Dr isaya febu
Member
- Jan 17, 2023
- 40
- 294
Kuwahi Kumwaga:
Kuwahi kumwaga (kuwahi kufika kileleni) kwa mwanaume ni hali ambayo hutokea pale mwanaume anapopata mshindo (anapofika kileleni) mapema zaidi kuliko yeye au mwenza wake wanavyotarajia, mara nyingi ndani ya dakika chache baada ya kuanza tendo la ndoa.Tatizo hili hujulikana kwa kitaalamu kama premature ejaculation.
Hili ni tatizo linalowakumba wanaume wengi kwa nyakati tofauti za maisha yao jambo ambalo hupelekea kujisikia aibu mbele za wenzi wao pale wanaposhindwa kuendelea kabisa baada ya hali hii kutokea.
Sababu Za Kuwahi Kumwaga:
Tatizo hili husababishwa na mambo mbalimbali ya kisaikolojia, kibailojia, na mtindo wa maisha.A) Sababu Za Kisaikolojia:
Sababu za kisaikolojia zinazochangia tatizo hili ni pamoja na:1) Hofu Ya Kushindwa (Performance Anxiety).
Mwanaume anapokuwa na hofu ya kutomridhisha mwenzi wake, anaweza kujikuta akifikia mshindo haraka zaidi.2) Wasiwasi Wakati Wa Tendo La Ndoa.
Wasiwasi kuhusu utendaji wa tendo la ndoa unaweza kumfanya mwanaume amalize haraka bila kutarajia.Mwanaume akiwa na historia ya kupata hali hii kabla, huwa anapoteza kujiamini na kuwa na wasiwasi kwamba hali hiyo itatokea tena na matokeo yake husababisha kumaliza mapema (kuwahi kufika kileleni).
3) Msukumo Wa Kisaikolojia (Psychological Conditioning).
Ikiwa mwanaume amekuwa na tabia ya kufanya mapenzi kwa haraka (kwa mfano, katika mazingira yasiyo salama au ya haraka), mwili wake unaweza kuzoea kufika kileleni mapema.4) Msisimko Mkubwa Kupita Kiasi.
Ikiwa mwanaume ana msisimko mkubwa sana, hasa kwa mpenzi mpya au baada ya muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa, anaweza kuwahi kufika kileleni.5) Tabia Ya Kujichua Mara Kwa Mara (Masturbation).
Mara nyingi mwanaume anayejichua (kupiga punyeto) huwa anafanya haraka kwa kujificha ili asikutwe na mtu hivyo mwili wake unaweza kuzoea kufika kileleni haraka hata wakati wa tendo la ndoa.B) Sababu Za Kibailojia:
Sababu za kibailojia zinazochangia tatizo hili ni pamoja na:1) Mabadiliko Ya Homoni.
Kiwango cha chini cha serotonin (homoni inayodhibiti mshindo) kinaweza kufanya mwanaume amwage haraka zaidi.2) Magonjwa Au Matatizo Ya Kiafya.
Magonjwa kama vile kisukari, shinikizo la juu la damu, matatizo ya tezi dume, au matatizo ya mfumo wa neva yanaweza kuchangia hali hii.Magonjwa ya Mfumo wa Fahamu: Mfumo wa neva unadhibiti hisia na msisimko; ikiwa kuna hitilafu yoyote, inaweza kusababisha kumaliza mapema (kuwahi kufika kileleni).