Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Kumekuwa na hisia tofauti kufuatia Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kuahirisha kulivunja Baraza la Wawakilishi jana Juni 23, 2025 na kusogeza hadi Agosti 13, 2025 akisema ni kutokana na matayarisho ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025.
Baadhi ya wachambuzi wameihusisha hatua hiyo na mareklebisho ya mifumo ya uchaguzi inayolalamikiwa na vyama vya upinzani nchini, jambo ambalo bado halijawekwa wazi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Akihutubia Baraza la Wawakilishi Juni 23, Rais Mwinyi alitaja kifungu cha 91 (2A) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kuwa sababu ya kusogeza mbele kulivunja baraza hilo.
Pia, Soma: Dkt. Mwinyi atangaza kulivunja Baraza la Wawakilishi Agosti 13
Kifungu hicho kinasema: "Rais hatakuwa na uwezo wakati wowote wa kulivunja Baraza la Wawakilishi isipokuwa tu: kama Baraza la Wawakilishi limemaliza uhai wake kwa mujibu wa kifungu cha 92 cha Katiba."
Kifungu cha 92.(1) kinasema, "Maisha ya Baraza la Wawakilishi yataendelea kwa muda wa miaka mitano tangu tarehe ile ulipoitishwa Mkutano wake wa kwanza baada ya kuundwa, ila tu pale iwapo Baraza la Wawakilishi limevunjwa mapema kutokana na sababu mbali mbali zilizoelezwa katika Katiba hii."
Baraza limeshavunjwa?
Licha ya Rais kusogeza muda mbele wa kulivunja Baraza hilo, mmoja wa waandishi wa habari anayeripoti habari baraza ambaye ameomba kutotajwa jina, amesema kimsingi limeshavunjwa kwani shughuli zote zimeshakamilika.
"Mijadala yote ya bajeti imeshakamilika na hata Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla alishahutubia kuhitimisha shughuli za Serikali. Baada ya kuhitibisha barazani walikwenda kufanya tafrija ya kuagana, kwa hiyo hatutarajii kuona vikao vingine," amesema.
Mwandishi huyo anaona hatua hiyo imefikiwa ili kukidhi haja ya ibara ya 90.(1) ya Katiba ya Zabnzibar inayosema, "Wakati Baraza litakapovunjwa, Uchaguzi Mkuu wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi utafanywa na mkutano wa mwanzo wa Baraza jipya utafanywa si zaidi ya siku tisini toka kuvunjwa kwa Baraza."
"Endapo Rais Mwinyi angelivunja baraza Juni 23, siku 90 zingeangukia Septemba 23 wakati ambao hata uchaguzi mkuu utakuwa haujafanyika, hivyo amesogeza ili hizo siku zifike uchaguzi ukiwa umeshakamilika," amesema.
Kuhusu kuwepo kwa maboresho ya mifumo ya uchaguzi kama wanavyolalamikia wapinzani, mwandishi huyo amesema, "Kama Serikali itataka kufanya mabadiliko yoyote ya sharia za uchaguzi, Baraza inaweza kuitwa wakati wowote kabla ya kuvunjwa Agosti 13."
Hata hivyo, mchambuzi wa siasa, Bubelwa Kaiza amesema hatua hiyo inaashiria kuwepo kwa mabadiliko ya sheria za uchaguzi, japo haijathibitishwa.
"Ninadhani kuna mabadiliko kwenye sheria na hata Katiba yanayokusudiwa kuletwa na Serikali Barazani kabla ya Baraza kuvunjwa," amesema.
Kwa upande mwingine, hakujawa na taarifa ya mabadiliko ya kuvunjwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano linalotarajia kuvunjwa Juni 27, 2025 na Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa mujibu wa ratiba ya CCM, kura za maoni zinatarajiwa kuanza Juni 28 baada ya Bunge kuvunjwa.