OMOYOGWANE
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 4,701
- 11,920
Wakuu mpo!
OMOYOGWANE sipoi, wengi wameshangaa sana kuona kocha wa KMC anaacha kazi na kujiunga Yanga katika nafasi ambayo siyo ya ukocha mkuu wala kocha msaidizi ila kapewa kazi ya kuwa mkurugenzi wa Ufundi.
MAJUKUMU YA MKURUGENZI WA UFUNDI NI YAPI?
Mkurugenzi wa ufundi kazi yake ni kuandaa programu maalum kwaajili ya kuimarisha kiwango cha mchezaji mmoja mmoja ktk timu mfano Mzize anapoteza nafasi nyingi za wazi unakuta kauvuka msitu wa mabeki kisha kabaki yeye na kipa ktk kupiga mpira kapiga vibaya kapaisha usawa wa kimo cha mnazi, sasa kazi ya mkurugenzi wa ufundi ni kuandaa programu maalum kwa mzize ya kumfua na kumpa mbinu za kiufundi ili aweze kufunga kwa kila nafasi atakayo pata
Kazi ya mkurugenzi wa ufundi ni kuandaa program maalum ktk tumu ya vijana ili kuibua vipaji
Kulishauri benchi la ufundi (kocha mkuu na kocha msaidizi)
Kusimamia nidhamu ya mchezaji mmoja mmoja kwa kumpa elimu ya kisaikolojia ili kuyamudu mazingira ya ndani na nje ya uwanja mfano kejeli mitandaoni
Kufanya vetting ktk usajili wa wachezaji wapya wanao endana na falsafa ya tumu
KWANINI YANGA WAMMEMUAJILI MOALIN?
Moalin amekuwa kiwanda cha kuibua vipaji vingi kila anapopita kuanzia AZAM mpaka KMC, kila msimu KMC inaibua vipaji vipya nadhani sihitaji kutoa maelezo mengi si mnamuona Awesu, Lanso, Salim na wengine wengi
Falsafa ya mpira anaofundisha ndio falsafa ya Yanga, soka safi pasi nyingi hamna butua butua. Si mnaiona KMC mpira inaocheza.
Anajicho la kuibua vipaji
Tutegemee vipaji vingi msimu hu kutoka YANGA SC
Viva Moalin viva Yanga
Nawasilisha.