Sababu za Raila kuyaeshimu maamuzi ya SC

Sababu za Raila kuyaeshimu maamuzi ya SC

Crucial Man

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2011
Posts
3,404
Reaction score
1,311
Nashawishika kusema kwamba Hon Raila Odinga Aliyajua maamuzi ya Sc hata kabla kutangazwa...

(1) vyombo vya habari vya kenya vilitangaza kwamba Raila angetoa speech punde tu baada ya hukumu,na kweli alifanya hivyo bila kuchelewa.

(2) ile speech yake ilikuwa imesha andaliwa mapema,ina maana alikuwa ameshajua maamuzi ya majaji hata kabla ya kusomwa,swali hapa ni.je mutunga na wenzake walimbrief kwamba maamuzi yao yatakuwa kinyume na matarajio yake?.

(3) asingeweza kupingana nayo kwa wakati ule,kwa sababu wafuasi wake wangeingia mtaani na kuandamana,kuanzia mombasa nairobi,kisumu,busia mpaka nyanza yote,na hapo mauaji yangetokea kwa sababu tayari police walikuwa wameshajiandaa.

(4)alikubali kukwepa mkono mrefu wa icc,ingeonekana yeye ni na wafuasi wake ni watu wapenda fujo,hili lingeashiria kwamba hata 207 kumbe yeye ndio alishababisha fujo.

Kwa hili nampongeza Hon Odinga kwa kuona mbali.Haya ni maoni yangu,natambua wazi kwamba mheshimiwa Odinga anavyokubali kwa wakenya wengi hadi sisi baadhi ya watanzania kumkubali,...Angesema tu kwamba sikubaliani na maamuzi ya mahakama basi kenye kungewaka moto.

Pia ameonyesha kwamba demokrasia ambayo ameipigania Kenya anaiheshimu na ndio maana aliamua kucool down,japo alikuwa na uwezo wa kuukataa maamuzi ya mahakama.

Hongera sana Rt Hon Raila Amolo Odinga.
 
Maamuzi ya Supreme Court mbona yalikuwa ni foregone conclusion?

Ile mahakama isingeweza kuthubutu hata kidogo kuamua uchaguzi urudiwe (licha ya huyo Uhuru kushindwa kupata idadi ya kura ambazo zingemuwezesha kushinda uchaguzi kwenye duru ya kwanza).

Wale majaji hawana na hawakuwa na ujasiri kwenda kinyume na matakwa ya establishment. Hata unanimity katika maamuzi yao iliakisi kwamba hakuna aliyekuwa tayari kuthubutu hata kutoa ki-dissension cha uongo na kweli.
 
Ni kweli mkuu nyani gabu..impunity na mlungula ulikuwa umeshachukua nafasi yake..kuna wengine humu walidiriki kusema eti hawakuwa tayari kuiona kenya ikiingia kwenye machafuko tena.nashindwa kuelewa kitu kimoja hapa..ina maana Odinga akishinda machafuko yanatokea? Kumbe kuna watu wako tayari kuingia msituni kama odinga angekuwa rais wa kenya?..hizi ndizo adhari za kuiaminisha jamii flani kwamba wao ndio the choosen one.
 
Maamuzi ya Supreme Court mbona yalikuwa ni foregone conclusion?

Ile mahakama isingeweza kuthubutu hata kidogo kuamua uchaguzi urudiwe (licha ya huyo Uhuru kushindwa kupata idadi ya kura ambazo zingemuwezesha kushinda uchaguzi kwenye duru ya kwanza).

Wale majaji hawana na hawakuwa na ujasiri kwenda kinyume na matakwa ya establishment. Hata unanimity katika maamuzi yao iliakisi kwamba hakuna aliyekuwa tayari kuthubutu hata kutoa ki-dissension cha uongo na kweli.

mkuu nyakua ka like kangu haka..natumia ka simu ka mchina ningekugongea like mia na hamsa
 
Back
Top Bottom