Sababu zinazokufanya usipungue ingawa unafanya mazoezi

Sababu zinazokufanya usipungue ingawa unafanya mazoezi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
=> Vyakula unavyokula hubeba 80% ya mapambano ya kupunguza uzito. Kula vyakula vya wanga kama viazi, wali na ugali siku ambazo utafanya kazi au mazoezi magumu tu ili kutoongeza uzito/unene.

=> Ikiwa umepanga vizuri aina ya vyakula unavyopaswa kula ili kupunguza uzito na bado haupungui tu, basi uwezekano ni mkubwa kuwa unakula kupita kiasi.

=> Unafanya mazoezi yasiyostahili mfano cardio kwa muda mrefu bila kubadilisha. Kufanya mazoezi haya kwa zaidi ya dakika 90 husababisha kuliwa kwa misuli muhimu inayoongeza kasi ya umetaboli.


Chanzo: TibaFasta
 
Chakula Chakula Chakula hapo ndio kiini cha kupungua au la
 
hakuna kitu kinaudhi kama unapungua then ukiacha diet mwili unarudi pale pale au unaongezeka zaidi
 
Kupunguza mwili kwa baadhi ya watu si tatizo maana kunawale wana ita diet ya kifo ka sijakosea yani mtua anaamkia maji anashindia majia analalia maji njaa ikimuuma anavumilia na ni kweli anapungua kwa haraka sana ila ni hatari kiafya, changamoto inakuwa ni kubakia pale mtu atakapo kubaki mfano kuwa mwembamba baada ya kupunguza unene.

Ila mie mimejifunza mengi katika nutrition na mengi kuhusiana na afya kitu chakwanza kiongezacho unene ni vyakula hasa wanga kupita kiasi na sukari nyingi ukiwa na namna ya kuacha sukari na kuacha wanga utapungua kwa haraka ila katika kiwango ambacho si hatari kiafya ila ukifika katika size uonayo yafaa ndo unakula vyakula vya protein, mboga, na matunda kiasi yenye sukari pia unaongeza kiasi cha wanga ila si kwa wingia ambako kutakupelekea kwenye kuongezeka uzito tena, mfano unaweza kula ugali kwa mara mbili kwa wiki mpaka tatu.
 
hakuna kitu kinaudhi kama unapungua then ukiacha diet mwili unarudi pale pale au unaongezeka zaidi
kikubwa yapaswa kujua kitugani kinakufanya uzito kuongezeka, then ndo unapunguza kwa kiasi kikubwa mfano wanga hufanya watu kunenepa sana na sukari, ila kunawale wenye miili ya kupambana na vyakula hivyo anaweza kula kwa wingi ila mwili ukawa vile vile
 
Asante miss zomboko hivi kuna uhusiano gani kati ya mwanamke anayezaa kupitia operesheni na unene maana akina dada wengi waliofanyiwa operesheni wanafumuka fumuuuuu
 
Tupeane diet ya kupunguza usavimbi huu basi
Ni hivi ni kupunguza kuzalisha insulin wakati woto kwakupunguza kula marakwa mara mfano saa 12 asubuhi, saa 4, saa 6, saa 10 saa 2 usiku, pia kupunguza vyakula vya sukari na wanga japo ni vigumu sana ila ndiyo naamna yenyewe
 
kikubwa yapaswa kujua kitugani kinakufanya uzito kuongezeka, then ndo unapunguza kwa kiasi kikubwa mfano wanga hufanya watu kunenepa sana na sukari, ila kunawale wenye miili ya kupambana na vyakula hivyo anaweza kula kwa wingi ila mwili ukawa vile vile
Nimejitahidi kuacha wanga naona napungua kiasi
 
Huku kwetu msosi mchana dona usiku wali sasa nafanyaje mwenzenu?
 
simara jaribu kula asubuhi halafu mlo unaofuata kula saa tisa jioni,ikifika saa mbili usiku kunywa chai tu ulale,mwanzoni itakuwa ngumu lakini kadiri unavyo zoea unazoea tu utaona ni kawaida,mimi binafsi ni legend kwa mazoezi nikitaka kunenepa naamua tu nikitaka kupungua naamua tu mwenyewe ,mara nyingi watu mabonge wanapenda sana kula kula akiona karanga letee akiona juice letee akiona mihogo letee unakuta muda wote ni kula yaani ni fujooo mtindo mmoja lazima uwe mkatili kidogo
 
Dawa ya kupungua ni kula sana vyakula aina za mimea, achana na mikate. Mihogo, viazi, matunda mbogamboga na karanga korosho maharage ndizi dona
 
Epuka Soda, epuka kula sana vyakula vya wanga kama mawali wali, Product za ngano kama mikate, machapati, maandazi n.k ..wengi wanafanya mazoezi na hawaoungua kwa sababu mtu anakimbia anaunguza 200 calories akimaliza mazoezi abadaka mili 500 ya soda na sahani ndii ya wali anagonga anaongeza 300 calories
 
Back
Top Bottom