na yeye mwenyewe kukiri kuwa kweli aliwatuma. Ndio maana Zombe aliachiwa huru bila shuruti.

Fact ya pili katika kesi hii ni uhusika wa mtu binafsi katika kutenda uhalifu. Baadhi ya askari waliachiwa huru kwa kuwa hawakuhusika kuwapiga risasi wafanyabiashara. Aliyehusika kufyatua risasi na kuua ni mmoja tu, naye ni Bageni. Ndio maana askari wengine waliachiwa huru, akahukumiwa Bageni tu.

Turejee kwenye kesi ya pili iliyomhusu mke wa Bilionea Msuya kuwatuma watu kumuua wifi yake (mdogo wake bilionea Msuya). Mahakamani ilithibitika kweli mke wa bilionea Msuya aliwatuma watu kufanya uhalifu. Na pia kisu kilichotumika kufanya mauaji kilipatikana na alama za vidole za wahalifu. Lakini mahakama ilitumia busara za kisheria kuwaachia huru watuhimiwa wote, akiwemo mke wa Msuya. Kwanini? Kwa sababu mtumaji hana kosa kisheria. Pia hata kama fingerprints za wahalifu zilionekana kwenye kisu, hakuna mtu mwenye uhakika kama kweli wao ndio waliua. Umeona eeh?

Sasa turejee kwenye hoja yetu ya msingi. Kuna baadhi ya mitandao ya kijamii (sio JF) imemtaja na kumuonesha hadharani afande aliyewatuma wale wafiraji kumdhulumu binti wa watu haki yake ya msingi. Pia haiwezekani binti aliyedhulumiwa amuombe afande msamaha hadharani halafu polisi wasimuombe awapeleke nyumbani kwa afande ili wamkamate. Haiwezekani.

Ni wazi kwamba afande anajulikana isipokuwa hata kama atakamatwa hatakuwa na kesi ya kujibu, kwa kuzingatia mfano wa kesi mbili nilizozitaja hapo juu ambazo watumaji waliachiwa huru bila shuruti. Kwa hiyo, polisi wanaona hata kama wakiamua kumpeleka afande mahakamani wataambulia patupu. Illmradi wahalifu wamekamatwa, hakuna haja tena ya kusumbuka na afande kwa kuwa hata akipelekwa mahakamani, hana kesi ya kujibu.

Sheria inatambua kwamba mtu mzima unapotumwa kutenda uhalifu nawe ukakubali kufanya hivyo, sheria itakuangukia wewe uliyetenda uhalifu na wala sio mtu aliyekutuma. Kwa hiyo, watanzania, hasa wale msiojua sheria, tulizeni mumkari na muendelee kuwa watulivu wakati wabakaji na wafiraji waliohusika kumdhalilisha binti wa Yombo Dovya wakishughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Nawasilisha.
Kutafsiri sheria ni kazi ya mahakama, kwa hiyo watuhumiwa wote wanatakiwa kupelekwa mahakamani then mahakama yenyewe ndo itoe hukumu, siyo suala la polisi kutoa tafsiri halafu eti wajiamulie tu huyu kumpeleka sawa yule si sawa hapana hiyo siyo kazi yao
 
Endapo kulikuwa na mawasiliano yalifanyika kati yao kwa njia ya simu na ikabainika ni kweli aliwatuma, ana kesi ya kujibu…

Pia Kama binti aliyefanyiwa ukatili akaleta ushahidi unaoonyesha endapo aliwahi kupokea either vitisho na kweli alikuwa na mahusiano na mume wa huyo afande- ana kesi ya kujibu..
 
We useme tu aliewatuma ni mtu wao wanamlinda na sio porojo ulizoandika, kesi zote ulizo refer zimekuq na uonevu na ukakasi.

Swali, vijana wangerusha bomu kwrnye msafara wa kiongozi, polisi wasingetaka kujua master minder wa hiyo issue?

Acheni polojo, semeni tu aliewatuma ni mtu wao wanalindana
bush lawyer huyo
 
Tunafahamu hayo, tunafahamu hakuna uhakika wa kupatikana kwa ushahidi against “Afande” tunachotaka ni kila mhusika aliyehusika kwa namna moja au nyingine consequence imfikie.

Ukimshitaki mtu hata kama hukumu haitomtia hatiani kuna kitu unakuwa umempunguzia, ikiwemo reputation.

Usifikiri wanaopush hilo hawajui, Namna ya kupata haki haijanyooka, but in the end kila mtu aumizwe, tuumie wote ili tujifunze kutendeana kwa usahihi.

Tunaishi Africa.
Inawezekana hakuna mahala alipotajwa huyo mlengwa.
Mfano walotumwa wanakana kutumwa nae na nijuavyo mm hawawezi kukubali kumtaja kama kesi ishafika mahakamani.

Pia nadhani issue ya kumuunganisha moja kwa moja na kesi hiyo ndo ngumu(huu ni mtizamo wangu). Kama unashindwa kumuunganosha moja kwamoja kutokana na kukosa doti tayar ishakuwa mpasuko. Pia ninawasiwasi na sheria zetu katika kula njama kutenda kosa la ubakaji wa makundi.

Ila kama hajatajwa na watuhumiwa na wamemkana hata kama binti akisema mdo yeye hapo hapo hawezi ingia hatiani tena maana pale aliposema afande naomba msamaha inawezekana alikuwa anamwomba msamaha "nyundo" maana naye ni afande.

Hii kesi kunanamna flan ni nyepesi kwa watuhumiwa ila kutokanan na presha lazma waumie
 
Kwa maana hiyo, kufadhil ugaidi sio, kufadhili mauaji sio kosa, kufadhili uhaini siyo kosa au
Ni kosa ila tatizo kuthibisha hilo kosa mahakamani ndo kimbembe labda kama unataka tu kumsumbua mtu kwenda na kurudi mahakamani mwisho wa siku mahakama itamuachia huru tu
 
Hili ndo nilikuwa nasema watu wanataka watu wapandishwe kizimbani kwa mihemko tu hawajui mahakamani ni ushahidi usio shaka ndo unasimama, kwa hiii kesi kumkuta na hatia huyu mama ni kazi sana maana inabidi ueleze kinaga ubaga chain yake na hao watu na uthibitishe kuwa yeye aliwatuma jambo ambalo si rahisi. Hii dunia ya mitando ni ngumu sana kwenda nayo maana kila mtu ni mtaalam na hisia ni bora zaidi kuliko ukweli
Acha mbilinge, afande alitakiwa aunganishwe, kwa kesi simple kwakuwa ndiye aliombwa msamaha, ndiye alimuamuru kwenye pub yake, binti alikiri kutembea na mume wake...alitakiwa ajisafishe mashambani...hii issue tunaijua vizuri sana kabla hata kuonekana mtandaoni...
 
Back
Top Bottom