Sababu za msingi zinazopelekea 'afande' wa ulawiti asikamatwe ni hizi?

Yaani kumuachia mke wa Msuya ilikua busara???

Seriously??
 
Kwa hiyo nikimpa muuaji shoka langu mchana kweupe.Akaenda akampasua kichwa,kwamba atalisafisha,atanirudishia mchana kweupe.Kwamba kesho niendelee na shughuli zangu police watajuana na muuaji wao!
 
Upo hapa kutetea "mtumaji" wakati yeye ndio chanzo cha kila kitu na inatakiwa afungwe miaka mingi zaidi ya wengine wote?

Nchi hii ina tabaka mbili za sheria,za wananchi wa kawaida na wakubwa?
 
Kwahiyo ukimtuma mtu akatende kosa ww unakuwa huna kosa??

Sheria gan?... Hizo kesi ulizotaja ulizisoma na hiyk ndo ikawa Reason ya judgments hizo?

HIVI WALIMU SI TULIWAKATAZA KUCHAMBUA MAMBO YA KISHERIA??
 
Kwani mkuu mbona kuna washtakiwa wengine wameshtakiwa kwa kulanjsma na kupanga uhalifu na kwenye Tokio wanakuwa awapo?
Sasa unadhani kwanini Zombe na mke wa Msuya waliachiwa huru mkuu?
 
Mimi siizungumzii hii kesi ila nazungumzia hoja yako ya kesi ya kwanza, aidha unadanganya au huijui hiyo kesi vizuri na sababu za kuachiwa wake askari wengine na kuhukumiwa Bageni .

Ukweli ni huu kwanza uelewe katika majeshi yote duniani ukipewa order na mkubwa wako lazima uitekeleze hata kama amri hiyo haina busara, ukigoma kutekeleza ni usaliti na adhabu yake ni kuuliwa. Hii ni tofauti na uraiani ambako unaweza kukataa anri ya mkubwa wako na ukawa sakama kikazi.

Zombe kilichomsaidia akachomoka wakati ndiye aliyetia amri ni kuwa kwanza alikataa kuwa hakutoa order wale wafanyabiashara wauawe pili hakuwepo eneo la tukio. yule askari akiyefyatua risasi kuwaua wale wafanyabiashara wa madini alisaidiwa akatoroka hivyo shahidi muhimu hakuwepo mahakamani. Pili yule askari akiyechukua miili ya wale marehemu na kuipeleka hospitali mochwari alikufa kifo cha kuugua mahtuti akalazwa hospitali na kufia huko hivyo naye kama shahidi muhimu akawa hayupo. Askari wengine wadogo wakiachiwa kwa sababu hawakutajwa kufyatua risasi licha ya order kutolewa ya kuwaua wale wafanyabiashara japo hata kama wangetajwa wasingetiwa hatiani. Bageni kilichomtia hatiani ni kuwa yeye ndiye alikuwa kiongozi wa operesheni wadhifa wake alikuwa afisa upelekezi wa wilaya na ndiye aliyepokea amri kutoka kwa Zombe na yeye ilithibitika ndiye aliyetoa order kwa askari wa chini kuua wale marehemu. Kumbuka Zombe aliruka kutoa order wafanyabiashara wauawe hivyo msala ukamuangukia mkuu wa operesheni site ( Bageni), kama ingethibitika Zombe ndiye aliyetoa order Bageni asingetiwa hatiani hata kama ingethibitika ndiye aliyewaagiza askari wa chini kuua kwa sababu kijeshi aliyetoa order ndiye mwenye hatia sio mtekekezaji.


Ni vizuri jambo usilolijua usilisemee
 
Hivi ndivyo ninavyokumbuka.
 
Upo hapa kutetea "mtumaji" wakati yeye ndio chanzo cha kila kitu na inatakiwa afungwe miaka mingi zaidi ya wengine wote?

Nchi hii ina tabaka mbili za sheria,za wananchi wa kawaida na wakubwa?
Mkuu naomba ieleweke kwamba sio mm ninayetetea hili jambo bali lipo kwa mujibu wa sheria za nchi. Labda cha msingi ungemuomba mbunge wako apeleke muswada wa mabadiliko bungeni ili kipengele hiki cha sheria kirekebishwe.
 
Ulichokiandika sio kweli na wala sio sahihi. Nitafafanua hapa.

Kwa sheria za Tanzania (huenda ulimwenguni kote), jinai inamuhusu yoyote yule aliyetekeleza, aliyepanga, aliyeratibu, aliyeamrisha, aliyeshinikiza au aliyefadhili mpango wa uhalifu.

Hizo kesi zako zote ulizozitumia kama rejea hapo, hukumu zake zinaonyesha waendesha mashtaka walishindwa kuthibitisha bila shaka yoyote ile mbele yq mahakama kisheria kuwa hao watuhumiwa namna walivyohusika katika mpango wa jinai (yaani kutekeleza, kupanga, kuratibu, kufadhili, kushinikiza au kuamrisha uovu kufanyika).
 
Tanzania watu wanapenda sana kulindana hata ukifanya uchafu+ushenzi gani

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…